konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,696
- 8,763
Nakumbuka kila kiongozi mwandamizi wa serikali ya awamu ya 4 akiwa kwenye tv alikuwa anahubiri ukomo wa tatizo la umeme pale mradi wa umeme wa gesi ya Mtwara utakapokamilika.
Kulikuwa na uzinduzi mwingi tu sijui wa Kinyerezi one, sijui terminal two. Tulihakikishiwa mradi ukikamilika hakutakuwa tena na tatizo la umeme.
Hivi watanzania ndio kusema hatukumbuki kama tuliahidiwa hivyo? Na kama tunakumbuka kwa nini tupo kimya tu hata hatuhoji utadhani hatukuwahi kuahidiwa kitu kama hiki na serikali yetu?
Bila aibu tunaletewa mipango mingine mipya na kuahidiwa tatizo la umeme linaenda kuisha ilihali juzi tu tulipewa ahadi kama hiyo na haikutimia.
Natamani watanzania wawe na ujasiri wa kuwahoji viongozi wao vitu kama hivi. Haiwezekani tunaahidiwa kitu flani, gharama kubwa inatumika na pengine maisha ya watu yanapotea (refer vurugu za Mtwara kwenye kusafirisha gesi kuja Dar) lakini Serikali inakuja na mpango mwingine kana kwamba haijawahi kuwa na mpango kama huo kabla.