Je, hii ni hali ya kawaida kwa wale wenye uzoefu?

Je, hii ni hali ya kawaida kwa wale wenye uzoefu?

Mimi katika hali hiyo, ningeomba Mungu nimalize chuo salama.nipate kazi, nitafute pesa zangu na maisha yangu ambacho ningepigania kwa kidg ni kama mzee angeuza nyumba ya mwanzo..Mzee hana kosa, anapewa usingizi ujue.
 
linapokuja swala la mapenzi hakuna mtu unaweza kumshauri akakuelewa....isitoshe wewe ni mtoto tu mambo ya baba hayakuhusu ata kidogo chamsingi soma uweze kuyaendesha maisha yako...ili kwenye maisha yako usije kufanya makosa kama anayo yafanya baba yako...ukitaka laana jaribu kuyaingilia mapenzi ya baba yako...utarudi hapa kutulilia...tengeneza maisha yako maisha ya mzazi wako hayakuhusu kabisa...alisikika mlevi mmoja
 
Kijana tafuta mali zako mwenyewe na sio kutegemea za mzazi wako. Kila binadamu amezaliwa uchi wa nyama hakuna anayezaliwa kashika mche wa dhahabu. Kufanikiwa ni juhudi za mtu binafsi. Shukuru Mungu wazazi wamewasomesha. Kuna watu hata wazazi hawana wamezaliwa na wamekuwa yatima.

Mzazi wako hana kosa kuwekeza kokote ndani ya nchi. Provided ndio maisha ameyachagua
 
Dogo nakushauri achana na huyo dingi umeshachelewa, stage aliyofikia ukimsema au kutaka kumshauri lolote ataenda kusema kwa mkewe utaonekana mbaya mwisho wa siku mtatengenezwa wote wawili
 
Dogo nakushauri achana na huyo dingi umeshachelewa, stage aliyofikia ukimsema au kutaka kumshauri lolote ataenda kusema kwa mkewe utaonekana mbaya mwisho wa siku mtatengenezwa wote wawili
Naam Sijui umejuaje!!! Kwamba akishauriwa kitu lazima taarifa zifike huko, lakini yote kwa yote nimeamua kuwaacha waishi kwa amani maana kubaki unashauri mara kwa mara ni kero kwa mzee pia@ kwa upande wangu natambua kwamba hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwangu, kwa hiyo Sina budi kupambana kwa hali na mali lakini vilevile kumwomba mwenyezi Mungu nisijetenda haya ya mzee ya kuishi eneo la ukweni.
 
Nawashukuru wote ambao mmechangia mawazo yenu tena mazuri, nimepokea ushauri wenu na kuuchambua vizuri Kuna kitu nimepata kutokana na mawazo yenu na nimeshaanza kufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom