Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

HAKUNA. Zaidi ya kukausha Sauti yake bungeni kwa kuwatukana viongozi na kukesha mahakamani mh. Mdee hajatufanyia lolote. Hatujajuwa kwanini. Labda ni utoto na utomboy wamsumbuwa. Au labda hajuwi majukumu yake. Yawezekana alitaka ubunge ili anufaike kibinafsi na kufikiri akidundulisha kesi polisi na mahakamani ataonekana mwanasiasa mahiri. She was and she is a waste of our votes. Tunajuta kumchaguwa. Ila tumesema YATOSHA...
 
Ivi kuna mtanzania atakayeweza mpigia kura ngwajima?jamani historia na matukio ya huyu mtu inaonesha ni tapeli kabisa laiti zingekua nchi zilizoendela asingeweza hata kupata nafasi ya kuwasilisha chama .ni muda wa watanzania kuacha kuchagua chama zaidi waangalie mtu zaidi hata kama Halima kwa miaka kumi haha fanya kitu lakin gwajima ni mtu ambaye sio sahihi kabisa kwa watu wa kawe
 

Pascal kahamie Chato umsaidie jiwe kulima bangi , lakini Kawe hatuwezi kumpa Askofu mlaji mivutu
 

Kada Pascal,

Hapa umepotosha kwa kiasi kikubwa.

Sasa twende kimantiki (logical reasoning). Kwamba, barabara za mitaa ya jimbo la Kawe hazina lami kwa sababu mbunge wa eneo hilo anatoka chama cha upinzani na kwamba barabara za Ilala na Kinondoni zina lami kwa sababu wabunge wa hayo majimbo ni makada wenzako wa CCM!! Du!

Kama hii premise iko sahihi basi unamaanisha kwamba katika jiji la Dar barabara za mitaa katika majimbo mengine yote yaliyokuwa na wabunge wa CCM kama Segerea, Ukonga na Kigamboni zina lami kwa hiyo Kawe pekee ndio exception!!!

Kwa kutumia hiyo hiyo argument yako, kwa vile barabara za mitaa ya Oyster-bay, Masaki na Mikocheni zina lami ilhali ziko katika jimbo la Kawe basi Halima automatically anastahili kuongezewa miaka mitano tena.

Kiuhalisia, unampigia kampeni Halima.

Lakini kama kuwa na mbunge wa CCM ni kigezo muhimu cha kupata maendeleo katika jimbo basi kwa sasa hii nchi isingekuwa maskini kwa sababu tangu uhuru CCM imekuwa na absolute majority ya wabunge bungeni. Labda kinyume chake ni sahihi. Kikwazo cha maendeleo ni wabunge wa CCM.
 
Suala hapo ni ukabila sio ukristo mana Gwajima alimtukana mpaka Kadinali Pengo Mkatoliki kama Paskal.
Alimdhalilisha kwa sababu tu Pengo alikataa kumhujumu JK aliyeruhusu Uhuru na maendeleo ya kisiasa na kijamii Gwajima akawa anatumika kumhujumu JK kwa sababu ya uislam wake huku akiaminisha watu kuwa JK hajafanya chochote bila kuangalia kuwa kama sio JK kuruhusu Uhuru wa kuabudu huenda makanisa binafsi yangefutiliwa mbali mana ni kichaka cha matapeli na wauaji kama akina Kibwetere na Mwamposa.
 
Tanzania tukifanikiwa kuiondoa CCM ambalo ni joka kuu tutakua tumepiga hatua kubwa sana kisiasa na kijamii.
CCM inasababisha kuwe na mifumo mibovu sana ya kupata viongozi. Kuna wanaCCM wazuri zaidi ya Gwajima wamekatwa na wanashindwa kufurukuta. Hawakupewa nafasi ya kujinadi kupitia vyombo vya habari kama ilivyokua mchakato majimboni ili tuwapime uwezo wao kabla ya kuwapa jukumu hilo Wajumbe. Pia Chadema wanahofu ya kumleta MTU mpya asiyekua na ujasiri wa kupambana na dhulma za CCM na kuwadindia Wakurugenzi wauaji na majambazi wanaovuruga uchaguzi na kusabasha vurugu na hata kuleta mauaji kama ya Akwilini.
 
Ulipaswa uwahoji wakusanya kodi wa nchi hii, Je Wananchi wa Kawe hawalipi Kodi?
Kodi wanayolipa mmewafanyia nini.?

Nchi imeingia katila ubaguzi mbaya sana kuwahi kutokea.

Na wanasiasa wanasema wazi kabisa usipochagua chama hiki hampati barabara , maneno ya kibaguzi kabisa vipi kuhusu kodi yao wanayolipa?
 
ushabiki wa vyama unakuzuzua,
Halima Umlinganishe na janjajanja tapeli!!
Tambua ccm yenu hiyo ni chama kwnza lkn HALIMA (CDM)NI TAIFA KWANZA.
 
Pascal hilo swali lako gumu hatuna majibu. Huwezi kujibu swali bila kuwa na kumbukumbu kama uliwahi kulisoma au kukutana nalo katika discussion. Uliza maswali yanayoweza kujibika.
 
Mkuu Jidu La Mabambasi ,
Naunga mkono hoja, Wana Kawe, twende na Gwajima.

P
 
Paschal wewe huwa sikuelewi kabisa,uko tayari wananchi waumie kabisa kwa kutetea haya mambo
 
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.
 
Ukishakuwa mtafuta uteuzi na au mteule katika ccm, lazima utumie ujinga wako wote. Nimeona kwa watu kama Mkumbo, Kabudi, Polepole, nk. Pascal Mayalla ni nani hata atumie akili yake ili hali kuna kitu anakitafuta ccm? Huwezi kuwa mfuasi wa ccm ukabakia na akili yako awali. Haiwezekani.
 
barabara ya kinzudi, madaktari 80 Walisomeshwa bure Lugalo na IMTU. Kwa hela ya halima,SALASALA anakoishi gwajima lami ile imewekwa na halima, Zahanati 19 zimejengwa. Barabara za mwendo kasi na upanuzi wa barabara ni halima
 
alivyowapa maji...aliyageuza kuwa msikiti??

usinichukie najaribu kuwaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…