ASIWAJU
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 1,938
- 1,632
Je, heshima ina lazimishwa ?Lengo ni kuuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je, heshima ina lazimishwa ?Lengo ni kuuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani
Ili iweje!?..unawanunulia wewe chakula!?Bidhaa hupanda bei kama uhitaji ni mkubwa kuliko upatikanaji.
Kipindi cha Ramdhani demand inaongezeka kwa maana ulaji wa vyakula unaongezeka kuliko kipindi cha kawaida.
Waulize wapishi majumbami watakujuza ni kipindi gani wanapika Sana utagundua kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu ndio wanapika Sana na wengi hasa Wafanyakazi wa majumbami hawakipendi kipindi hiki kwa kuwa kazi za kupika zinaongezeka maradufu siku nzima inakua maandalizi ya kupika kupika na kufanya usafi hasa wa vyombo vingi.
Tupunguze kula kipindi cha mfungo ili demand na supply ziendelea kuwa kama kipindi kisicho cha mfungo na bei iwe kawaida.
Kama una watoto jiulize huwa unawalazimisha wakugeshimu au wanahiyari!?...yaani wanakuheshimu kwa kuwa unawapa mahitaji muhimu au wanakuheshimu kwa kuwa wanatakiwa kukuheshimu,wasipokuheshimu utachukua hatua gani?Je, heshima ina lazimishwa ?
Swali nililo uliza kutokana na maelezo ya mleta mada na maswali yako kuna uwiano wowote ?Kama una watoto jiulize huwa unawalazimisha wakugeshimu au wanahiyari!?...yaani wanakuheshimu kwa kuwa unawapa mahitaji muhimu au wanakuheshimu kwa kuwa wanatakiwa kukuheshimu,wasipokuheshimu utachukua hatua gani?
Keyword 'heshima'Swali nililo uliza kutokana na maelezo ya mleta mada na maswali yako kuna uwiano wowote ?
Iliyo jikita kwenye nini ?Keyword 'heshima'
Heshima Haina pa kujikita,inajitegemeaIliyo jikita kwenye nini ?
Upo nje ya swali la mwanzo, usiku mwema.Heshima Haina pa kujikita,inajitegemea
safi sana mwalimu wengi tume kufahamu ila wachache tu wakina miujiza kawada yao kujitoa akiliBaada ya kuandika post ambayo ilikuwa inahusiana na Dhana ya Futari na Daku kumeibuka maswali mengi na kashfa nyingi kuhusiana na funga ya Waislamu kwamba, wamebadili ratiba ya kula,mara sijui wanakula usiku mzima na bla bla bla nyingine kibao.
Sasa Jamiiforums ni jukwaa la elimu na maarifa hivyo nikaona si vibaya nikaja na post nyingine ili tutoane ukungu kwenye bongo zetu.
Kwahiyo tutaona nini maana ya Swaumu/ funga na lengo lake.
Maana ya Swaumu (Funga)
Kilugha; neno “Swaum” lina maana ya kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa nabii Isa (A.S) alijizuilia (alikuwa katika Swaum ya) kutosema na mtu yoyote juu ya mtoto wake.
“... Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: `Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya Swaum (kufunga), kwa hiyo leo sitasema na mtu’” (19:2 6).
Katika Sharia ya Kiislamu kufunga (Swaum) ni kujizuilia kula, kunywa, kujamii, kuingiza kitu chochote katika matundu ya mwili na kujizuilia kumuasi Allah (S.W) kuanzia alfajiri ya kweli mpaka kuingia ma gharibi.
Lengo la Swaumu
Lengo la Swaum katika Uislamu ni kumuwezesha mja awe mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Hivyo, ili lengo hili litimie mfungaji pamoja na kujizuilia kula, kunywa, kujamii, hanabudi pia kujizuilia na kitendo chochote kitakachompelekea kuvunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w).
Kwa maana nyingine, ili Swaum ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, mfungaji hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu pamoja na fikra na hisia zake -na matendo aliyoyakataza Allah (s.w.).
Funga ya macho ni kujizuilia kutazama yale yote aliyoyakataza Allah (s.w), funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w), kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana n.k, funga ya masikio ni kujizuilia kusikiliza yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w); funga ya miguu ni kujizuilia kuendea yale yote aliyotukataza Allah (s.w); funga ya fikra na hisia, ni kujizuilia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea mja kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith zifuatazo:
“Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuw a anaacha chakula chake na kinyw aji chake - ( Allah (s.w) hana haja na funga yake). (Bukhari).
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema; Ni wangapi wamefunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu, ni wangapi wanaoswali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).
Hadith hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuilia na maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.
Naona mpaka hapo tutakuwa tumepata faida ya kujua funga na makusudio yake
Ni hayo tu!
huo ni msimu wakulima wa mihogo magimbi viazi wamesubilia mfungo kupiga hela hacha watu wanufaike uapo sema watu wanakula sana wafungaji hata wakala si wanakula .hela yaoBidhaa hupanda bei kama uhitaji ni mkubwa kuliko upatikanaji.
Kipindi cha Ramdhani demand inaongezeka kwa maana ulaji wa vyakula unaongezeka kuliko kipindi cha kawaida.
Waulize wapishi majumbami watakujuza ni kipindi gani wanapika Sana utagundua kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu ndio wanapika Sana na wengi hasa Wafanyakazi wa majumbami hawakipendi kipindi hiki kwa kuwa kazi za kupika zinaongezeka maradufu siku nzima inakua maandalizi ya kupika kupika na kufanya usafi hasa wa vyombo vingi.
Tupunguze kula kipindi cha mfungo ili demand na supply ziendelea kuwa kama kipindi kisicho cha mfungo na bei iwe kawaida.
nunua maitaji kabla uweke ndaniKabla ya Ramadhani kula ni mara tatu na bei haipandi. Twambie kwa nini kula mara mbili kunapandisha bei.
[emoji120]Chief
Kama ilivyo wakati WA sikukuu mbali mbali ziwe x-mas ,Eid au pasaka Kwa kawaida wafanyabiashara huona kama hii ni fursa ya kupata faida zaidi.
The same Kwa ramadhamani wafungaji ni wengi Sana kwasababu waislamu Wana mwitikio mkubwa WA kutekeleza ibada hii,kwahiyo wafanyabiashara wanatumia huu mwanya kupata faida zaidi.
Nadhani Jambo liko wazi kabisa hauhitaji hata mchumi kuliona hili
Ukweli ni kwamba mfungo wa Ramadan ni sherehe ya kulaMokiti swali lako limejibiwa huku
Kwahiyo hiyo ndio ishu!
Jibu liko wazi funga ya Ramadhani ni maarufu kuliko kwaresma na INA mwitiko mkubwa Sana kuliko kwaresma.
Kwahiyo bilashaka hiyo ni fursa Kwa wafanyabiashara kutaka kupata faida zaidi ingawa inawaumiza walengwa ambao ni wafungaji
Ukweli ni kwamba mfungo wa Ramadan ni sherehe ya kula
Ndio maana uitaji wa chakula unakuwa mkubwa mno na price inapanda , ni kama waislamu wanashindana na sikuu za Christmas wanavyo waona wakristo mwezi mzima wanasherehekea ,
waislamu mwezi wa Ramadan wanachukua likizo makazini wanaingia kwenye madeni makubwa kisa kula sana
Shida kubwa inakuja kuvimbiwa chakula Cha kula usiku saa 10 tena umeshindilia Sana ili usisikie njaa mchana , ukikutana akicheua mavimbizi ni hatari
MashaaAllahBaada ya kuandika post ambayo ilikuwa inahusiana na Dhana ya Futari na Daku kumeibuka maswali mengi na kashfa nyingi kuhusiana na funga ya Waislamu kwamba, wamebadili ratiba ya kula,mara sijui wanakula usiku mzima na bla bla bla nyingine kibao.