Je, funga ya Waislamu ni kula na kunywa tu?

Chief

Amini usiamini mwezi wa ramadhani Una baraka Sana huwa haupiti Bila kuacha athar Kwa waislamu,kila mwaka kuna watu wanaacha maovu na kumrudia Mola wao na wanashika sala.

Kuna watu wanaacha kuishi na mahawara na kufunga ndoa,hao nao ni wengi Sana mwezi huu.

Mimi binafsi ni Shahidi juu ya haya,huko nyuma miaka kadhaa nilikuwa siswali swala tano lkn nakumbuka kuna ramadhani moja ilibadilisha Maisha yangu na kunifanya nidumu na swala mpaka Leo.

Kwahiyo kifupi kila mwaka kuna watu wanabadili Maisha Yao na kujikurubisha zaidi Kwa Allah
 
Hoja zako hazina uhalisia kabisa, Yani watu waingie mikopo kwasababu ya kununua chakula cha ramadhani? Hapana nakataa.

Na likizo ni haki ya kila mfanyakazi,kwahiyo inategemea huenda siku zake za likizo zimeangukia karibu na ramadhani, au mwengine anaomba Kwa makusudio ya kupata Mda WA kufanya ibada kikamilifu katika mwezi mtukufu WA ramadhani.

Kuhusu kupanda bei ni hulka za wafanyabiashara kutaka kupata faida zaidi
 
Chief

Hatuvungi Kwa AJILI ya kutoa sadaka Bali tunafunga Kwa AJILI ya kuwa wachamungu
 
Kuhusu kupanda bei ni hulka za wafanyabiashara kutaka kupata faida zaidi
Walaji wakipungua faida gani wanapata si mavyakula yatawaozea

Ni kinyume chake Ramadan ni eating festival, ni kula kupitia maelezo

Ngoja ianje utajionea mwenyewe ma picha ya ma buffet
 
Walaji wakipungua faida gani wanapata si mavyakula yatawaozea

Ni kinyume chake Ramadan ni eating festival, ni kula kupitia maelezo

Ngoja ianje utajionea mwenyewe ma picha ya ma buffet
Huna jipya wewe ndugu yangu

Uwe na jioni njema
 
Huna jipya wewe ndugu yangu

Uwe na jioni njema
Sio Tanzania tu Dunia nzima Ramadan ni eating festival, waislamu wanakuka kupitia maelezo , ata nyumba za kawaida tu walikuwa wanakula kawaida ila ikifika Ramadan wanakula vyakula vya hali ya juu tena kwa wingi wake

Nina ndugu mpaka wanakwambia uwatumie pesa , sasa jiulize
 
Naongea kitu nimeona kabisa , wewe kukataa hakuondoi ukweli
watu wengi wanafunga hili waonekane kukopa hela kwa sababu ya ramadhani sio ajabu ndio maana kuna baadhi ya watu hawafungi kisa hawana futari walisha kalili kuwa futari ni tambi maziwa chapati za kumimina kusukuma mchele basimati 5000 kilo mayai

wanashindwa kuelewa kuwa futari ni chakula hikihiki tunacho kula kila siku tena baadhi ya waisilamu mwezi ukiandama wanakuwa na mbwembwe sana mala nyingi ufunga kumi la kwanza na lapili basi wanarudi kula mchana hasa hili kundi lisilo swali swala 5 ndilo lenye mbwenbwe udhani mwezi wa ramadhani ni sherehe
 
Kwani wewe hutaki watu wale vizuri kijana?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Umemiza mjadala,umeelezea kielimu,na kiwanachuoni wa hali ya juu.Atakayejifanya hajaelewa,anajipotezea muda tu.
 
Wakristo wengi hawana hoja kwenye Imani ya Kiislam. Wengi Wanabaki na mambo ya vioja Badala ya kuhoji uhalali na msingi Wa Imani ya Kiislam.

Mimi SIO Muislam lakini Ukweli ni kwamba Waislam wamefundishwa Vizuri juu ya misingi ya uislam na Kitabu chao.Wanaheshimu sana maelekezo ya kitabu chao na misingi yake. Hata wanaokiuka wanakiuka Kwa Siri sana.

Wakristo Kila mmoja na tafsiri yake. Matokeo yake wametoa Mwanya Kwa Mashetani nayo kujichomeka kwenye Ukristo na kuharibu Biblia na Imani ya Kweli ya Yesu Kristo.
Mfungo Wa Ramadha ni unafanyika Dunia nzima Kwa uaminifu mkubwa sana bila kukejeliwa na MTU yeyote ambaye ni Muislam.

Pameibuka Wakristo ambao Kwao hakuna dhambi ,Kila kitu ni halali. Uzinzi Sawa,ulevi Sawa, ushirikina Sawa, Wizi Sawa alimradi uibe Kwa akili bila kukamatwa,Ushoga Sawa , utapeli Sawa, ulevi Sawa. Hawa kucha kutwa wanahoji Kwa kejeli Kwa Nini Waislam hawali nguruwe, kwani Waislam wanafunga mchana na kula usiku.

Kuna mambo Mengi ya Msingi ambayo Wakristo baada ya kugundua hila za Wazungu na agenda zao za Siri kulihujumu kanisa walipaswa wayajadili na Kuona namna ya kuyabadili lakini wanajawa na ubinafsi Wa Kupata maslahi kwenye sadaka. Mfano mambo ya ubatizo Wa Maji Mengi na machache, chakula Cha bwana KUTUMIA mkate usiotiwa Chachu na mvinyo uliotiwa Chachu Tofauti na maelekezo ya Mungu kwenye Kuelekea pásaka ya mwanzo Baada ya kutoka MISRI ambayo Yesu aliitimiliza bila kuvunja SHERIA. Suala la Sábato ya Jumamos na Mzungu mmoja kuamua kuipeleka Jumapili Kwa manufaa ya Mila zake na kundi la watu waliokua wamekengeuka na Mila zisizofaa.
Masuala ya wanawake kuwa Wachungaji.
Masuala ya mavazi nusu Uchi makanisani.
Masuala ya wanawake na wanaume kuchangamana kwenye Viti kwenye Ibada .
Masuala ya wanawake kuhubiri wakiwa vichwa wazi makanisani. Masuala ya Ndoa za MKE mmoja wakati Wanawake ni wengi kuliko wanaume n.k.
Masuala ya Kusema Yesu ndiye Mungu na kuacha maswali yasiyo na Majibu.

Haya ndiyo Wakristo walipaswa kuendelea kuyajadili Kwa namna ya kipekee sana mana yanagusa Imani na Taratibu zake kutokana na maelekezo ya Biblia.
 
Umemiza mjadala,umeelezea kielimu,na kiwanachuoni wa hali ya juu.Atakayejifanya hajaelewa,anajipotezea muda tu.
Sherehe ya kula sana Ramadhani inaanza lini , ninetumiwa mpaka ratiba ya ma vyakula kwa kila siku 😂, najua ndugu lazima anipige kizinga Cha pesa ili ale Sana 😂
 
Pale mbusu jiwe unavyojifanya sio mbusu jiwe 😂😂🤣😂

Ramadhani ni sherehe ya kula kupita kiasi
 
Pale mbusu jiwe unavyojifanya sio mbusu jiwe [emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23]

Ramadhani ni sherehe ya kula kupita kiasi
Mimi ni Mkristo ninayeamini katika Biblia sio watu. Ni Mkristo mwadilifu na kusimama katika misingi ya Kristo Mwakozi.
Ukibaki na Ukristo Wa jumuia Utakua tu kama Kada Wa Vyama vya siasa kuwakejeli Waislam bila kuangalia nini Musa alifundishwa na Mungu, Nini Ilikua Imani ya Ibrahim ambaye ni Baba wa Imani . Je, aliamini Imani za wapagani Wa Kiyunani na Kirumi iliyopo leo ?

Je, Yesu AKIRUDI leo ataona Wakristo wanaoamini katika uadilifu na Ukweli Wa Neno la Mungu Tangu Ibrahim mpaka Ufunuo ulipokuja?
 
Wewe ni mbusu jiwe, acha kujifanya mkristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…