Katika pitapita zangu mtandaoni nimewahi kukutana na watu wengi wakilalamika kuhusu kufichwa kwa historia halisi ya Afrika na kufundishwa historia ya wakati wa ukoloni jambo hili nililipenda sana hasa kutokana kuwa mimi ni mtu nayependa kufukunya mambo mbalimbali, nilivyotafakari nikaona hii mada nikiileta jukwaa la historia JamiiForums basi naweza pata watu wa kunisapoti katika mjadala wangu.
1. Ugunduzi wa sarafu ya Kilwa huko Australia
Wengi tunaliskia bara hili la Australia mahali lilipo nidhani ni Mashariki mwa Afrika wanahistoria waliweza kugundua hii sarafu huko. Mnapo May 11 2019 gazeti la The Guardian liliweza kuandika hii habari na kujaribu kuelezea ni namna gan hili suala linaweza badilisha historia ya Afrika katika ile habari wanajaribu kusema kuwa huenda sarafu hiyo aidha ilipelekwa huko na Wareno waliofika Pwani ya Afrika Mashariki miaka hiyo.
Ndugu zangu mimi si msomi wa historia ila hapa lengo langu ni kuanzisha mada kwa wanahistoria na wengine wote hivo naomba mchango wenu katika mada hii ili tuweze kuelimishana zaidi kuhusu Afrika yetu
Hii ndio link ya taarifa kuhusu sarafu ya kilwa