Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee atatimba Bungeni kwa tiketi ya Viti Maalum?

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee atatimba Bungeni kwa tiketi ya Viti Maalum?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Halima Mdee kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa BAWACHA ndio Mbunge wa Viti Maalumu namba moja kama CHADEMA itapata sifa ya kuwa na wabunge hao.

Ngoja niangalie jumla ya kura na uwiano wake nione kama CHADEMA ina qualify kutoa wabunge wa viti maalumu ( Wanawake)

Nitarejea.

Maendeleo hayana vyama!
 
Lakini nadhani Halima Mdee hawezi kwenda, maana atakuwa amekubaliana na dhuluma hii.

Na ndiyo maana kamanda Khenan ambaye kapata ushindi jimboni, amesema yuko tayari kugoma kwenda bungeni endapo chama kitamtaka kufanya hivyo.
 
Halima aligombea pia viti maalum, ndio uone watu walivyo wabinafsi.
Mtu anagombea nafasi mbilimbili, ili akikosa moja apate nyingine
Siyo kwamba aligombea. Lumumba bhana, yaani huna unachojua. Anapata viti maalumu kutokana na nafasi yake ktk chama. Yeye ni mwenyekiti taifa wa BAWACHA.

Hata CCM mwenyekiti UWT anaingia viti maalumu kwa nafasi yake.
 
Hiyo percent uliyoitaja ni ya urais waliyoipata, inayozingatiwa kwenye kupata nafasi za ubunge wa viti maalumu ni percent ya kura za ubunge chama kilizopata kwa nchi nzima, na inatakiwa iwe angalau 5% ndio chama kinakuwa na sifa ya kutoa wabunge wa viti maalumu.
Ok! Sawa.
 
Weye waamini kuwa Halima Mdee atarudi bungeni kwa tiketi ya viti maalum?

Mtu huyohuyo ambae ameondolewa kwenye kiti cha ubunge na Gwajima?

Sababu kubwa khasa itakuwa ni ipi?
 
Hiyo percent uliyoitaja ni ya urais waliyoipata, inayozingatiwa kwenye kupata nafasi za ubunge wa viti maalumu ni percent ya kura za ubunge chama kilizopata kwa nchi nzima, na inatakiwa iwe angalau 5% ndio chama kinakuwa na sifa ya kutoa wabunge wa viti maalumu.
Na kupata ruzuku!
 
Lakini nadhani Halima Mdee hawezi kwenda, maana atakuwa amekubaliana na dhuluma hii.

Na ndiyo maana kamanda Khenan ambaye kapata ushindi jimboni, amesema yuko tayari kugoma kwenda bungeni endapo chama kitamtaka kufanya hivyo.
Mi naombea chama kimtake afanye hivyo. Ili wananchi waliemchagua wajue kwamba yupo kwa ajili ya chama chake na siyo kwa ajili yao.
 
Mi naombea chama kimtake afanye hivyo. Ili wananchi waliemchagua wajue kwamba yupo kwa ajili ya chama chake na siyo kwa ajili yao.
Kwani chama kina wanyama? Nacho kinq wananchi. Kwahiyo akiikubali nafasi batili atakuwa kakubali kulitumikia tumbo lake
 
Wanatakiwa wapate angalau 5% ya jumla ya kura zote halali za ubunge ndo wataqualify kupata Viti Maalum.
Ukiwa na 5% unapewa wabunge wangapi? Au mgawo unakuwa sawa Kati ya chama chenye 80% na chenye 5%??? Tunaomba elimu hii tafadhali.
 
Back
Top Bottom