Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Huenda kinachompata Nay wa Mitego ndio sababu inayowaogopesha wasanii na kuamua kutangaza wao ni CCM kwani ukiwa CCM uko salama dhidi ya mkono hakuna baya litakupata.
Ila tumeoma wasanii waliokataa kuvaa kijani namna wanapelekeshwa na mkono wa dola, leo BASATA wamewaita kesho BASATA wamewafungia, kesho kutwa wameitwa kwa Pilato ili mradi tu kuwatia jambajamba waone kusimama na Wananchi na kuwafumbua macho ni kitanzi.
Je, Wasanii wa Tanzania ni kwa ajili ya kukibeba chama cha kijani kionekane kina wafuasi wengi na si kuiongoza jamii kutambua ukweli wa mambo ili waweze kufanya maamuzi sahihi?
Haya endeleeni kuwapa tuzo hao wanaoimba, chomeka, chomoa ingiza toa, weka mate ziteleze nk huku mkiwabugudhi wanaosema uwajibikaji kwa Taifa ni muhimu nyie si ndio mmeshika kwenye mpini nani atawasumbua na huku kashika kwenye makali bwana.
PIA SOMA
- BASATA waufungia wimbo wa Nay 'Nitasema'