Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

Tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi Mkuu, mwaka huu Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC) imechapisha form ya kupigia kura kwa ngazi ya Urais wa JMT isiyo na mfumo rasmi wa mpangilio wa alfabeti...
Barafu, nimezunguka maeneo mengi sana ya Tanzania. Watanzania wenye akili timamu ni wengi sana, watanzania wasio na akili timamu ni wachache sana. Sioni shida na Tundu Lissu na Chadema wakisema ukienda kwenye karatasi ya kura nenda mwisho kabisa kuna picha ya Salum Mwalimu na Tundu Lissu alafu weka alama ya tiki kwenye kiboksi mbele ya Tundu Lissu.

Uzuri wa hili ni kuwa neno la kwenye Biblia linaenda kutimia mwaka huu kuwa “Wa Mwisho atakuwa wa Kwanza na wa kwanza atakuwa wa Mwisho “
Tukutane tarehe 29 Oktoba kuanza kusikiliza matokeo!
 
Uwoga umewashika, bado kidogo yatapiga vyupi vyenu

Chambo cha Mabeberu chali
 
Uwoga umewashika, bado kidogo yatapiga vyupi vyenu

Chambo cha Mabeberu chali
Andiko linaenda kutimia mwaka huu
4691784F-0373-4BD0-9C65-F9E38237483E.jpeg
 
Najarbu kuwaza lkn hainiingii akilin eti najua kabisa naenda kumpigia kura mzee wa ubwabwa alafu nishindwe hata kumtafuta yuko namba ngapi? Km kweli watu wanaweza kwenda na kushindwa kufanya hivyo basi lamda uchaguzi wa 2045 ndio tunaweza kuwa siriaz
 
Kunukuu na ku attached Mandiko mahali popote pale huwa hayakatai Kwa kuwa hayana mdomo wa kusema,

Kwani hata wachawi na majambazi hutumia Mandiko katika upumbavu Wao

Tukutane baada ya 28october kama hutokuja na ngonjera za kijinga kuzidi ujinga huu

Chambo chaliiii
Amini amini nakwambia, Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 ni Tundu Antiphas Lissu
4C5A1BEF-E8B4-4D1C-A83D-8C7EC4CDB671.jpeg
 
Tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi Mkuu, mwaka huu Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC) imechapisha form ya kupigia kura kwa ngazi ya Urais wa JMT isiyo na mfumo rasmi wa mpangilio wa alfabeti..
"Wewe siku ya kupiga kura wala usihangaike kuangalia majina yote ya wagombea. CCM tupo juu kabisa ya wagombea wote, utamuona Mama Samia Suluhu, . Weka tiki hapo. Usihangaike kuangalia wagombea wengine, wale hawakuhusu. Angalia jina la juu ambapo CCM tupo mwanzo
IMG-20201021-WA0034.jpg

utamuona baba mmoja ana kaupara kazurikazuri hivi
 
mzee umejikunja balaa
unaowasemea tayari tumeambiwa wana tiket za ndege .
uanlijua hilo.
ushauri: angalia kuwa mstaarabu usilete taharuki.
 
Huenda
Tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi Mkuu, mwaka huu Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC) imechapisha form ya kupigia kura kwa ngazi ya Urais wa JMT isiyo na mfumo rasmi wa mpangilio wa alfabeti.

Hii ni tofauti na form ya Urais wa Zanzibar chini ya ZEC ambayo imechapishwa kwa kufuata alfabeti. Form ya ngazi za wabunge na madiwani pia imefuata mtiririko huohuo.

Hii inaweza kuonekana jambo dogo machoni pa wengi, lakini katika fitna na mbinu za ushindi, Chama Cha Mapinduzi hapa kimecheza karata mahiri kwani mshindani na mpinzani mkubwa wa Mgombea Urais wa CCM ndugu Lissu amewekwa chini kabisa kwenye mpangilio wa Wagombea wote wa Urais.

Na kwa kuthibitisha hilo, mgombea Urais wa CCM akiwa Hedaru-Same amenukuliwa akisema:

"Wewe siku ya kupiga kura wala usihangaike kuangalia majina yote ya wagombea. CCM tupo juu kabisa ya wagombea wote, utamuona Mama Samia Suluhu, utamuona baba mmoja ana kaupara kazurikazuri hivi. Weka tiki hapo. Usihangaike kuangalia wagombea wengine, wale hawakuhusu. Angalia jina la juu ambapo CCM tupo mwanzo"

Akaenda mbali zaidi akaongezea

"Watu wa Hedaru, huu ndio mfano wa karatasi ya kupigia kura. Mimi na Mama Samia Suluhu tupo mwanzo kabisa kwenye karatasi ya kupigia kura. Ukifika tu unaweka tiki kwangu, unachukua kwa Mbunge Mathayo na diwani. Hayo majina mengine huko usiangalie, tena kama majina ya huko chini usiangalie kabisa, unaweza kupofuka"

Hii ni mbinu nzuri ya ushindi, kuna maeneo watu hawajibiidishi na kutafuta jina la mgombea mshindani wa CCM, watatazama jina la mwanzo na kuweka tiki.

Na ili kuiboresha mbinu yao, sasa CHAMA CHA MAPINDUZI kimetoa karatasi ya mfano wa kupigia kura na mshindani wao mkuu amekatwa na haonekani, hii ni hatua ya mwanzo ya "kumuondoa" mgombea mwenye ushindani na chama chao na NEC inawajibika kutoa tamko kama "karatasi ya Mfano" ya kupigia kura inapaswa kuhaririwa kwa maslahi ya chama kimoja cha siasa, maana kutoa "karatasi ya mfano" isiyofanana na "karatasi rasmi" kwa kumkata mmoja wa wagombea inaleta maswali mengi.

Hii ni wiki ya lala salama, tunapohubiri amani, tukumbuke kuwa AMANI NI ZAO LA HAKI...Tutendeane haki ili kudumisha amani ya nchi.
HUENDA BAADHI YA FORM MAJINA YA WATU WA UPINZANI YAKAWA YAMEFIFISHWA KABISA ILI YASIONEKANE AIDHA HUENDA PIA KATIKA BAADHI YA FORM JINA LIKAONEKANA KATIKATI YA FORM
 
Back
Top Bottom