Kuna Gari 400 plus za Halmashauri zote Tanzania kuna Halimashaur unakuta ina gari 3, Mkrugenzi gari lake na watumishi wengine gari zao kwa ujumla Arusha kuna Gari 500 na zaidi za Hamashauri Tanzania nzima.
Sasa chukulia kwa mfano Hamashauri za Mkoa wa Lindi wakaamua kuungana na Mtwara wakachukua Yutong moja safi kabisa wakaja nayo Arusha je jua halitazama? Arusha wakifika wanaweza kodi Tax za kuwapeleka nkutanoni na kuwarudisha Hotelini, lakini kwa Taifa ambalo kuanzia Mkuu hadi Chini ni watu wa matumizi hili haliwezekani.
Mzigo unaishia kwa kuongeza Tozo kwa raia ili kuhudumia Haliamshauri kwa sababu ya matumizu ya anasa. Ukiwakuta juu ya majukwaa wanalia lilio cha Mamba kwa shida za wananchi.
Arusha kwa leo ukikata kona ni unakutana na gari za Halamashauri mara Kibondo mara kishapu mara Manyoni hapo bado ma V8 ya Wakurugenzi ambayo hayana maandishi yoyote.
Na hapo anaye fungua mkutano utasikia anawaambia waongeze juhudi kwenye kuhudumia raia, Huku nje ya ukumbi kukiwa na Magari 400 plus, na hapo hapo Vijijini kumejaa project zinazo aendeshwa kwa michango ya wananchi wanao changishwa kwa nguvu na wala sio kwa hiari yao.
Hawa ndio watawala tunangoja watufikishe uchumi sawa na Veitanam au Thailand au Malaysia.
Ukiwakuta Viongozi wajuu kama Raisu, Waziri Mkuu na Makamo wa Raisi wanavyo lia utajua wako Serious na kuinua hali za maisha ya wananchi kumbe ni hadaaa tupu. Hakuna kiongozi ndani ya CCM yuko intrested kuondoa umasikini.