Wewe Chizi (kifupi cha
Chizi Maarifa ) huna maarifa yoyote!!
Unajuwa kitu inaitwa colonization of mind!!
Kwanza lazima uwaze hao mafarao walikuwa na historia ipi!? Ambayo mwanao akiijuwa as black atajiamini kuwa hata blacks wanauwezo!!
Wazungu kuvunja zile pua kwenye pharaonic statues na kuanzisha madai kuwa farao alikuwa mzungu sio wapumbau !!
Mara moja moja tumia kichwa kufikiri!!!
Tafuta kitabu kinaitwa [HASHTAG]#African[/HASHTAG] saga by willium Dubois
Sisi waafrika tuna majanga makubwa sanamkuu,hatujui kuwa kama leo wakisema ukweli kuwa Wamisri walikuwa weusi hii itakuwa na maana kwamba mtu mweusi aliwahi kuitawala dunia kupitia Egypt Empire na hii itamuinua kiroho [siyo kidini] na kimwili kwa kiwango kikubwa sana.....
Hilo haliishii hapo bali litapelekea safari nyingine kubwa kabisa ya kuufunua ukweli wa kutisha kuwa Yesu na Waisraeli walikuwa weusi kwasababu kuu mbili za haraka haraka...
1;Isingewezekana Yesu mweupe [kama wao wanavyotaka watu waamini] aende akajifiche katikati ya watu weupe wakati Herode akimtafuta amuuwe yeye na wazazi wake weupe...
2;Haiwezekani ndugu zake Yusuph washindwe kumtambua nduigu yao ambaye ni mweupe [kama wao wanavyotaka sisi tuamini] wakati wameenda Misri kufuata chakula wakati wa njaa iliyoikumba dunia wakati ule...
Jambo hili ni pigo kubwa sana maana litakwenda hadi kuwafanya Waisraeli kuwa siyo hawa tunaowajua leo bali ni wengine kabisa na ni miongoni mwa watu weusi,hii ni hasara ya hatari kabisa ambayo watu walioamua kuudanganya ulimwengu hawatataka kukubali kabisa itokee....
Ikishakuwa hivi fikiria tu ni kwa namna ipi mtu mweusi atapata nguvu za ndanbi na nje?
Ngoja niseme jambo moja kubwa....
Ili uweze kumtawala mtu ni lazima umfanye awe duni kuanzia ndani yake hadi nje.Sisi watu weusi tupo namna hii,tunaamini tulilaaniwa kutoka kwenye kizazi cha Nuhu,tunaamini hakuna chema hata kimoja tulichowahi kukifanya hapa duniani kwasababu tunaamini sisi ni watu tusiokuwa na akili kabisa.Haya na mengine mengi yametufanya tuwe hivi leo,tunajidharau hatujipendi kabisa....
Hii na nyingine ni mipango maalum kwaajili ya kumtawala mtu mweusi na hata alichokisema Donald Trump kwenye kampeni kuhusu mtu mweusi ni muendelezo tu wa harakati zile zile za zamani sana....
Unaweza kujiuliza ni kwanini mtu mweusi ashambuliwe namna hii kila kona ya dunia? Kwanini yeye tu aonekane duni? kwanini bara la mtu mweusi ndilo lionekane duni zaidi kuliko yote?
Kimsingi mtu unayemuogopa na kumuona bora mara nyingi utakuwa unamtengenezea majungu ya kila aina,ukiangalia hata mitaani kwetu wale ambao wamefanikiwa ndiyo wanatangazwa kuwa na tabia mbayambaya bila ushahidi wowote,mabinti wazuri husemwa wanaringa n.k.Haya yote hayawafuati hawa kwa bahati mbaya bali ubora wao ndiyo unawafanya watu wawaogope na kusababisha waanze kushambuliwa....
Mtu mweusi ndiyo binadamu bora kabisa na wanajua kabisa akipata nguvu zake za asili hakuna ambaye atasimama mbele yake,jambo hili dunia haitaki kabisa lkitokee na ndiyo maana historia yake inafichwa maana itamrudishia nguvu zake za nje na ndani....
Leo ikijulikana kuwa Misri ya kale ilikuwa yua mtu mweusi...
Leo ikijulikana kuwa Yesu alikuwa mweusi...
Leo ikajulikana kuwa Waisraeli walikuwa weusi....
Leo ikijulikana kuwa mwanadamu wa kwanza kwa maana ya Adam alikuwa mweusi...
N.k n.k,unadhani ni kwa kiwango kipi dunia itabadilika kabisa na kuanza kumuona mtu mweusi katika namna nyingine kabisa?
Halafu mtu anakuja hapa anaponda tu eti mtu kuhoji suala hili ni ujinga,sijui nani mjinga hapa kati ya anayeitafuta historia yake akitaka kujijua na yule anayetaka kwenda kikondoo tu.....