Je, hii katuni ina ujumbe wa ukweli?

Je, hii katuni ina ujumbe wa ukweli?

Wanao pinga mkataba wa bandari wengi hawana sababu za msingi ni ushabiki tu huenda na ubaguzi na udini ila hoja hazina msingi.
Wakati tunapinga mkataba kwenye gas yetu ya Mtwara, kejeli zilikuwa kama hizi hizi toka kwa chawa wa Kikwete. Leo hii tunaambiwa gas sio yetu na wala hakuna zile faida tuliokuwa tunaambiwa. Hivyo hizi kejeli zenu sio mpya kabisa.
 
Acha kutukana mkuu leta hoja plz.
Hakuna anayekutana ila hilo swali la hicho kibonzo chenu halina maana, maana alipaswa kumuuliza ni wapi haelewi, ni kwenye IGA au HGA. Sasa yeye anamuuliza mkataba badala ya makubaliano. Mikataba ni siri nchi hii.
 
Kuna tabia ya kuuza mali za Tanganyika na kwenda mwanza na Arusha kupima upepo au hali ya hewa.

Masuala ya bangi yslikuwepo ila la bandari ni jipya.

Upepo hausomeki mama!!!

CCM wanakutapeli 100%
 
Ni kweli....wengi we know nothing ...ushabiki tu🤣
Na..... wengi we know nothing.... bali kuunga mkono tu.

Nilimsikia Msigwa akifafanua jana kwa waandishi wa habari ile yule mwandishi wa mwisho alipojaribu kumweleza vifungu vyenye utata kwenye mktaba au makubaliano hayo, yeye akapinga na kuwa mkali sana kiasi kuwa yule mwandishi aliamua kutouliza swali lake kabisa. Halafu kuna waandishi waliokuwa wanatamka kuwa wameelewa maelezo yake bila kujua mkataba au makubalinao yenyewe ni nini.
 
Na..... wengi we know nothing.... bali kuunga mkono tu.

Nilimsikia Msigwa akifafanua jana kwa waandishi wa habari ile yule mwandishi wa mwisho alipojaribu kumweleza vifungu vyenye utata kwenye mktaba au makubaliano hayo, yeye akapinga na kuwa mkali sana kiasi kuwa yule mwandishi aliamua kutoluiza swali lake kabisa. Halafu kuna waandishi waliokuwa wanatamka kuwa wameelewa maelezo yake bila kujua mktaba au makubalinao yenyewe ni nini.
🤣🤣🤭Tabu tupu
 
Na wewe unaepinga umeingiziwa sh ngapi?!!
Hakuna thamani ya pesa inayoweza kununua msimamo wangu juu ya maslahi ya Tanzania na wananchi wake.

Sitashangaa kama huelewi nilichoandika hapa..

Ninakukumbuka sana, kwa tuliyobadilishana hivi karibuni, humu humu JF. Kwa hiyo siwezi kushangaa kwa swali hilo.
 
Huyo SweetyCandy alitaka tupinge mwaka 2021?!
Hata bila ya kujua kuna uhujumu huo unaopangwa dhidi ya nchi yetu.

Wameifanya kuwa siri kubwa hadi mwisho, baada ya kumaliza kila kitu ndipo wanatuletea, tena kwa ujanja ujanja.
Njia hii ya kufanya mambo gizani ndio ushahidi mkubwa wa hila wanazofanya.
 
Hakuna thamani ya pesa inayoweza kununua msimamo wangu juu ya maslahi ya Tanzania na wananchi wake.

Sitashangaa kama huelewi nilichoandika hapa..

Ninakukumbuka sana, kwa tuliyobadilishana hivi karibuni, humu humu JF. Kwa hiyo siwezi kushangaa kwa swali hilo.
Haya mkuu, ili mtu awe mzalendo basi lazima afikiri na kupita kwa njia zenu tu mzipendazo.......kinyume na hapo si mzalendo. Hapo ndo penye tatizo
 
Hata bila ya kujua kuna uhujumu huo unaopangwa dhidi ya nchi yetu.

Wameifanya kuwa siri kubwa hadi mwisho, baada ya kumaliza kila kitu ndipo wanatuletea, tena kwa ujanja ujanja.
Njia hii ya kufanya mambo gizani ndio ushahidi mkubwa wa hila wanazofanya.
Ni waroho sana na wahujumu wakubwa. Hawaridhiki na walivyokwishaiba.
Isingekuwa kanuni ya kwamba IGA lazima iwe ratified, tusingejua kitu.

Ukitaka ujue mazeri ni msanii...subiri uone list ya mashirika ya umma ambayo Mhazina Mchechu atampelekea yafutwe/yauzwe. Ni hatari..
 
Haya mkuu, ili mtu awe mzalendo basi lazima afikiri na kupita kwa njia zenu tu mzipendazo.......kinyume na hapo si mzalendo. Hapo ndo penye tatizo
Sijazungumzia sifa zozote zinazomfanya mtu kuwa "mzalendo" mahali popote; lakini hilo halikukuzuia wewe kuleta jambo ambalo halijazungumziwa kabisa!
Huoni maajabu hayo?

Sasa ngoja nikueleze ninavyoufahamu uzalendo mimi, kwa kifupi tu.

Siyo mtu anayejitangaza kwa wengine kuwa yeye ni mzalendo, kwa mfano kwa kuvaa makofia, maskafu ya nguo, n.k.

Na wala siyo kupiga kelele nyingi juu ya uzalendo huku matendo yakionyesha tofauti kabisa

Mzalendo ni kwa matendo ya mtu husika kwa mambo yanayohusu taifa lake na watu wa taifa hilo. Huyu mtu hahitaji kujitangaza, ni watu hao hao ndio watakaoona matendo ya huyo mtu, na kukubali uzalendo wake.

Kama Samia anafanya matendo anayojua yataliumiza taifa lake na wananchi wake, kiongozi huyu hastahili kabisa kuwa na sifa za uzalendo, bali atakuwa ni Haini kwa nchi yake. Na hasa anapotahadharishwa juu ya mambo anayoyafanya, halafu yeye anakaza shingo kama hao wanaompigia kelele wote ni vichaa, huoni ulaghai wa kiongozi wa namna hiyo?

Kama unatetea mtu kama huyo, na unaona wazi kabisa matendo yake siyo ya kizalendo, wewe unayetetea uzalendo utautoa wapi huo uzalendo?
 
Ni waroho sana na wahujumu wakubwa. Hawaridhiki na walivyokwishaiba.
Isingekuwa kanuni ya kwamba IGA lazima iwe ratified, tusingejua kitu.

Ukitaka ujue mazeri ni msanii...subiri uone list ya mashirika ya umma ambayo Mhazina Mchechu atampelekea yafutwe/yauzwe. Ni hatari..
Huyu mtu hajapigiwa kura na mtu yeyote, pamoja na kwamba uchaguzi uliowaweka madarakani ulikuwa wa hovyo; na mbaya zaidi, huyo aliyekuwa anamsaidia alikuwa na msimamo ambao yeye kaugeuza kabisa na kufanya kinyume chake!

Ni hapa Tanzania pekee unapoweza kukuta kiongozi wa namna hiyo anafanya anavyotaka kufanya mwenyewe, bila ya kuhojiwa na yeyote.

Kwingine, huyu mama angefungashiwa vilago mapema sana na kutupwa nje, lakini siyo Tanzania.

Tuna matatizo sana na upole wetu huu.
 
Wanao pinga mkataba wa bandari wengi hawana sababu za msingi ni ushabiki tu huenda na ubaguzi na udini ila hoja hazina msingi.
Hoja ya ubaguzi wa udini imeletwa na wanao unga mkono na ni Hoja dhaifu sana kujificha nyuma yake
 
Back
Top Bottom