Wanabodi,
Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu, kama kuna mtu anaweza kutueleza humu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, ameufanyia nini Kawe Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10, ili tumfanyie assessment kama anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, au apumzishwe?.
Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji la kweli kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?.
Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani ikufanyie nini, bali ujiulize, utaifanyia nini Marekani. Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.
Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe ni mdau wa maendeleo ya Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya makubwa kwa Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida!.
Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Kwanza alichimba visima virefu 12 kwenye misikiti ya Salasala na kuwapatia maji Waislamu, kisha akanunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mabomba na mita za maji na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.
Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.
Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.
Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, Utakubaliana na mimi, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa heshima na upendo na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako Kawe?, na Jee tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kunwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima?.
Nauliza tuu!.
Paskali