Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee atatimba Bungeni kwa tiketi ya Viti Maalum?

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee atatimba Bungeni kwa tiketi ya Viti Maalum?

Hesabu ngumu
Ila ikipatikana nafasi wapelekwe vichwa
Waliopata jura nyingi angalau kwenye ubunge..
Mfano Aliyekua mgombea dodoma mjin , rungwe, na vichwa wengine
Kwanza vinatambuliwa vyama vyenye hiyo angalau 5% ya kura za ubunge, kwa mfano cdm na ccm kwa sasa. Kisha unatafutwa uwiano tena wa kura zao za ubunge kwa hivyo vyama vyenye sifa tu. Kwa mfano kura za ujumla za ubunge za cdm ni x na za ccm ni y, kwa hiyo uwiano wa cdm utakuwa ni (x/(x+y))100% na wa ccm ni (y/(x+y))100%. Halafu huo uwiano utazidishwa na jumla ya viti maalumu vilipo kwa sasa kujua cdm na ccm wanapata nafasi ngapi ngapi. Ni wazi ccm watanufaika zaidi.
 
Wanachukua jumla idadi ya kura zote halali za ubunge wanagawanya kwa kura zote ilizopata chama halafu wanazidisha kwa 113 ambayo ni idadi ya wabunge wa Viti maalum inayotakiwa kuwa bungeni.
Uko sawa mkuu. Idadi ya 113 ni kutokana na 40% ya wabunge wote. Wabunge wote inajumuisha:264 wa kuchaguliwa majimboni+10 wa kuteuliwa na Rais+5 wanaoteuliwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar +1 (Mwanasheria mkuu wa Serikali ambaye anachukuliwa kuwa ni mbunge) +1 Speaker (kwa sababu Speaker anaweza kuwa siyo mbunge)
Hivyo 264+10+5+1+1=281
40/100×281=112.4 ambayo inakaribishwa na kuleta wabunge 113 wa viti maalum.
 
Mpango ulikuwa kuondoa cdm mazima.waingie wenyewe inatosha
 
Mi naombea chama kimtake afanye hivyo. Ili wananchi waliemchagua wajue kwamba yupo kwa ajili ya chama chake na siyo kwa ajili yao.
Mtaje mbunge wa CCM aliye kwaajili ya watu wake (wananchi).
 
Mi naombea chama kimtake afanye hivyo. Ili wananchi waliemchagua wajue kwamba yupo kwa ajili ya chama chake na siyo kwa ajili yao.
Mtaje mbunge wa CCM aliye kwaajili ya watu wake (wananchi)
 
Sisi tunataka bunge la kijani, hatutaki visingizio sijui viti maalum ndio vilikuwa vinapinga maendeleo, tunataka bunge lenye connection na rais ili tupate maendeleo yaliyokuwa yanahubiriwa
 
Halima aligombea pia viti maalum, ndio uone watu walivyo wabinafsi. Mtu anagombea nafasi mbilimbili, ili akikosa moja apate nyingine
Kanuni za cdm wanaanza na waliodhubutu kugombea ubunge jimboni
 
Siyo kwamba aligombea. Lumumba bhana, yaani huna unachojua. Anapata viti maalumu kutokana na nafasi yake ktk chama. Yeye ni mwenyekiti taifa wa BAWACHA.

Hata ccm mwenyekiti UWT anaingia viti maalumu kwa nafasi yake.
WEWE NDIO HUJUI, JINGA KABISA. HALIMA ALIGOMBEA VITI MAALUM KUPITIA CHADEMA WAKATI WA KURA ZA MAONI NA ALISHINDA.
 
Weye waamini kuwa Halima Mdee atarudi bungeni kwa tiketi ya viti maalum?

Mtu huyohuyo ambae ameondolewa kwenye kiti cha ubunge na Gwajima?

Sababu kubwa khasa itakuwa ni ipi?
Waliiba kura mkuu gwajima hakupata zaid ya 100 kituo chochote na moyo wake unajua
 
Waliiba kura mkuu gwajima hakupata zaid ya 100 kituo chochote na moyo wake unajua
Ni kwamba sisi humu JF tupo watu wa aina mbalimbali na sifa tofauti.

Wapo watu humu tukiongelea masuala fulani ni lazima wengine ujiulize hawa wanamaanisha nini?

Mimi niliwahi kusema humu kwamba Kawe ni moja ya majimbo ya kimkakati ambayo CCM ilikuwa imejiandaa kuyapigania kupitia sanduku la kura.

Sasa mmewahi kujiuliza Kawe ni jimbo la kimkakati kwa vipi na ni kwanini CCM inalitaka jimbo hilo?

Lakini si mliona kampeni za Gwajima Kawe?

Lakini Halima Mdee hakuliona hilo na badala yake mkaanza mizaha ya kejeli na kashfa kwa Gwajima.

Wakati mwafanya hivyo mitandaoni, mwenzenu Gwajima akawa pia afanya vikao na wananchi vijiweni akijibu masuali ya papo kwa hapo huku akiomba kura.

Baadae "full CCM Machine" ikaingia Kawe tena kwenye mvua kuomba kura?

Alichofanya Halima Mdee kwenye siku ya kampeni ambayo alipaswa kutema hoja za msingi za kuomba tena kura kwa wananchi ,unakijua.

Sasa msilalamike.
 
Ni kwamba sisi humu JF tupo watu wa aina mbalimbali na sifa tofauti.

Wapo watu humu tukiongelea masuala fulani ni lazima wengine ujiulize hawa wanamaanisha nini?

Mimi niliwahi kusema humu kwamba Kawe ni moja ya majimbo ya kimkakati ambayo CCM ilikuwa imejiandaa kuyapigania kupitia sanduku la kura.

Sasa mmewahi kujiuliza Kawe ni jimbo la kimkakati kwa vipi na ni kwanini CCM inalitaka jimbo hilo?

Lakini si mliona kampeni za Gwajima Kawe?

Lakini Halima Mdee hakuliona hilo na badala yake mkaanza mizaha ya kejeli na kashfa kwa Gwajima.

Wakati mwafanya hivyo mitandaoni, mwenzenu Gwajima akawa pia afanya vikao na wananchi avijiweni akijibu masuali ya papo kwa hapo huku akiomba kura.

Baadae "full CCM Machine" ikaingia Kawe tena kwenye mvua kuomba kura?

Alichofanya Halima Mdee kwenye siku ya kampeni ambayo alipaswa kutema hoja za msingi za kuomba tena kura kwa wananchi ,unakijua.

Sasa msilalamike.
Jibu maswali yako mawili uliyoyaacha.
1. Kwanini Kawe ni jimbo la kimkakati?
2. Kwanini CCM ililitaka ?
 
Back
Top Bottom