Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee atatimba Bungeni kwa tiketi ya Viti Maalum?

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee atatimba Bungeni kwa tiketi ya Viti Maalum?

Ukiwa na 5% unapewa wabunge wangapi? Au mgawo unakuwa sawa Kati ya chama chenye 80% na chenye 5%??? Tunaomba elimu hii tafadhali.
Kwanza vinatambuliwa vyama vyenye hiyo angalau 5% ya kura za ubunge, kwa mfano cdm na CCM kwa sasa. Kisha unatafutwa uwiano tena wa kura zao za ubunge kwa hivyo vyama vyenye sifa tu. Kwa mfano kura za ujumla za ubunge za CHADEMA ni x na za CCM ni y, kwa hiyo uwiano wa cdm utakuwa ni (x/(x+y))100% na wa ccm ni (y/(x+y))100%. Halafu huo uwiano utazidishwa na jumla ya viti maalumu vilipo kwa sasa kujua CHADEMA na CCM wanapata nafasi ngapi ngapi. Ni wazi CCM watanufaika zaidi.
 
Halima Mdee kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa Bawacha ndio mbunge wa viti maalumu namba moja kama Chadema itapata sifa ya kuwa na wabunge hao.

Ngoja niangalie jumla ya kura na uwiano wake nione kama Chadema ina qualify kutoa wabunge wa viti maalumu ( Wanawake)

Nitarejea.

Maendeleo hayana vyama!
Una hamu sana Halima awepo bungeni?
 
Ukiwa na 5% unapewa wabunge wangapi? Au mgawo unakuwa sawa Kati ya chama chenye 80% na chenye 5%??? Tunaomba elimu hii tafadhali.
Wanachukua jumla idadi ya kura zote halali za ubunge wanagawanya kwa kura zote ilizopata chama halafu wanazidisha kwa 113 ambayo ni idadi ya wabunge wa Viti maalum inayotakiwa kuwa bungeni.
 
Yule dada aliekuwa amejipa kazi ya kuhamasisha watu kuhusu mikutano mbali mbali ya Lisu na sometimes baadhi ya mikutano ya wabunge wa cdm siku mbili hizi simuoni humu jukwaani aidha kwa kuchangia nyuzi mbali mbali au kuleta uzi wake mwenyew kama alivyokuwa anafanya siku za nyuma. Nahisi yule ndio alikuwa halima mdee mwenyew!
 
Hiyo percent uliyoitaja ni ya urais waliyoipata, inayozingatiwa kwenye kupata nafasi za ubunge wa viti maalumu ni percent ya kura za ubunge chama kilizopata kwa nchi nzima, na inatakiwa iwe angalau 5% ndio chama kinakuwa na sifa ya kutoa wabunge wa viti maalumu.
Maccm hayanaga akili mkuu, hayajui hata nchi inaenda vipi. Sijui yamesomea shule gani na vyuo gani?. Au ndio wale wanaomaliza PHD hata kutamka sentence mbili za kingereza tabu, huku yamefundishwa kwa kingereza.
 
Hahahahaha huijui sababu ni ipi au umeamua kujitoa ufahamu? 😳😳😳

Weye waamini kuwa Halima Mdee atarudi bungeni kwa tiketi ya viti maalum?

Mtu huyohuyo ambae ameondolewa kwenye kiti cha ubunge na Gwajima?

Sababu kubwa khasa itakuwa ni ipi?
 
Na kupata ruzuku!
Ruzuku inawahusu vyama vilivyo na uwakilishi bungeni tu, hata kama kuna chama kina mbuge mmoja kitapata mgao wake wa ruzuku. Uwiano wa ruzuku kwa kila chama chenye uwakilishi bungeni unazingatia uwiano wa idadi ya wabunge wa chama husika. Kwa hiyo ccm itapiga hela ya kutosha.
 
Uje kabisa na estimate ya ruzuku ya chama, kwa sababu hiyo ndiyo muhimu zaidi kwa mwenyekiti wa chama wa maisha!
 
Yule dada aliekuwa amejipa kazi ya kuhamasisha watu kuhusu mikutano mbali mbali ya Lisu na sometimes baadhi ya mikutano ya wabunge wa cdm siku mbili hizi simuoni humu jukwaani aidha kwa kuchangia nyuzi mbali mbali au kuleta uzi wake mwenyew kama alivyokuwa anafanya siku za nyuma. Nahisi yule ndio alikuwa halima mdee mwenyew!
Erythrocyte unaitwa hukuuu??!!
 
Kwanza vinatambuliwa vyama vyenye hiyo angalau 5% ya kura za ubunge, kwa mfano cdm na ccm kwa sasa. Kisha unatafutwa uwiano tena wa kura zao za ubunge kwa hivyo vyama vyenye sifa tu. Kwa mfano kura za ujumla za ubunge za cdm ni x na za ccm ni y, kwa hiyo uwiano wa cdm utakuwa ni (x/(x+y))100% na wa ccm ni (y/(x+y))100%. Halafu huo uwiano utazidishwa na jumla ya viti maalumu vilipo kwa sasa kujua cdm na ccm wanapata nafasi ngapi ngapi. Ni wazi ccm watanufaika zaidi.
Asante sana mkuu kwa elimu hii.
 
Wanachukua jumla idadi ya kura zote halali za ubunge wanagawanya kwa kura zote ilizopata chama halafu wanazidisha kwa 113 ambayo ni idadi ya wabunge wa Viti maalum inayotakiwa kuwa bungeni.
Asante Sana kwa ufafanuzi wako mkuu. Umenifuta ujinga ktk hili.
 
Article 66 (1) (b) of URT Constitution 1977; inasema women members of not less than 30% elected on the basis of propirtion of votes among the political parties, hii inasomwa pamoja na Article 78.

Simply, wenye wabunge wengi wa majimboni ndio watapata asilimia kubwa ya viti maalum.
 
Na ndiyo maana kamanda Khenan ambaye kapata ushindi jimboni, amesema yuko tayari kugoma kwenda bungeni endapo chama kitamtaka kufanya hivyo.
Hiyo itakuwa big mistake. Akigoma kwenda bungeni na uchaguzi ukarudiwa hawezi kushinda.
 
Back
Top Bottom