Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Kwa wabunge wengi waliopo katika miji mkuu kama huu DAR ni ngumu sana kuweza kuona kazi aliyofanya Mbunge. Mfano kwa sisi wakazi wa ILala jimbo la Zungu huwezi kumpima Zungu kwa kazi alizofanya jimboni kwani hadi leo barabara za ndani maeneo ya Upanga na kwingineko hayana lami...na leo anaomba tena...
So same na kwa Halima Mdee.....achilia mbali kipindi cha miaka 10 anayoenda kumaliza October 28 zaidi ya 1/2 katumikia mahakamani.....
So let her take another 5 years tuone atabadili nini lakini pia ikumbukwe kuwa eneo alipo mpinzani serikali kupeleka huduma inachukua muda.....
 
Pascal Mayalla mwambie Gwajima ajenge kwanza Kanisa ambalo ndio chanzo chake cha mapato.

Haiwezekani mtu kujenga nyumba ya jirani wakati yeye mwenyewe hana nyumba.

Yaani yeye na huduma yake hawana pa kuabudia leo aende akajengee wananchi sijui vitu gani.

Maneno yoooote anayoongea Gwajima sasa ni kampeni tu kama wengine wanaosema mabomba yatatoa maziwa.

Swali hili ulielekeze pia kwa wabunge yote wa CCM wamefanya nini kwenye majimbo yao tena wakina na benefit ya chama tawala kuwa chao.
 
kale ka pesa ka mfuko ka jimbo kametumika vipi?
 
Ni vyema ungejikita kujibu hoja zake....
 
alivyowapa maji...aliyageuza kuwa msikiti??

usinichukie najaribu kuwaza
Wala sikuchukii kwanza unapaswa kujiuliza aliyesema anataka aigeuze misikiti kuwa Sunday schools ni nani? Labda kuwapa maji ndio gia ya kubadili kwenyewe.
 
Sugu na Mdee wanakazi mwaka huu

Mbeya hata kwa bao la mkono hatuwezi kushinda.

Kawe sitaki kuhukumu, Mungu anaenda kuhukumu mwenyewe. Mungu hadhihakiwi hata siku moja.

Kilio chaja muda si mrefu, ndipo watakapolia wale wanaowategemea wanadamu
 
Nyie makada wa chadema aka chadomo ndio mna akili gani ? Naongelea mikakati ya kimaendeleo aliyoweka bi kidude katika jimbo la kawe ni ipi ?
 
Na wewe umetufanyia nini sisi wakazi wa Kawe kiasi cha kuamua kabisa kuomba ridhaa ya wajumbe ili utuwakilishe "bangeni"!??
Naamini rafikiyo "Yohana Mtembezi" mweusi alikudanganya bwana njaa.
Gwajima aanze kuwajali wale wafuasi wake wachache masikini wa kutupwa kabla hajaja kutaka kutuhadaa makumi elfu elfu ya wakazi wa Kawe.
 
Mkuu nguvu ,upo sahihi kabisa. Kongole kwa kuisimamia kweli na imani yako.
Mimi binafsi siwezi kamwe kumchagua mtu ambaye ameacha kuchunga kondoo na kukimbilia kuwa mla kondoo.
 
Nyie makada wa chadema aka chadomo ndio mna akili gani ? Naongelea mikakati ya kimaendeleo aliyoweka bi kidude katika jimbo la kawe ni ipi ?


Ulitaka aanze kutoa kutoa nyama choma na sahani za ugali na soda za bure ndio uite maendeleo ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…