Je, Hayati Magufuli alikuwa na hirizi ya simba?

Je, Hayati Magufuli alikuwa na hirizi ya simba?

Pamoja na madhaifu yake meeeengi....
Lakini alileta nidhamu na uwajibikaji.
Pia wezi na mafisadi walimuogopa kwasababu alizijua njia zao kwakua aliishi kwenye mfumo tangu wakati wa BM.
Alikua na uchungu na rasilimali za taifa pia alikua alikua na maono yake kwa taifa.
Aliwapenda wanyonge na nakupenda masikini aonewe.
Alisimamia kile alicho kiamini hata kama alikua anaumiza wengine, lakini alisisitiza msimamo wake.
Shida one man show badala ya mfumo
 
Moja ya chanzo cha umasikini ni kuamini huu upuuzi wa ushirikina.
Nchi yetu imejengwa kwenye msingi huu, ndio maana ina mwenge, na taifa linatumia mabilioni kufanya ibada za mwenge. Tunaamini mwenge unaleta amani na tumaini. Ila mwaka 1978 hatukuupeleka mwenge frontline tulipeleka vijana wetu wakafe
 
Hizi imani za kijinga ni moja ya sababu kubwa watu wengi wa Tanzania bado wanaogelea kwenye lindi la umasikini.
Screenshot_20230626-112051_1.jpg


Usome hiki kitabu sawa mkuu then urudi hapa kujadili...
 
Magufuli alikuwa ni mtawala anayeogopwa sana. Ukiitwa ofisini kwake unapatwa na ubaridi yabisi hadi kwenye mifupa.

Watu wote tulimuogopa sana. Nchi nzima hakuna aliyeweza kumnyooshea kidole.

Wataalam wa mambo yasiyoonekana wanasema ili uweze kuwa na kaliba ile ni lazima uwe na hirizi ya Simba. Je, Rais wetu alikuwa na hiyo hirizi?



Alikuwa na hirizi ya fisi ndio maana alikuwa na tamaa sana na aliwaibia watu pesa zao kuanzia yale maduka ya kubadilisha pesa mpaka bank
 
Ukiona mtu anajitangaza tangaza sana kwamba yeye ni mtu wa Mungu, huku akiwa hajali utu wa mtu, wala maisha ya watu, anaongea uwongo hadi madhabahuni, huyo mtu lazima awe mchawi.
Magu alikuwa kiboko ya wapumbavu, wajinga, wazembe, wezi na mataahira yote aina ya Rostam.

Hungeweza kuona bandari inauzwa kwa wajomba kisha kina Rostam wanatokea kutetea katika awamu yake
 
Wengine walitumia mikia ya wanyama kabla ya kuanza kuhutubia waliipunga hewani wakasema Nyayo harambee... wote kimya mnapigwa baridii hakuna mwenye wazi la kumpinga hata mmoja.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Acha bwana!
 
Pamoja na madhaifu yake meeeengi....
Lakini alileta nidhamu na uwajibikaji.
Pia wezi na mafisadi walimuogopa kwasababu alizijua njia zao kwakua aliishi kwenye mfumo tangu wakati wa BM.
Alikua na uchungu na rasilimali za taifa pia alikua alikua na maono yake kwa taifa.
Aliwapenda wanyonge na nakupenda masikini aonewe.
Alisimamia kile alicho kiamini hata kama alikua anaumiza wengine, lakini alisisitiza msimamo wake.
Well said
 
Huwezi ukawa mtawala usiwe mshirikina,thus tangu kuumbwa kwa dunia hakuna mtawala yeyeto Duniani aliyefaulu kuingia mbinguni.
Huwezi tenganisha utawala na kafara ya damu za watu Kama shukrani kwa shetani ili kulinda utawala.
Uliona nadhani masiku ya kusimikwa mfalme wa sasa wa uingereza namna matambiko yalivokuwa yanafanyika.
Huku kwetu yakifanyika mnasema ushirikina kwa wazungu mnasema Ni jadi yao.
 
Sijui kuhusu swala la yeye kuvaa hirizi ila katika nchi hizi za KiAfrica ni ngumu sana kiongozi kwenye nyadhifa yoyote ya maana kujitanganisha na ushirikina.

Kanuni ni moja tu, wewe uliyepo kwenye hiyo nyadhifa usipokuwa mtu wa ndumba basi wanaokuzunguka watazitumia dhidi yako, kwasababu hapo ulipo hata wenzako wanapataka vilevile.

Maofisini mambo sio lelemama, na wanaotaka kuaminisha watu hapa kuwa mambo ni simple basi ni either wanaficha au ni waropokaji ambao hawajawahi kuwepo kwenye nyadhifa.
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom