Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Hata kama basi linaondoka saa 7 usiku siwezi chelewa, ni mipango tu, kuacha mda wa kutosha, na nusu saa ya zarura, ni discipline tu na kuwa in control.
Watanzania na muda ni maji na mafuta. Ukiwa mtu wa ku keep time utagombana na watu kila siku.
 
Watanzania na muda ni maji na mafuta. Ukiwa mtu wa ku keep time utagombana na watu kila siku.

Regardless, mimi na keep time, yani kuchelewa mahali ni mateso sana. Na watu wa karibu wamenizoea.
 
Nakumbuka ilikuwa Mwanza naenda musoma buzuruga pale gari likaniacha afu kuna mizigo yangu ndani ya gari. Nikachukua boda kulifuata akaniuliza umetokea wapi nikamwambia Dar, basi akawa anatembea mwendo mdogo namwambia tuwahi anasema atakamatwa na askari kukimbia. Mungu si Selemani kumbe tuliachwa kama mtu 5 so wakasimama kutusubiri maeneo ya makaburi ya MV bukoba pale. Nampa boda 5000 anataka 10,000 anasema tumetoka mbali, nikamwambia konda ampe 3000 maana sikuwa na heka ndogo zaidi ya 5000, napanda gari ananizuia mbona 3000 tena badala ya 10000 na 5000 unasepa nayo. Nikamjibu nauli ya boda ni 2000 mpaka hapa, huwezi kushukuru nimekupa 3000 , nilitaka kukupa 5000 ukaniona boya unataka 10, akajifanya mtata nikamwambia nimekulia nyakato na mlango mmoja , mji naujua kusikia nimetoka Dar usipagawe ukajua mzaramo ntakuvuruga. Akasepa.
 
We nae muwasho wako tu ungetulia kwenye bus yasingekukuta
 
Utaratibu mzuri sana.

Ukichelewa basi jamaa wanauza ile uliyochelewa wanakukatia nyingine ya muda unaofuata.
 
😁😁 muda mwingine ubabe unalipa
 
Si rudii tena hiiichezo niliachwa na gari nyegezi stand,naka3nda kuipata pale mizani Usagara. B0da kamaliza speed yote ile yaaani akikatisha ata inzi tulikuwa tumasagikaaa
 
Si rudii tena hiiichezo niliachwa na gari nyegezi stand,naka3nda kuipata pale mizani Usagara. B0da kamaliza speed yote ile yaaani akikatisha ata inzi tulikuwa tumasagikaaa
ni michezo ya hatari Mungu tu ndie anaesaidia
 
Chief umenikumbusha mbali tulifukuza bus la zuber tuulipata kamanga feri wale boda walidai pesa nying sana maana mwendo tulotembea nao sio kitoto
 
Kuna siku natoka Dom kwenda Arusha nimekata Shabiby. Siku hiyo nililala kahoteli flani kako karibu kabisa na ofisi za Shabiby sikakumbuki jina.

Bus lilikua linaondoka saa 1 kamili, picha linaanza nimeshtuka usingizini saa 1 kasorobo! Kwanza sikuamini macho yangu manake mi huaga mwepesi sana kuamka mapema. Aisee nilikurupuka, tupia manguo kwn begi, piga mswaki huku navaa. Nilitoka mkuku pale hotelini hata sijaaga. Mbio mpaka Shabiby nimefika saa 1 kasoro 5 sioni bus! Nauliza jamaa pale nje wananiambia mbona bus limetoka mda tu? Nikadata!

Ila nikatuliza akili nikasema mimi sikimbizi bus, kama nimechelewa nachukua lingine. Nikaingia mule ndani ofisini nikawafata wale wadada kuwaonyesha ticket na kuuliza vizuri wakaniambia tulia boss bus limechelewa kidogo linakuja soon. Ndio nikapumua
 
[emoji16][emoji16] ungeanza kulikimbiza, ungeshangaa lipo nyuma yako linakukimbiza wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…