Je, funga ya Waislamu ni kula na kunywa tu?

Je, funga ya Waislamu ni kula na kunywa tu?

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Baada ya kuandika post ambayo ilikuwa inahusiana na Dhana ya Futari na Daku kumeibuka maswali mengi na kashfa nyingi kuhusiana na funga ya Waislamu kwamba, wamebadili ratiba ya kula,mara sijui wanakula usiku mzima na bla bla bla nyingine kibao.

Sasa Jamiiforums ni jukwaa la elimu na maarifa hivyo nikaona si vibaya nikaja na post nyingine ili tutoane ukungu kwenye bongo zetu.

Kwahiyo tutaona nini maana ya Swaumu/ funga na lengo lake.

Maana ya Swaumu (Funga)

Kilugha; neno “Swaum” lina maana ya kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa nabii Isa (A.S) alijizuilia (alikuwa katika Swaum ya) kutosema na mtu yoyote juu ya mtoto wake.

“... Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: `Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya Swaum (kufunga), kwa hiyo leo sitasema na mtu’” (19:2 6).

Katika Sharia ya Kiislamu kufunga (Swaum) ni kujizuilia kula, kunywa, kujamii, kuingiza kitu chochote katika matundu ya mwili na kujizuilia kumuasi Allah (S.W) kuanzia alfajiri ya kweli mpaka kuingia ma gharibi.

Lengo la Swaumu

Lengo la Swaum katika Uislamu ni kumuwezesha mja awe mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Hivyo, ili lengo hili litimie mfungaji pamoja na kujizuilia kula, kunywa, kujamii, hanabudi pia kujizuilia na kitendo chochote kitakachompelekea kuvunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w).

Kwa maana nyingine, ili Swaum ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, mfungaji hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu pamoja na fikra na hisia zake -na matendo aliyoyakataza Allah (s.w.).

Funga ya macho ni kujizuilia kutazama yale yote aliyoyakataza Allah (s.w), funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w), kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana n.k, funga ya masikio ni kujizuilia kusikiliza yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w); funga ya miguu ni kujizuilia kuendea yale yote aliyotukataza Allah (s.w); funga ya fikra na hisia, ni kujizuilia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea mja kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith zifuatazo:

“Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuw a anaacha chakula chake na kinyw aji chake - ( Allah (s.w) hana haja na funga yake). (Bukhari).

Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema; Ni wangapi wamefunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu, ni wangapi wanaoswali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).

Hadith hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuilia na maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.

Naona mpaka hapo tutakuwa tumepata faida ya kujua funga na makusudio yake

Ni hayo tu!
 
We elewa kwamba kipindi cha Kwaresma bei za vyakula inashuka na kipindi cha Ramadhani bei inapanda.
 
We elewa kwamba kipindi cha Kwaresma bei za vyakula inashuka na kipindi cha Ramadhani bei inapanda.
Kwahiyo hiyo ndio ishu!

Jibu liko wazi funga ya Ramadhani ni maarufu kuliko kwaresma na INA mwitiko mkubwa Sana kuliko kwaresma.

Kwahiyo bilashaka hiyo ni fursa Kwa wafanyabiashara kutaka kupata faida zaidi ingawa inawaumiza walengwa ambao ni wafungaji
 
Kwahiyo hiyo ndio ishu...
Bidhaa hupanda bei kama uhitaji ni mkubwa kuliko upatikanaji.

Kipindi cha Ramdhani demand inaongezeka kwa maana ulaji wa vyakula unaongezeka kuliko kipindi cha kawaida.

Waulize wapishi majumbami watakujuza ni kipindi gani wanapika Sana utagundua kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu ndio wanapika Sana na wengi hasa Wafanyakazi wa majumbami hawakipendi kipindi hiki kwa kuwa kazi za kupika zinaongezeka maradufu siku nzima inakua maandalizi ya kupika kupika na kufanya usafi hasa wa vyombo vingi.

Tupunguze kula kipindi cha mfungo ili demand na supply ziendelea kuwa kama kipindi kisicho cha mfungo na bei iwe kawaida.
 
Kula kwingi unakosema wala sioni uhalisia wake, maana tutakula mara mbili Tu wakti WA kufungua na Kula Daku

Labda useme wakati WA ramadhani kuna udambwi udambwi mwingi, hapa sambusa, kachori, katlesi, na ghasia nyingine nyingi Tu Bila Kusahau mapishi ya nazi Kwa Sana.

Uwingi unakuja katika upishi WA Aina mbali mbali za vyakula lakini si eti kwamba tunakula Sana laa!
 
Kula kwingi unakosema wala sioni uhalisia wake, maana tutakula mara mbili Tu wakti WA kufungua na Kula Daku

Labda useme wakati WA ramadhani kuna udambwi udambwi mwingi,hapa sambusa,kachori,katlesi, na ghasia nyingine nyingi Tu Bila Kusahau mapishi ya nazi Kwa Sana.

Uwingi unakuja katika upishi WA Aina mbali mbali za vyakula lakini si eti kwamba tunakula Sana laa!a
Kabla ya Ramadhani kula ni mara tatu na bei haipandi. Twambie kwa nini kula mara mbili kunapandisha bei.
 
Kabla ya Ramadhani kula ni mara tatu na bei haipandi. Twambie kwa nini kula mara mbili kunapandisha bei.
Chief

Kama ilivyo wakati WA sikukuu mbali mbali ziwe x-mas ,Eid au pasaka Kwa kawaida wafanyabiashara huona kama hii ni fursa ya kupata faida zaidi.

The same Kwa ramadhamani wafungaji ni wengi Sana kwasababu waislamu Wana mwitikio mkubwa WA kutekeleza ibada hii,kwahiyo wafanyabiashara wanatumia huu mwanya kupata faida zaidi.

Nadhani Jambo liko wazi kabisa hauhitaji hata mchumi kuliona hili
 
Itaadimika kwasababu wakristo watakuwa. Hawana kampani ya Kula mdudu
Kwamba bila waislamu wakristo hawawezi kula mdudu?

Mbona hoja yako haina mashiko!

Yaani mlaji wa kitimoto aache kula kitimoto kisa Abdallah/Juma amefunga !
 
Kula kwingi unakosema wala sioni uhalisia wake, maana tutakula mara mbili Tu wakti WA kufungua na Kula Daku

Labda useme wakati WA ramadhani kuna udambwi udambwi mwingi,hapa sambusa,kachori,katlesi, na ghasia nyingine nyingi Tu Bila Kusahau mapishi ya nazi Kwa Sana.

Uwingi unakuja katika upishi WA Aina mbali mbali za vyakula lakini si eti kwamba tunakula Sana laa!
Sasa huo udambwi udambwi si ndio wingi wenyewe mkuu!

Unajicontradict wewe mwenyewe.
 
Kwamba bila waislamu wakristo hawawezi kula mdudu?

Mbona hoja yako haina mashiko!

Yaani mlaji wa kitimoto aache kula kitimoto kisa Abdallah/Juma amefunga !
Chief

Wewe ndio umedandia mwendo Kasi Kwa mbele!

Mdudu huwa anapatikana kwenye moja baridi na moja Moto, sasa Akina Ahmed na ahmet kipindi cha ramadhani huwa hawaendi hayo maeneo,kwahiyo Akina John na Joseph hukosa kampani ya kwenda huko na hivyo mdudu hukosa soko
 
Hivi kwanini sehemu yenye waislamu wengi kama zenji wanakataza watu kula hadharani wakati wa ramadhani ?

Kwani kufunga ni lazima au hiyari ?
 
Si kweli.

Ingekuwa kweli yale maeneo yenye mdudu pekee bila kimea/bia yangekuwa yanauza wakati wa ramadhani.
 
Hivi kwanini sehemu yenye waislamu wengi kama zenji wanakataza watu kula hadharani wakati wa ramadhani ?

Kwani kufunga ni lazima au hiyari ?
Lengo ni kuuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani
 
La hasha.

Bali tukubaliane tu kuwa wakati wa ramadhani watu wanakula zaidi kwa sababu uhitaji wa vyakula fulani unaongezeka.
Nadhani unamajibu yako binafsi, anyways sio kesi ishi nayo hayo
 
Back
Top Bottom