Je goli la 4 la Yanga vs Mtibwa ni la Skudu au la beki wa Mtibwa aliyejifunga?

Je goli la 4 la Yanga vs Mtibwa ni la Skudu au la beki wa Mtibwa aliyejifunga?

Embu tukumbuke sheria za mpira wa miguu zinasemaje kuhusu goli la kujifunga ili tujue kama mtu anayestahili kupewa credit ya goli la nne katika mechi ya jana ya Yanga vs Mtibwa ni Skudu au beki wa Mtibwa.

Skudu alipopiga mpira, kipa alianza kuruka kuufuata ule mpira ila kuna beki wa Mtibwa akaupiga kichwa na kuupeleka mpira juu zaidi ya eneo ambalo kipa alidhani mpira unaelekea matokeo yake akashindwa kuufikia. Ukiangalia vizuri utaona yule beki baada ya kujifunga alishika kichwa.

Angalia goli hili katika fainali ya kombe la dunia 2018, Ufaransa vs Croatia. Goli hili linafanana sana na hili la Skudu na lilihesabika kama goli la kujifunga kwa mchezaji wa Croatia aliyeuparaza mpira kwa kichwa.


View attachment 2846487
Nenda kaangalie goli la liver vs crystal palace la kusawazisha halafu uone nani kaandikwa mfungaji
 
Nenda kaangalie goli la liver vs crystal palace la kusawazisha halafu uone nani kaandikwa mfungaji
Hili ni jibu zuri kwa wale waliokuwa wanasema mpira usipobadili uelekeo ni la kujifunga, hili limebadili uelekeo. Lile shuti la Mo Salah limebadili uelekeo na pia lisingemgonga mchezaji mwingine ule mpira ulikuwa unaenda nje ila bado amepewa Mo Salah.

Ukweli ni kuwa credit ya kujifunga siyo credit nzuri kwa mchezaji aliyejifunga na hayo magoli hayahesabiki kama goli lake. Pia FIFA hawana sheria bali wana miongozo tu kuhusu jinsi ya kutoa credit kwenye magoli haya. Ndiyo maana ni nadra sana kukuta ni issue ya majadiliano.
 
Back
Top Bottom