Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Wanabodi,

Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu aliyemaliza muda wake, Mhe. Halima Mdee, ambaye, baada ya kuwa Mbunge wa Kawe kwa vipindi viwili mfululizo, na sasa anaomba tena tumchague, hivyo nauliza kama kuna mtu yoyote anaweza kutueleza humu, hata jambo moja tuu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, amelifanyia nini jimbo la Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10?, ili tumfanyie assessment kama anastahili jee anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, or she did nothing hivyo anastahili apumzishwe?

Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji ya halali na swali la ukweli la mwana Kawe, kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?

Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani imekufanyia nini, bali ujiulize, wewe utaifanyia nini Marekani". Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.

Najua kuna watu watasema kazi ya kuleta maendeleo ni kazi ya serikali, kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali, tumekuwa tukishuhudia wabunge wa majimbo mengine wakipigamia majimbo yao Bungeni, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, aliwahi kupigania nini cha maendeleo ya Kawe?. Kama kuna anayejua humu, atuambie hata kitu kimoja tuu cha Kawe ambacho Halima Mdee alikipigania?.

Kuna zile fedha za Mfuko wa Jimbo. Jee kuna mwana Kawe yoyote, aliwahi kumshuhudia Mbunge wetu Mhe Halima Mdee akija eneo lolote la Kawe na kuchangia shughuli zozote za maendeleo kupitia fedha za mfuko wa Jimbo?.

By the way: Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe huyu Askofu ni mdau mkubwa wa maendeleo ya watu wa Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya mambo makubwa kwa wana Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida bila hata kujua kuwa kuna siku atakuja kugombea ubunge wa Kawe.

Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Na kufuatia eneo la Kunduchi ni eneo la pembezoni mwa bahari, ukichimba visima vifupi, utapata maji ya chumvi, Hivyo Askofu Gwajima kwanza alichimba visima virefu 12 vya mita 300 kwenda chini ili kupata maji safi na salama kwa ajili ya wana Kawe!. Miongoni mwa wafaidika wa visima hivyo virefu, kwenye misikiti 7 ya Salasala hivyo kuwapatia maji Waislamu, maji ya kutawadha kabla ya kuswali.

Kisha akayatafuta maji ya Dawasco, yanapita mbali, akaomba kibali Dawasco, akanunua manomba kama ya Dawaco ya kusambaza maji, akayatandika kuwatumia mafundi wa Dawasco, anunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mita za maji kama za Dawasco na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.

Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.

Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.

Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Mhe. Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, ukiambiwa umchague mmoja kati ya hawa wawili, utamchagua nani?.

Utakubaliana na mimi kuuliza, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa upendo, heshima na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako wa miaka 10 Kawe?, na Jee sasa tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kumwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima ili kuikamilisha kazi nzuri ulioshaanza kuitenda kabla hata hujawa Mbunge?.

Kama kuna mtu yoyote ana video clip yoyote ya Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee akishiriki shughuli yoyote ya maendeleo Kawe, naomba aielete ili angalau tumuone!
Shuhudia mwana Kawe huyu anavyojituma kwenye kuleta maendeleo

View attachment 1558915

Nauliza tuu!.

Paskali
HAKUNA. Zaidi ya kukausha Sauti yake bungeni kwa kuwatukana viongozi na kukesha mahakamani mh. Mdee hajatufanyia lolote. Hatujajuwa kwanini. Labda ni utoto na utomboy wamsumbuwa. Au labda hajuwi majukumu yake. Yawezekana alitaka ubunge ili anufaike kibinafsi na kufikiri akidundulisha kesi polisi na mahakamani ataonekana mwanasiasa mahiri. She was and she is a waste of our votes. Tunajuta kumchaguwa. Ila tumesema YATOSHA...
 
Ivi kuna mtanzania atakayeweza mpigia kura ngwajima?jamani historia na matukio ya huyu mtu inaonesha ni tapeli kabisa laiti zingekua nchi zilizoendela asingeweza hata kupata nafasi ya kuwasilisha chama .ni muda wa watanzania kuacha kuchagua chama zaidi waangalie mtu zaidi hata kama Halima kwa miaka kumi haha fanya kitu lakin gwajima ni mtu ambaye sio sahihi kabisa kwa watu wa kawe
 
Mkuu kifaulongo , kwanza asante kwa mchango wako , umechangia very objectively, kwasababu tangu bandiko hili lianze, hadi linafika posts 344, wewe ndie mtu pekee uliejitokeza na kujibu at last Halima did something Kawe. Thanks for this.

Pamoja na yote hayo, kufuatia kauli thabiti kutoka Juu, za Serikali inapeleka wapi maendeleo, nikitolea mfano mmoja tuu wa barabara za lami za mitaani, nikifanya a comperative analysis ya barabara za mitaa ya Ilala, na Kinondoni, compared to Kawe, utakubaliana na mimi, kuwa Halima Mdee, pamoja na Juhudi zake zote, na kumpenda tunampenda mimi nikiwemo, nampenda Halima na mwenyewe anajua nampenda, lakini Sisi wana Kawe kindakindaki, katika umoja wetu, tumeamua kwa dhati kabisa kuwa i hii miaka 10 ya Halima Mdee Kawe sasa imetosha, tuna lirudisha jimbo la Kawe, nyumbani kumenoga!.
P

Pascal kahamie Chato umsaidie jiwe kulima bangi , lakini Kawe hatuwezi kumpa Askofu mlaji mivutu
 
Mkuu kifaulongo , kwanza asante kwa mchango wako , umechangia very objectively, kwasababu tangu bandiko hili lianze, hadi linafika posts 344, wewe ndie mtu pekee uliejitokeza na kujibu at last Halima did something Kawe. Thanks for this.

Pamoja na yote hayo, kufuatia kauli thabiti kutoka Juu, za Serikali inapeleka wapi maendeleo, nikitolea mfano mmoja tuu wa barabara za lami za mitaani, nikifanya a comperative analysis ya barabara za mitaa ya Ilala, na Kinondoni, compared to Kawe, utakubaliana na mimi, kuwa Halima Mdee, pamoja na Juhudi zake zote, na kumpenda tunampenda mimi nikiwemo, nampenda Halima na mwenyewe anajua nampenda, lakini Sisi wana Kawe kindakindaki, katika umoja wetu, tumeamua kwa dhati kabisa kuwa i hii miaka 10 ya Halima Mdee Kawe sasa imetosha, tuna lirudisha jimbo la Kawe, nyumbani kumenoga!.
P

Kada Pascal,

Hapa umepotosha kwa kiasi kikubwa.

Sasa twende kimantiki (logical reasoning). Kwamba, barabara za mitaa ya jimbo la Kawe hazina lami kwa sababu mbunge wa eneo hilo anatoka chama cha upinzani na kwamba barabara za Ilala na Kinondoni zina lami kwa sababu wabunge wa hayo majimbo ni makada wenzako wa CCM!! Du!

Kama hii premise iko sahihi basi unamaanisha kwamba katika jiji la Dar barabara za mitaa katika majimbo mengine yote yaliyokuwa na wabunge wa CCM kama Segerea, Ukonga na Kigamboni zina lami kwa hiyo Kawe pekee ndio exception!!!

Kwa kutumia hiyo hiyo argument yako, kwa vile barabara za mitaa ya Oyster-bay, Masaki na Mikocheni zina lami ilhali ziko katika jimbo la Kawe basi Halima automatically anastahili kuongezewa miaka mitano tena.

Kiuhalisia, unampigia kampeni Halima.

Lakini kama kuwa na mbunge wa CCM ni kigezo muhimu cha kupata maendeleo katika jimbo basi kwa sasa hii nchi isingekuwa maskini kwa sababu tangu uhuru CCM imekuwa na absolute majority ya wabunge bungeni. Labda kinyume chake ni sahihi. Kikwazo cha maendeleo ni wabunge wa CCM.
 
Paskal ulipaswa kutueleza kazi za mbunge kwanza kabla kumpigia debe mtu wako, ila sishangai huyo unaempigia debe una sababu zako kwanza chama kimewataka wote mlioangushwa kuwapigia debe waliopita pili gwajima ni mkristo mwenzio pengine nawewe ungependa misikiti iwe Sunday schools
Suala hapo ni ukabila sio ukristo mana Gwajima alimtukana mpaka Kadinali Pengo Mkatoliki kama Paskal.
Alimdhalilisha kwa sababu tu Pengo alikataa kumhujumu JK aliyeruhusu Uhuru na maendeleo ya kisiasa na kijamii Gwajima akawa anatumika kumhujumu JK kwa sababu ya uislam wake huku akiaminisha watu kuwa JK hajafanya chochote bila kuangalia kuwa kama sio JK kuruhusu Uhuru wa kuabudu huenda makanisa binafsi yangefutiliwa mbali mana ni kichaka cha matapeli na wauaji kama akina Kibwetere na Mwamposa.
 
Ivi kuna mtanzania atakayeweza mpigia kura ngwajima?jamani historia na matukio ya huyu mtu inaonesha ni tapeli kabisa laiti zingekua nchi zilizoendela asingeweza hata kupata nafasi ya kuwasilisha chama .ni muda wa watanzania kuacha kuchagua chama zaidi waangalie mtu zaidi hata kama Halima kwa miaka kumi haha fanya kitu lakin gwajima ni mtu ambaye sio sahihi kabisa kwa watu wa kawe
Tanzania tukifanikiwa kuiondoa CCM ambalo ni joka kuu tutakua tumepiga hatua kubwa sana kisiasa na kijamii.
CCM inasababisha kuwe na mifumo mibovu sana ya kupata viongozi. Kuna wanaCCM wazuri zaidi ya Gwajima wamekatwa na wanashindwa kufurukuta. Hawakupewa nafasi ya kujinadi kupitia vyombo vya habari kama ilivyokua mchakato majimboni ili tuwapime uwezo wao kabla ya kuwapa jukumu hilo Wajumbe. Pia Chadema wanahofu ya kumleta MTU mpya asiyekua na ujasiri wa kupambana na dhulma za CCM na kuwadindia Wakurugenzi wauaji na majambazi wanaovuruga uchaguzi na kusabasha vurugu na hata kuleta mauaji kama ya Akwilini.
 
Ulipaswa uwahoji wakusanya kodi wa nchi hii, Je Wananchi wa Kawe hawalipi Kodi?
Kodi wanayolipa mmewafanyia nini.?

Nchi imeingia katila ubaguzi mbaya sana kuwahi kutokea.

Na wanasiasa wanasema wazi kabisa usipochagua chama hiki hampati barabara , maneno ya kibaguzi kabisa vipi kuhusu kodi yao wanayolipa?
 
Mnaodai serikali ndio haipeleki hela kwenye majimbo ya upinzani

muwe hata mnaangalia majimbo mengine ya upinzani hali iko vipi

nendeni mikumi huko kwa bwana Joseph muone mabalaa yake halafu

ndio muongee nje nje nje zenu,Hoja hamjibu mpo kumshambulia paschal

kaleta mjadala watu mseme yupi n yupi hata kama n kampeni sawa mkosoeni

kulingana na thread inavyotaka sio kuleta ujuaji mwingi,ki ufupi Halima this time Aje kitaani tu.
ushabiki wa vyama unakuzuzua,
Halima Umlinganishe na janjajanja tapeli!!
Tambua ccm yenu hiyo ni chama kwnza lkn HALIMA (CDM)NI TAIFA KWANZA.
 
Pascal hilo swali lako gumu hatuna majibu. Huwezi kujibu swali bila kuwa na kumbukumbu kama uliwahi kulisoma au kukutana nalo katika discussion. Uliza maswali yanayoweza kujibika.
 
Kwa miaka 10 aliyokaa Halima Mdee kuwakilisha jimbo la Kawe, maendeleo ya miundombinu ya kijamii ni kama hakuna.

Nimeishi jimbo ka Kawezaidi ya miaka 20 baada ya kuhamia huku toka Temeke, hali ya Kawe inatisha.
Mdee hawezi kazi ya kuleta maendeleo, ni kwamba hafai.

Tatizo lipo kwa muwakilishi wetu, Halima Mdee.
Watu wasichague kwa mazoea, chagua Gwajima tupate mabadiliko na maendeleo.
Hata waliomchagua Trump si kwamba wanampenda, wamemchagua kwa maslahi ya maendeleo yao.

Wana Kawe tuwe strategic, chagua Gwajima.
Mkuu Jidu La Mabambasi ,
Naunga mkono hoja, Wana Kawe, twende na Gwajima.

P
 
Paschal wewe huwa sikuelewi kabisa,uko tayari wananchi waumie kabisa kwa kutetea haya mambo
 



 
Pascal Mayalla ni amekuwa mjinga sana this time,badala ya kutuletea blah blah za kijinga zisizo na utaalam wowote ule aitishe hata mchango aombe tumnusuru kutokana na kukosa kabisa kazi ya kumuingizia kipato. Mwambieni tupo tayari kumchangia ili abaki na uhuru wake wa akili ambao anaelekea kuupoteza.

Mada ya kipuuzi sana hii aliyoleta!
Ukishakuwa mtafuta uteuzi na au mteule katika ccm, lazima utumie ujinga wako wote. Nimeona kwa watu kama Mkumbo, Kabudi, Polepole, nk. Pascal Mayalla ni nani hata atumie akili yake ili hali kuna kitu anakitafuta ccm? Huwezi kuwa mfuasi wa ccm ukabakia na akili yako awali. Haiwezekani.
 
barabara ya kinzudi, madaktari 80 Walisomeshwa bure Lugalo na IMTU. Kwa hela ya halima,SALASALA anakoishi gwajima lami ile imewekwa na halima, Zahanati 19 zimejengwa. Barabara za mwendo kasi na upanuzi wa barabara ni halima
 
Paskali nisiwe mnafiki siwezi mchagua Gwajima kwakuwa alishasema anataka kuigeuza misikiti kuwa Sunday schools, nikiwa kama muislam nawaza huyu hakuwa na madaraka aliongea vile je nikimkabidhi madaraka itakuwaje? Mimi ni muislam na najivunia kuwa muislam
alivyowapa maji...aliyageuza kuwa msikiti??

usinichukie najaribu kuwaza
 
Back
Top Bottom