Je, Hayati Magufuli alikuwa na hirizi ya simba?

Je, Hayati Magufuli alikuwa na hirizi ya simba?

hii mambo ya ndumba za kuvaa hirizi au kuchanjia sura za wanyama zipo lakini kwa mwendazake sijui ingawa alikuwa na utiisho kweli kweli.

kuna mzee mmoja kwetu alikuwa jamii ya magufuli alikuwa akiogopeka sana akitokea mahali mtastuka akiingea jambo wote mtakubaliana nae. ukiikingia kwenye anga zake umekwisha! likaibuka jina la chui akawa anaitwa chui.
huyu mzee pia ni muumini wa ushirikina

nikaja nikaunganisha dot nikagundua huyu mzee aliunganisha (Maagano)damu yake na mnyama chui ili aogopeke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na madhaifu yake meeeengi....
Lakini alileta nidhamu na uwajibikaji.
Pia wezi na mafisadi walimuogopa kwasababu alizijua njia zao kwakua aliishi kwenye mfumo tangu wakati wa BM.
Alikua na uchungu na rasilimali za taifa pia alikua alikua na maono yake kwa taifa.
Aliwapenda wanyonge na nakupenda masikini aonewe.
Alisimamia kile alicho kiamini hata kama alikua anaumiza wengine, lakini alisisitiza msimamo wake.
Wengi wanaomchukia jiwe ni wezi au wazembe, ndio hao hao walimuogopa, watumishi waliokuwa wanajituma awamu ya jiwe walikula teuzi
 
Nilipokuwa nafanya kazi TANROADS kuna uzembe fulani ulifanyika ofisini. Mkurugenzi wa idara pamoja na mimi tulipigiwa simu twende ofisini kwake. Yule m'baba hakuwa wa kawaida aisee
hii chai wewe
 
Attachments

  • images(5).jpeg
    images(5).jpeg
    9.9 KB · Views: 2
Pamoja na madhaifu yake meeeengi....
Lakini alileta nidhamu na uwajibikaji.
Pia wezi na mafisadi walimuogopa kwasababu alizijua njia zao kwakua aliishi kwenye mfumo tangu wakati wa BM.
Alikua na uchungu na rasilimali za taifa pia alikua alikua na maono yake kwa taifa.
Aliwapenda wanyonge na nakupenda masikini aonewe.
Alisimamia kile alicho kiamini hata kama alikua anaumiza wengine, lakini alisisitiza msimamo wake.
Kwani watumishi wa serikali hawakuwa wanyonge kwa nini aliwanyima haki zao za kisheria
 
ulikuwa humjui ndugu yangu, yule alikiuwa anatisha, huo utiisho alikuwa nao. hata hali ya hewa tu ilikua inabadilika eneo alipo.
Thubutu zake, yaani mtu akiwa na kiburi cha madaraka tu ndio mnuona ana sifa zote hizo?!
 
Nilipokuwa nafanya kazi TANROADS kuna uzembe fulani ulifanyika ofisini. Mkurugenzi wa idara pamoja na mimi tulipigiwa simu twende ofisini kwake. Yule m'baba hakuwa wa kawaida aisee
Huyo aliyekuwa anamuogopa ni wale watumwa wa ajira. Kuna mtu akikosa ajira anaweza hata kuolewa hapa mjini.
 
Achana na imani za kishirikina, aint no such thing as hirizi ya simba.
Ukali wake ulitosha kuweka hofu na si ushirikina
Wala hakuwa mkali, bali alikuwa ni mtu mwenye jazba. Nyerere ndio alikuwa mkali. Kuna tofauti kubwa kati ya jazba na ukali. Watu walikuwa wanaogopa mkihitilafiana kwa kuwa alikuwa na madaraka makubwa, alikuwa anaweza kuyatumia kukukomoa kwani katiba yetu ni dhaifu na rais ni mungu mtu.

Sasa unapokuwa na rais mwenye jazba, kisha mwenye kiburi cha madaraka hapo unajua nini kitatokea mkipishana. Lakini sio hiyo sijui hirizi ya Simba na upuuzi kama huo.
 
Back
Top Bottom