Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
Tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi Mkuu, mwaka huu Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC) imechapisha form ya kupigia kura kwa ngazi ya Urais wa JMT isiyo na mfumo rasmi wa mpangilio wa alfabeti.

Hii ni tofauti na form ya Urais wa Zanzibar chini ya ZEC ambayo imechapishwa kwa kufuata alfabeti. Form ya ngazi za wabunge na madiwani pia imefuata mtiririko huohuo.

Hii inaweza kuonekana jambo dogo machoni pa wengi, lakini katika fitna na mbinu za ushindi, Chama Cha Mapinduzi hapa kimecheza karata mahiri kwani mshindani na mpinzani mkubwa wa Mgombea Urais wa CCM ndugu Lissu amewekwa chini kabisa kwenye mpangilio wa Wagombea wote wa Urais.

Na kwa kuthibitisha hilo, mgombea Urais wa CCM akiwa Hedaru-Same amenukuliwa akisema:

"Wewe siku ya kupiga kura wala usihangaike kuangalia majina yote ya wagombea. CCM tupo juu kabisa ya wagombea wote, utamuona Mama Samia Suluhu, utamuona baba mmoja ana kaupara kazurikazuri hivi. Weka tiki hapo. Usihangaike kuangalia wagombea wengine, wale hawakuhusu. Angalia jina la juu ambapo CCM tupo mwanzo"

38C964E4-15B3-406F-9C96-30A4E350D16E.jpeg


Akaenda mbali zaidi akaongezea

CA555B2B-B494-46C8-AB07-E0E898E62D21.jpeg


"Watu wa Hedaru, huu ndio mfano wa karatasi ya kupigia kura. Mimi na Mama Samia Suluhu tupo mwanzo kabisa kwenye karatasi ya kupigia kura. Ukifika tu unaweka tiki kwangu, unachukua kwa Mbunge Mathayo na diwani. Hayo majina mengine huko usiangalie, tena kama majina ya huko chini usiangalie kabisa, unaweza kupofuka"

Hii ni mbinu nzuri ya ushindi, kuna maeneo watu hawajibiidishi na kutafuta jina la mgombea mshindani wa CCM, watatazama jina la mwanzo na kuweka tiki.

Na ili kuiboresha mbinu yao, sasa CHAMA CHA MAPINDUZI kimetoa karatasi ya mfano wa kupigia kura na mshindani wao mkuu amekatwa na haonekani, hii ni hatua ya mwanzo ya "kumuondoa" mgombea mwenye ushindani na chama chao na NEC inawajibika kutoa tamko kama "karatasi ya Mfano" ya kupigia kura inapaswa kuhaririwa kwa maslahi ya chama kimoja cha siasa, maana kutoa "karatasi ya mfano" isiyofanana na "karatasi rasmi" kwa kumkata mmoja wa wagombea inaleta maswali mengi.

Hii ni wiki ya lala salama, tunapohubiri amani, tukumbuke kuwa AMANI NI ZAO LA HAKI...Tutendeane haki ili kudumisha amani ya nchi.​

1603227074857.jpg
 
"Watu wa Hedaru,huu ndio mfano wa karatasi ya kupigia kura.Mimi na Mama Samia Suluhu tupo mwanzo kabisa kwenye karatasi ya kupigia kura.Ukifika tu unaweka tiki kwangu,unachukua kwa Mbunge Mathayo na diwani.Hayo majina mengine huko usiangalie,tena kama majina ya huko chini usiangalie kabisa,unaweza kupofuka"
Mkuu sisi tunamtaka yule wa mwisho kabisa kwani tunataka utawala wa sheria na katiba ifuatwe. Samahani kwa hilo mkuu wetu.
 
Na hizo ni mbinu za kizamani sana, CCM na Tume wanashindwa jitambua kuwa Dunia hairudi nyuma, inasonga mbele,tunaendelea kuwaelimisha wapiga kura. Na sisi tunawaambia usihangaike kusoma majina, angalia wa mwisho kabisa chini ya karatasi

2590581_Mfano_wa_Karatasi_ya_Kura__Uchaguzi_wa_Rais_2020__640_X_640_.jpg
 
Hili limeniongezea sababu ya kujiandaa kupiga kura kupitisha katika inayoivua time huo uwezo wa kufanya hizo manipulation .

CCM waoga aisee wangekuwa na uwezo hata Picha ya Lissu ingefifishwa au jina lingeandikwa kwa font ya kufifia kabisa.

Mbona tulikuwa tumejiandaa kuchagua JPM bila haya Mahila?
 
Badala ya kulalamika na kusubiri tume eti itoe tamko kwanini CCM wamekata karatasi ya mfano ni vema mngejikita kwenye kuwaelimisha wapiga kura wenu namna rahisi ya kumpigia kura mgombea wenu.

Kibaya zaidi mnapozidi kuijadili hiyo karatasi kuwa CCM wamewekwa wa kwanza, basi automatically mnazidi kuwasaidia CCM maana hata wale ambao walikuwa hawajui hilo watajikuta wanajua na wakanasa kwenye huo mtego wa kuweka tick kwa mgombea aliye juu zaidi. Ni bahati mbaya kwa vyama vya upinzani havijajifunza kutumia weekness ya CCM kama mtaji wao wa kujijenga. Na hata pia hawajajua kutumia changamoto wanazokutana nazo na kuzigeuza kuwa mtaji wao wa kisiasa.
 
Wamekosea sana kumuweka JPM pamoja na hawa wasio hata na chembe ya uzalendo. Wamekosea sana
 
Mkuu umeandika vyema sana ila lazma wafahamu kuwa Tanzania hii sio ya mwalimu Nyerere, kama Mh. T. Lissu atakuepo kwenye karatasi ya kura basi wamekwishaaaa. Otherwise wamkate tu.
Lissu yupo na hata robo ya robo ya kura za JPM hazifikii
 
Kama siku yako ya kuanguka imefika imefika hata uwe wapi! CHADEMA kuwa wa mwisho na CCM kuwa wa Kwanza wote wana probability sawa ya kuonwa tofauti na vyama vya katikati, na watu huwa lazima wasome karatasi ndo wapige kura, sasa anaanza kusoma CCM halafu anashuka na harudi juu tena kwa CCM ndipo balaa la CCM linapokuja
 
Badala ya kulalamika na kusubiri tume eti itoe tamko kwa nini CCM wamekata karatasi ya mfano ni vema mngejikita kwenye kuwaelimisha wapiga kura wenu namna rahisi ya kumpigia kura mgombea wenu..
Ni kweli kulalamika bila kuchukua hatua ni ujinga,,INA gharimu kiasi gani kutoa kopi za kutosha na kusambaza nakala za mfano huko kwa wananchi?
 
Back
Top Bottom