Sasa hiyo Quora si ni kama JF tu kila mtu anatoa maoni yake, yaani ndiyo unatumia kama chanzo chako cha kuja kutunisha kifua. Nimeileta mada ili ijadiliwe na watu wa mpira na si suala la kishabiki au kuna mtu ameita wivu.
Unasema ikiwa on target basi haiwezi kuwa goli la kujifunga na mimi nikasema inaweza kuwa on target lakini kama mazingira yanaonyesha kwa kugongwa mpira unazuia mtu mwingine mfano golikipa asiweze kuuokoa kutokana na jinsi ambavyo alikuwa amejipanga kabla haujaguswa na mchezaji mwenzake hilo ni goli la kujifunga.
Ukitaka mifano, kwenye mechi ya fainali kombe la dunia 2018 Croatia vs Ufaransa alijifunga Mandzukic goli linalofanana kabisa na hilo la Mtibwa na lilikuwa on target.
Ukitaka mifano zaidi angalia hiyo hiyo kombe la dunia 2018, Tunisia vs Panama alilojifunga Yassin Meriah. Angalia Poland vs Senegal, goli alijifunga Cionek. Hizo zote mipira ilikuwa on target na credit ya magoli walipewa hao waliojifunga.