Je, gari hii itaenda kuua soko la Kluger na Harrier Tanzania?

Je, gari hii itaenda kuua soko la Kluger na Harrier Tanzania?

Soko lipi la Klugger litakalokufa? Maana tangia hapo Kluger haijafanya vizuri sokoni
Kufanya vizuri sokoni si kipimo cha uzuri wa gari, bali ni kipimo cha wengi kumudu gharama ya gari husika. Kluger kwa sasa ndiyo habari ya mjini japo wengi hawawezi bei yake pamoja na gharama za kuiweka barabarani. Kluger ni gari ya heshima!
 
Wakinga wanane jirani zako kuwa na Kluger haimaanishi soko kubwa. Kluger ni moja ya magari yaliyokosa soko Tanzania. Research za magari hufanyika kwenye miji mikubwa. Ukitrap magari Magomeni hadi faya, pande zote yajae, si ajabu ukakosa Kluger hata moja. Tembelea show rooms za kitaa, nyingi hazina kabisa hata moja

Nikukumbushe pia, kuna watu wengi tu hawaijui Kluger kabisaa.
Sababu ni kwamba wengi hawamudu gharama za kununua na za kuiweka barabarani, lakini kluger ni gari zuri mno!!! Wengi wanamudu IST!!! Kuonekana IST kwa wingi barabarani kuliko kluger haimaanishi IST ni bora kuliko kluger!!! Labda niseme hivi: Ukitembelea familia 100 kwenye lunch, utakutana na maharage zaidi kuliko samaki!

Hii haina maana kuwa maharage ni bora zaidi kuliko samaki!!!!!! Achana na kitu kluger!! Hiyo ni middle class luxury, inazidiwa na high class luxury tu kama vile V8, etc (kwa level ya watanzania).
 
Kitu kluger ni habari nyingine!!! Tatizo mtu anakuwa na kluger halafu matumizi yake ni ya kutembea km 15 tu kwa siku kwa mizunguko midogo midogo kwenye barabara mbaya, hapo hautaona thamani ya kluger!! Utaliona kama jini la kunywa mafuta!

Hebu weka full tank yake lita 70, halafu uitafute Dodoma toka Dar lakini uanze safari kama saa tisa usiku hivi kabla magari hayajawa mengi barabarani. Nakwambia utashangaa utakavyotumia mafuta kidogo na utafika dodoma na mafuta kubaki mengi sana!
 
Kufanya vizuri sokoni si kipimo cha uzuri wa gari, bali ni kipimo cha wengi kumudu gharama ya gari husika. Kluger kwa sasa ndiyo habari ya mjini japo wengi hawawezi bei yake pamoja na gharama za kuiweka barabarani. Kluger ni gari ya heshima!!!
Tuliza basi kidogo ufahamu wako angalau mwenyewe ujielewe ili na wengine tukuelewe. HAKUNA MAHALI NIMESEMA KLUGGER NI GARI BAYA...nilichosema ni kuwa HAIJAFANYA VIZURI KWENYE SOKO LA TANZANIA.

Soko la bidhaa yeyote ile huamuliwa na factors kadhaa, vikiwemo bei, uimara, uzuri, kasumba, mazingira na hata mienendo ya jamii (soacial preferences)

Umekurupuka mbio kuja kuitetea Klugger as if kuna mtu kasema ni gari mbaya, ukasahau kuwa hoja ni KUFANYA VIZURI SOKONI.

Kwenye mbwabwajo wako, umeitaja IST. Sasa huo ndio mfano bora kabisa wa gari iliyofanya vizuri sokoni. Ukienda kwenye mikusanyiko ya jamii, ukaangalia megesho ya magari, utaona IST ni nyingi kuliko gari nyingine zozote. Kwa muktadha huu IST imefanya vyema sokoni.

Kufanya vyema sokoni kwa hili gari pendwa, yaani IST, kunachangiwa na sababu kadhaa ambazo KLUGGER imezikosa
1. Bei ndogo
2. Ulaji mdogo wa mafuta
3. Gharama ndogo ya matunzo
4. Umbo dogo. Unaweza kupaki sehemu ndogo
5. Na nyinginezo

Nikukumbushe kuwa, mada hapa ni kufanya vizuri sokoni. Ikiwa Klugger inauzwa kwa bei ambayo kati ya watu 100 ni wawili wanaafford na IST inauzwa kwa bei ambayo kati ya watu 100 watu 17 wanaweza kununua, hii inamaanisha IST inafanya vizuri sokoni.

Kuhusu umadhubuti na ufahari wa gari, nguvu, mbio na sifa za kijinga, hayo ni mambo mengine.
 
Hio Subaru Forester ukiilinganisha na Harrier au Kluger hio Subaru bado ipo chini sana wakati hizo zingine zipo juu kimtindo juu namaanisha umbali wa kutoka kwenye ardhi hadi bodi ya gari ilipo
 
Hio Subaru Forester ukiilinganisha na Harrier au Kluger hio Subaru bado ipo chini sana wakati hizo zingine zipo juu kimtindo juu namaanisha umbali wa kutoka kwenye ardhi hadi bodi ya gari ilipo
Sawa mkuu
 
Forester za 2006 kurudi nyuma ndio subaru,hizo za 2007 kuja juu ni upuuzi tu(kwa mtizamo wangu lkn).

Kwanzia 2009 ndo naona wametoka kwenye sport look na kuingia ushindan na kina rav4 .yan zimekuwa za kiutu uzima sana ila crossport ya 2008 ni kali sana ukiweka wa BOV yako map ya maana ni gari flan hivi unaeza chukua attention muda wowote
 
Hio gari nimeiendesha juzi tu. Ni ya best yangu plate DSF. Kiukweli ni gari ambayo nje ina muonekano wa kibabe ila ndani full plastics. Dashboard haivutii kabisa halafu pia kiti chake kiko chini sana. Kiukweli sikufeel kama niko ndani ya suv. Japo inaitwa SUV.

The next day niliendesha Suzuki Sport Grand Vitara V6 2.7ltr toka beforward DSM to Moshi. Aisee gari lina pulling kinoma yani. Linatembea balaa yani full kukata upepo. Halafu ndani liko very spacious ukikaa unakuwa juu juu yani una feel umekalia SUV kabisa. Naona Suzuki iko comfortable kuliko hio Subaru.
 
Mkuu hapo kwenye suzuki umenikuna asee, hii gari iko njema mno inatulia sana barabarani,
 
Back
Top Bottom