Kura za Urais hazihojiwi popote wao wanaruhusu uongelee za ubunge tu so hoja itafia hapo hapo.
Then police wapo kwenye video na wali detain hizo kura kma ushahidi maana ni mali ya NEC wasingeweza waachia CHADEMA.
Kingine kma hizo kura zilikua planted na CHADEMA je kwanini hawajawakamata kwa forgery? Au ina maana CHADEMA wana access na kura za NEC kabla hazijapigwa? Je kma CHADEMA tu wameweza pandikiza kura feki waichafue CCM ina maana kumbe mtu yeyote anaweza access hizo karatasi kirahisi sana? Huoni mnazidi kuonyesha uchaguzi ulivuokua compromised!!
Kazi ya waangalizi sio kukagua kura bali kuangalia process tu. Mfano walemavu wana vyokua handled, uchaguzi kufuata kanuni zilizopo, hayo ya kura bandia au halali sio kazi yao afterall wao wanachukua sample ya vituo. Kwa nchi nzima wameenda vituo 80 pekee kati ya vituo elfu 80!! Sidhani kama nahitaji kuelezea zaidi.
"Irregularities" ipo kila chaguzi, hivyo hakuna uchaguzi wa asilimia 100 perfect.
Narudia kusema hivi, ikiwa Chadema wanadai kulikuwa na kura feki walipaswa kuzipeleka polisi ambao nao wangewasiliana na NEC.
Pili, kwa kuwa kulikuwepo na wawakilishi wa balozi za nje pale Kawe wao nao pia wangepewa hizo nakala ili watafute authentication yake ikiwemo hata kupeleka kwenye "international court".
Hivi wafahamu balozi za Ujerumani na Uingereza haziungi mkono kinachofanywa na balozi wa Marekani hapa nchini?
Lakini kupiga moto makaratasi hayo na kudai "tumekamata kura feki" hiyo ni ujinga.
Upinzani Tanzania haupo na nilikwishauondoa tangia uchaguzi wa 2015.
Mbowe, Zitto, Membe, Tundu Lissu na wengine kama kweli wana ushahidi wa wanachokiongea wapeleke madai mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Je, mmemtafuta Membe mbona yeye hajaongea lolote?
Vinginevyo, Tundu Lissu huenda akarudi Ubelgiji, Zitto Kabwe na Mbowe wakaendelea na maisha ya kawadia ambayo wana uwezo nayo.
Vijana walowatumia mitandaoni na kwingine ndo waathirika.
Kubalini matokeo, la mmeamua kuingia barabarani bila kibali basi Jumatatu mjidamke mlianzishe.