Invigilator
JF-Expert Member
- Aug 16, 2016
- 3,219
- 6,080
Wakuu, kwa hali ya mambo ilivyo ni dhahiri kuwa kwa mtu yeyote mwenye kuona mbali, mwenye mapenzi ya dhati na nchi yake na pia mwenye kuheshimu utu na haki za raia wenzake, kamwe hawezi kufurahishwa na ujinga huu unaondelea hapa nchini unaoitwa siasa.
Sote tunafahamu siasa inapofanyika kwa misingi ya usawa, ujenzi bora wa hoja na mtiririko mzuri wa mawazo (Train of Thought) huleta tija kwa taifa na maendeleo ya wananchi wake kwa ujumla.
Lakini itumiwapo tofauti kwa maslahi ya watu au kikundi kidogo huzua taharuki, kujenga chuki, migogoro na hata vifo. Kwa aina ya siasa tuliyonayo leo kama nchi si salama kwa maendeleo ya nchi, siasa isiyo huru, yenye kuegemea upande mmoja (one side based) wa kichama na kiitikadi, yenye kudhalilisha utu, kujenga chuki na kuamsha hasira.
Vyombo vya habari havipo huru, watu hawako huru kutoa mitazamo yao, kikundi kidogo tu kinataka watu wote zaidi ya milioni 60 tuwe na imani moja, itikadi moja, ufahamu mmoja, utadhani maroboti, kitu ambacho hakiwezekani.
Lugha za matusi ndizo ajenda, hakuna hoja, wala sera bora, ni ujivuni na umwamba tu ndio unaotamalaki, tufanyeni maamuzi ya dhati ndugu zangu aina hii ya siasa sio salama kwa afya ya kizazi chetu.
Fikria maneno hayo yangetolewa kwa waziri, mkuu wa mkoa au hata Rais tungeshuhudia nini leo? Upi ni mtazamo wako kwa siasi ya aina hii?