MSUKUMA02
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 1,454
- 3,978
Shalom shalom watanzania! Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja.
Hivi ni sahihi kwa mkuu wa mkoa wa mji mkubwa wa Dar es salaamu tena uliojaa matukio ya watu kutekwa, kupotezwa Hadi kuuliwa kutoa kauli hiyo mbele ya kadamnasi ya umma? Hivi hii kauli angeitoa kiongozi yeyote wa upinzani angekuwa salama kweli hata kwa nusu saa baada ya hapo?
Je sasa hivi suala la kupotezwa Tanzania limekuwa jambo la kawaida ndani ya utawala huu kiasi kwamba Hadi mkuu wa mkoa anasimama kifua mbele kwa kujiamini kuwa atampoteza Hadi familia yake imsahau?
Nina maswali mengi sana ya kujiuliza ndani ya kauli hii ya mkuu wa mkoa ila ngoja kwanza nitulie na mke wangu mama wawili tulee watoto wetu maana nchi ishakuwa ngumu hii