Je, funga ya Waislamu ni kula na kunywa tu?

Je, funga ya Waislamu ni kula na kunywa tu?

Eating festival sherehe ya kula ramadhani inaendeleaje?
 
Ni kuchagua tu timing ya kula,unafunga Halafu unamnunia asiyefunga, halafu usiku unaamka kula? Nikifunga siku arobaini, Ni uji tu ndiyo unaingia kinywani mwangu
 
Baada ya kuandika post ambayo ilikuwa inahusiana na Dhana ya Futari na Daku kumeibuka maswali mengi na kashfa nyingi kuhusiana na funga ya Waislamu kwamba, wamebadili ratiba ya kula,mara sijui wanakula usiku mzima na bla bla bla nyingine kibao.

Sasa Jamiiforums ni jukwaa la elimu na maarifa hivyo nikaona si vibaya nikaja na post nyingine ili tutoane ukungu kwenye bongo zetu.

Kwahiyo tutaona nini maana ya Swaumu/ funga na lengo lake.

Maana ya Swaumu (Funga)

Kilugha; neno “Swaum” lina maana ya kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa nabii Isa (A.S) alijizuilia (alikuwa katika Swaum ya) kutosema na mtu yoyote juu ya mtoto wake.

“... Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: `Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya Swaum (kufunga), kwa hiyo leo sitasema na mtu’” (19:2 6).

Katika Sharia ya Kiislamu kufunga (Swaum) ni kujizuilia kula, kunywa, kujamii, kuingiza kitu chochote katika matundu ya mwili na kujizuilia kumuasi Allah (S.W) kuanzia alfajiri ya kweli mpaka kuingia ma gharibi.

Lengo la Swaumu

Lengo la Swaum katika Uislamu ni kumuwezesha mja awe mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Hivyo, ili lengo hili litimie mfungaji pamoja na kujizuilia kula, kunywa, kujamii, hanabudi pia kujizuilia na kitendo chochote kitakachompelekea kuvunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w).

Kwa maana nyingine, ili Swaum ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, mfungaji hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu pamoja na fikra na hisia zake -na matendo aliyoyakataza Allah (s.w.).

Funga ya macho ni kujizuilia kutazama yale yote aliyoyakataza Allah (s.w), funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w), kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana n.k, funga ya masikio ni kujizuilia kusikiliza yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w); funga ya miguu ni kujizuilia kuendea yale yote aliyotukataza Allah (s.w); funga ya fikra na hisia, ni kujizuilia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea mja kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith zifuatazo:

“Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuw a anaacha chakula chake na kinyw aji chake - ( Allah (s.w) hana haja na funga yake). (Bukhari).

Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema; Ni wangapi wamefunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu, ni wangapi wanaoswali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).

Hadith hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuilia na maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.

Naona mpaka hapo tutakuwa tumepata faida ya kujua funga na makusudio yake

Ni hayo tu!
Lengo la funga NI waja kujifunza tabia njema KUWA WACHAMUNGU

Hivyo Aliefunga atakiwa afunge macho yake
Masikio yake
Ulimi wake n.k
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم
من لا يدع قول زور والعمل به فليس لله أن يترك طعامه و شرابه
Yule asieacha maneno mabaya na vitendo viovu (wakati amefunga) basi Allah Hana haja na kuacha Kula kwake na kinywa kwake
 
Bajeti ya chakula kwa mwezi wa ramadhani ni kubwa mara dufu kuliko miezi mingine halafu eti ni mwezi wa funga .
Kwahiyo hiyo ndio ishu!

Jibu liko wazi funga ya Ramadhani ni maarufu kuliko kwaresma na INA mwitiko mkubwa Sana kuliko kwaresma.

Kwahiyo bilashaka hiyo ni fursa Kwa wafanyabiashara kutaka kupata faida zaidi ingawa inawaumiza walengwa ambao ni wafungaji
 
Bajeti ya chakula kwa mwezi wa ramadhani ni kubwa mara dufu kuliko miezi mingine halafu eti ni mwezi wa funga .
Ungejua kuwa huwa hatufungi Kula Tu wala usingeshughulishwa na haya mambo ya chakula hata kidogo
 
Ungejua kuwa huwa hatufungi Kula Tu wala usingeshughulishwa na haya mambo ya chakula hata kidogo
Aisee Kuna house girl apa budget yake ya kufunga imepita ya familia na yeye ni mmoja tu

Punguzeni kula waislamu jaribuni kufunga
 
Aisee Kuna house girl apa budget yake ya kufunga imepita ya familia na yeye ni mmoja tu

Punguzeni kula waislamu jaribuni kufunga
Je huwa anakula mchana WA Ramadhani au baada ya kufungua?
 
Anakula usiku mpaka saa 10 kama mchwa , mchana anakuwa anaanda Cha kula usiku
Okay,

Kwahiyo Kwanza kumbe lengo la kufunga Alisha lifanya,Kwa maana alifunga vizur Ila baadae ndio akaajia achia na maudambu udambu, kama ni hivyo hakuna Baya alilo lifanya,na kuhusu Kula usiku kucha si kweli naomba tukubaliane juu ya Hilo.
 
Anakula jioni, sasa sita na saa 10 alfajiri, issue ni vyakula special mwenyewe vingine ndo naviona mpaka vya kihindi
 
Lengo la funga NI waja kujifunza tabia njema KUWA WACHAMUNGU

Hivyo Aliefunga atakiwa afunge macho yake
Masikio yake
Ulimi wake n.k
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم
من لا يدع قول زور والعمل به فليس لله أن يترك طعامه و شرابه
Yule asieacha maneno mabaya na vitendo viovu (wakati amefunga) basi Allah Hana haja na kuacha Kula kwake na kinywa kwake
Swadakta chief
 
Anakula jioni, sasa sita na saa 10 alfajiri, issue ni vyakula special mwenyewe vingine ndo naviona mpaka vya kihindi
Sawa,

Hiyo ni ratiba binafsi kwahiyo sioni tatizo hapo....

Khs vyakula vya kihindi ni kubadilisha Radha Tu ya chakula,kwani umesikia ni haramu?
 
Ni kuchagua tu timing ya kula,unafunga Halafu unamnunia asiyefunga, halafu usiku unaamka kula? Nikifunga siku arobaini, Ni uji tu ndiyo unaingia kinywani mwangu
Point yako ni nini chief?

Kwamba wewe unakunywa uji Tu ndio Una funga kiuhalisia au ndio unadhibiti matumizi ya chakula?
 
Back
Top Bottom