Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Gari la kulikimbiza ni lile ambalo unajua kabisa mbele Kuna mzani ila kama hakuna na limeondoka kabla ya muda wahi kupiga simu LATRA kabla muda haujaenda inakuwa kama ushahidi wa kweli limeondoka kabla ya muda na litasimamishwa popote pale litakapokuwa limefika (angalizo huwa wanajitetea reporting time ni nusu saa kabla ya safari, nawe unajihami upo stand zaidi ya nusu saa Ubungo ulikuwa unalitafuta bus hukuliona baadae ukauliza ndo ukashangaa unaambiwa limeondoka)
 
Gharama ya kufukuza basi kwa boda Bora ununue tiketi ingine panda basi la nyuma
Mtu akiachwa na gari huwa anakuwa na wenge ila alishalipata bus baada ya kulifukuza ndo anakumbuka mambo ya gharama alizotumia.

Ni sawa na wengine, unakuta kasahau kubeba mswako labda yupo jirani na nyumbani anaichukua boda kufuata mswaki wa buku
 
Niko naelekea kigoma kabla ya stand ya chalinze km kama 5 hiv kuna vx iligongana na lori la mchanga sasa ikasababisha foleni
Nikashuka ku****a bwana nakuja kurud bus ishaondoka aiseee boda chap mpaka stand ya chalinze naikuta bus ndo inatoka boda anataka 5000 na mm nina 10 hana chench nilihahaaa aisee jirani yangu ndo akaniazima 5000
Betrice popote ulipo kunywa peps kwa mara nyingne ulinisave sana siku hiyo
 
Habari ya uzima wana JF moja kwa moja niingie ktk mada bila ya kupoteza muda Je..? umewahi kuachwa na bus au kuchelewa kufika stendi kwaajili ya safari na ukakuta bus limesha ondoka kisha ukatumia bodaboda kufukuzia bus embu tueleze ilikuaje na gharama za kulifukuza zilikua kiasi gani.

Mimi niliachwa na bus enzi zile stendi ipo Ubungo nilikuwa naelekea Dodoma na bus ya Al-Saedy tiketi iliandikwa safari inaanza saa 4:00 asubuhi nafika pale majira ya saa 3:50 asubuhi naambiwa gari imeshaondoka muda si mrefu nilivurugwa ikabidi nichukue namba za konda akaniambia hawako mbali nichukue bodaboda wao wataenda mdogomdogo, chap nikavuta bodaboda nikaanza kuifukuzia nilikuja kuipata kibaha bodaboda ananiambia gharama yake nilibaki hoi ni bora ningeongezea kidogo nipande bus nyingine ikawa mzozo ila konda akalipa kwa kumuahidi nikifika Dodoma nitamlipa maana pale sikuwa na kitu, nilipofika Dodoma nikamkimbia sikumlipa kitu.

Je wewe ilishawahi kukutokea tueleze ilivyokua ...

Hapana, siwezi kuachwa na bus.
 
Niko naelekea kigoma kabla ya stand ya chalinze km kama 5 hiv kuna vx iligongana na lori la mchanga sasa ikasababisha foleni
Nikashuka ku****a bwana nakuja kurud bus ishaondoka aiseee boda chap mpaka stand ya chalinze naikuta bus ndo inatoka boda anataka 5000 na mm nina 10 hana chench nilihahaaa aisee jirani yangu ndo akaniazima 5000
Betrice popote ulipo kunywa peps kwa mara nyingne ulinisave sana siku hiyo
inawezekana alikua na chenji ila aliiona fursa ya kumuachia pesa yote
 
Mtu akiachwa na gari huwa anakuwa na wenge ila alishalipata bus baada ya kulifukuza ndo anakumbuka mambo ya gharama alizotumia.

Ni sawa na wengine, unakuta kasahau kubeba mswako labda yupo jirani na nyumbani anaichukua boda kufuata mswaki wa buku
upo sahihi wenge ndio linalo sumbua
 
wazo lakununua tiketi mpya huwa halipo sababu unakua umevurugwa alfu wale maagent wanakushawishi uchukue bodaboda kwa kigezo cha bus halijafika mbali
Enzi hizo tulikuwa tunafukuzia kwa taksi za kukodi. Wakati huo mabasi yanaondokea Kisutu na yalikuwa machache sana. Uzuri ni kwamba hakukuwa na foleni kama sasa hivyo taksi ilikuwa inakata barabara kwa speed ya ajabu. Bodaboda mimi nimewahi kuitumia ''kufukuzia'' ndege DIA. Enzi hizo wanajenga ile junction ya Buguruni. Magari hayasogei na ndege inakaribia kuondoka.
 
Mkuu, Ubungo kuna mabasi yalikuwa yanaruhusiwa kuondoka saa 10:00 asubuhi? Nakumbuka mabasi yalianza safari saa 12:00 asubuhi.
Bila shaka wewe si msafiri wa mara kwa mara, nenda stendi anytime unapata gari.
 
Ni juzi tu hapo 2017 nilikua naenda Kahama tokea Dsm.
Nilikua sijawahi kwenda, katika uliza uliza magari nikashauriwa nipande kisbo safari.

Safari ilikua inaanza saa 12 asubuhi, abiria ufike saa 11 na nusu. Na vifoleni hivi vya tabata kufika pale ni 12 na madakika na ndinga ishang'oa.

Uzuri kisbo ilikua na ndinga nyingi zinazopanda huko, nikadanda ndinga ya tabora nikitegemea kuikuta hiyo gari yangu moro na hapo mfukoni nina buku 5 tu dadeki.

Nimefika moro nikashushwa niisubiri ile gari pale, Mungu alikua upande wangu maana niliiona wakati inaingia pale msavu maana wale jamaa (wa gari yangu) hawakua na taarifa na mimi wala hawakujua kama wameacha abiria.
 
Back
Top Bottom