Uchaguzi 2020 Je, hii ndiyo sababu ya NEC kutochapisha fomu za wagombea Urais kwa "Alphabetical order"?

mzee umejikunja balaa
unaowasemea tayari tumeambiwa wana tiket za ndege .
uanlijua hilo.
ushauri: angalia kuwa mstaarabu usilete taharuki.
12CB1521-3BAC-45AB-8FBF-F08CF16D7012.jpeg
 
Kwa hiyo mkuu unataka kusema uwa watanganyika wengi bado ni wajinga kiasi hicho...??

Wapiga kura wengi ni wajinga na wavivu sana, usijisahaulishe huko vijijini hali ikoje kuhusu elimu.
 
Hakuna kitu rahisi kwa binadamu kama kuangalia mwanzo na mwisho.

Hapo hakuna walichofanya mwisho pia ni rahisi sana kuona!

Nakumbuka hata shule ilikua inatokea automatic tu unachek maswali ya kwanza, unageuza pepa mwisho na unajikuta unaanza mwisho kwenye maswali ya max nyingi
 
Wakati serikali ina hamasisha watu wajitokeze Kwenda kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi mkuu Chadema walikua wakihamasisha watu wasijitokeze Mbaka ipatikane katiba mpya.
 
Hivi hili suala mbona sielewi. Yaani mtu umepanga kwenda kumchagua Lissu, halafu unafika kituoni unamkuta Magufuli amewekwa picha yake wa kwanza. Basi tu kwasababu Magufuli yupo wa kwanza unaghairi kumchagua Lissu, ambaye picha yake ipo mwisho, unaweka tick kwa Magufuli. Like seriously.
 
Tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi Mkuu, mwaka huu Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC) imechapisha form ya kupigia kura kwa ngazi ya Urais wa JMT isiyo na mfumo rasmi wa mpangilio wa alfabeti.

Hii ni tofauti na form ya Urais wa Zanzibar chini ya ZEC ambayo imechapishwa kwa kufuata alfabeti. Form ya ngazi za wabunge na madiwani pia imefuata mtiririko huohuo.

Hii inaweza kuonekana jambo dogo machoni pa wengi, lakini katika fitna na mbinu za ushindi, Chama Cha Mapinduzi hapa kimecheza karata mahiri kwani mshindani na mpinzani mkubwa wa Mgombea Urais wa CCM ndugu Lissu amewekwa chini kabisa kwenye mpangilio wa Wagombea wote wa Urais.

Na kwa kuthibitisha hilo, mgombea Urais wa CCM akiwa Hedaru-Same amenukuliwa akisema:

"Wewe siku ya kupiga kura wala usihangaike kuangalia majina yote ya wagombea. CCM tupo juu kabisa ya wagombea wote, utamuona Mama Samia Suluhu, utamuona baba mmoja ana kaupara kazurikazuri hivi. Weka tiki hapo. Usihangaike kuangalia wagombea wengine, wale hawakuhusu. Angalia jina la juu ambapo CCM tupo mwanzo"

Akaenda mbali zaidi akaongezea

"Watu wa Hedaru, huu ndio mfano wa karatasi ya kupigia kura. Mimi na Mama Samia Suluhu tupo mwanzo kabisa kwenye karatasi ya kupigia kura. Ukifika tu unaweka tiki kwangu, unachukua kwa Mbunge Mathayo na diwani. Hayo majina mengine huko usiangalie, tena kama majina ya huko chini usiangalie kabisa, unaweza kupofuka"

Hii ni mbinu nzuri ya ushindi, kuna maeneo watu hawajibiidishi na kutafuta jina la mgombea mshindani wa CCM, watatazama jina la mwanzo na kuweka tiki.

Na ili kuiboresha mbinu yao, sasa CHAMA CHA MAPINDUZI kimetoa karatasi ya mfano wa kupigia kura na mshindani wao mkuu amekatwa na haonekani, hii ni hatua ya mwanzo ya "kumuondoa" mgombea mwenye ushindani na chama chao na NEC inawajibika kutoa tamko kama "karatasi ya Mfano" ya kupigia kura inapaswa kuhaririwa kwa maslahi ya chama kimoja cha siasa, maana kutoa "karatasi ya mfano" isiyofanana na "karatasi rasmi" kwa kumkata mmoja wa wagombea inaleta maswali mengi.

Hii ni wiki ya lala salama, tunapohubiri amani, tukumbuke kuwa AMANI NI ZAO LA HAKI...Tutendeane haki ili kudumisha amani ya nchi.

Uzuri uchaguzi huu wagombea ni wawili tu, wa juu na wa chini basi. Hapo ni rahisi sana, unafika chini kabisa kisha unamwaga maji. Na kizazi hiki watu wanavyojitambua, hata Lisu agewekwa nyuma ya karatasi, bado tutampa kura za ukweli.
 
Hivi hili suala mbona sielewi. Yaani mtu umepanga kwenda kumchagua Lissu, halafu unafika kituoni unamkuta Magufuli amewekwa picha yake wa kwanza. Basi tu kwasababu Magufuli yupo wa kwanza unaghairi kumchagua Lissu, ambaye picha yake ipo mwisho, unaweka tick kwa Magufuli. Like seriously.

Mpangilio rasmi ni wa alphabetical, aidha ni by ascending order au descending order, kinyume na hapo ni mbinu za kizee.
 
Tofauti na miaka mingine ya Uchaguzi Mkuu, mwaka huu Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC) imechapisha form ya kupigia kura kwa ngazi ya Urais wa JMT isiyo na mfumo rasmi wa mpangilio wa alfabeti.

Hii ni tofauti na form ya Urais wa Zanzibar chini ya ZEC ambayo imechapishwa kwa kufuata alfabeti. Form ya ngazi za wabunge na madiwani pia imefuata mtiririko huohuo.

Hii inaweza kuonekana jambo dogo machoni pa wengi, lakini katika fitna na mbinu za ushindi, Chama Cha Mapinduzi hapa kimecheza karata mahiri kwani mshindani na mpinzani mkubwa wa Mgombea Urais wa CCM ndugu Lissu amewekwa chini kabisa kwenye mpangilio wa Wagombea wote wa Urais.

Na kwa kuthibitisha hilo, mgombea Urais wa CCM akiwa Hedaru-Same amenukuliwa akisema:

"Wewe siku ya kupiga kura wala usihangaike kuangalia majina yote ya wagombea. CCM tupo juu kabisa ya wagombea wote, utamuona Mama Samia Suluhu, utamuona baba mmoja ana kaupara kazurikazuri hivi. Weka tiki hapo. Usihangaike kuangalia wagombea wengine, wale hawakuhusu. Angalia jina la juu ambapo CCM tupo mwanzo"

Akaenda mbali zaidi akaongezea

"Watu wa Hedaru, huu ndio mfano wa karatasi ya kupigia kura. Mimi na Mama Samia Suluhu tupo mwanzo kabisa kwenye karatasi ya kupigia kura. Ukifika tu unaweka tiki kwangu, unachukua kwa Mbunge Mathayo na diwani. Hayo majina mengine huko usiangalie, tena kama majina ya huko chini usiangalie kabisa, unaweza kupofuka"

Hii ni mbinu nzuri ya ushindi, kuna maeneo watu hawajibiidishi na kutafuta jina la mgombea mshindani wa CCM, watatazama jina la mwanzo na kuweka tiki.

Na ili kuiboresha mbinu yao, sasa CHAMA CHA MAPINDUZI kimetoa karatasi ya mfano wa kupigia kura na mshindani wao mkuu amekatwa na haonekani, hii ni hatua ya mwanzo ya "kumuondoa" mgombea mwenye ushindani na chama chao na NEC inawajibika kutoa tamko kama "karatasi ya Mfano" ya kupigia kura inapaswa kuhaririwa kwa maslahi ya chama kimoja cha siasa, maana kutoa "karatasi ya mfano" isiyofanana na "karatasi rasmi" kwa kumkata mmoja wa wagombea inaleta maswali mengi.

Hii ni wiki ya lala salama, tunapohubiri amani, tukumbuke kuwa AMANI NI ZAO LA HAKI...Tutendeane haki ili kudumisha amani ya nchi.
Kimsingi hili ni goli la Mkono, na ushahidi tosha kua Tume INATUMIKA.
 
Uxuri mgombea wangu wa chauma nimeona alipo nikifika sina cha kukawia

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom