Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi


Pascal , huyu Lawiti , akipata ubunge Kawe mtaipata


 
Bro P hupendezi kuwa kada wa CCM, unapokuwa kada wa CCM ni lazima uuvae uongo huku ukiutupa mbali ukweli.
Huyo bishop hana lolote la kuwafanyia wana Kawe kwa sababu ameamua kuwa muongo ili atimize malengo yake ya kuendeleza utapeli pamoja na biashara haramu.
Bro P ukiachana na ukada wa CCM kweli itakuwa pamoja nawe maana uongo utatoweka kwako, ila kwa sasa wewe na bishop Gwaji lenu ni moja ambalo ni KUTAPELI WANA KAWE.
nawapa angalizo hili kuwa hamtaweza maana wana Kawe walishatoka ktk zama za ujinga ulioasisiwa na ccm, hivyo mnachokifanya sasa wana CCM wote hapo kawe ni sawa na kufukuza upepo.
 
Jimbo la Kawe si ndiko kulikuwaga na migogoro ya ardhi isiyoisha? Hiyo ni credit kwa Mdee!
 
Nakazia hapa
 
Kumbe nawe unataka madrasa zetu zigeuzwe misikiti co?angeenda tu huko usukumani angeupata co hapa kwa watu tunaojitambua
 
IfOTE="Pascal Mayalla, post: 36582337, member: 17813"]
Wanabodi,

Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu, kama kuna mtu anaweza kutueleza humu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, ameufanyia nini Kawe Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10, ili tumfanyie assessment kama anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, au apumzishwe?.

Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji la kweli kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?.

Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani ikufanyie nini, bali ujiulize, utaifanyia nini Marekani. Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.

Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe ni mdau wa maendeleo ya Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya makubwa kwa Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida!.

Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Kwanza alichimba visima virefu 12 kwenye misikiti ya Salasala na kuwapatia maji Waislamu, kisha akanunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mabomba na mita za maji na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.

Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.

Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.

Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, Utakubaliana na mimi, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa heshima na upendo na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako Kawe?, na Jee tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kunwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima?.

Nauliza tuu!.

Paskali
[/QUOTE]
Gwajima anafanya Kazi gani ya kumuingizia kipato kikubwa hivyo Hadi kununua tingatinga za kuchonga Barabara? Hizo Kazi zake zimeonekana tuu kipindi hiki cha Kampeni?
 
Jibu hoja ,acha ufala ,Halima Mdee kaifanyia nini Kawe ndani ya miaka kumi akiwa mwakilishi wa jimbo ?
1....
2.....
3.....
4......
5.......
 
kumbe mbunge sio majukumu yake kuleta maendeleo na mbunge sio sehemu ya serikali ? Naomba ufafanuzi hapo tafadhali
 
Watu wa CCM mnapenda sana kujitoa ufahamu. Kikatiba na kisheria kazi ya mbunge ni nini?
Je Mdee alikuwa anakusanya kodi?
CCM tunaokaa kwenye majimbo ya CCM mbunge wetu hatukuwahi muona tangu uchaguzi wa 2015, bahati mbaya hata bungeni hajawahi ongea.
 
Kwahiyo misikiti au hizo Sunday school ndo maendeleo siyo?

Mbona dini zilizoletwa kwa mashua mnamo Karne ya 18/19 zinataka kuwafanya mkose Akili Namna hiyo?

Namchukia Sana mtu anaemuchukia Mtanzania mwenzake kisa dini za kutoka nchi za mbali huko.

Kwahiyo wewe na huyo gwajima wako mnaoshadadia utamaduni wa waarabu na wazungu wote nawaona Kama hamjielewi tu.
 
Watu wa kanda ileeee sio wa kuwapa madaraka kabisa nimeona! Ni washamba sana na wanafanya mambo ya kiwaki na kuleta mtafaruku, na wa binafsi sana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…