Habari ya uzima wana JF moja kwa moja niingie ktk mada bila ya kupoteza muda Je..? umewahi kuachwa na bus au kuchelewa kufika stendi kwaajili ya safari na ukakuta bus limesha ondoka kisha ukatumia bodaboda kufukuzia bus embu tueleze ilikuaje na gharama za kulifukuza zilikua kiasi gani.
Mimi niliachwa na bus enzi zile stendi ipo ubungo nilikua naelekea dodoma na bus ya Al-Saedy tiketi iliandikwa safari inaanza saa 10:00 asubuhi nafika pale majira ya saa 3:50 asubuhi naambiwa gari imeshaondoka muda si mrefu nilivurugwa ikabidi nichukue namba za konda akaniambia hawako mbali nichukue bodaboda wao wataenda mdogomdogo, chap nikavuta bodaboda nikaanza kuifukuzia nilikuja kuipata kibaha bodaboda ananiambia gharama yake nilibaki hoi ni bora ningeongezea kidogo nipande bus nyengine ikawa mzozo ila konda akalipa kwa kumuahidi nikifika dodoma nitamlipa maana pale sikua na kitu, nilipofika dodoma nikamkimbia sikumlipa kitu.
Je wewe ilishawahi kukutokea tueleze ilivyokua ...
Mimi nimeexperience kinyume
Nishawahi kukata tiketi gari la kuelekea Dodoma (nadhani ilikuwa alsaedy au super champion)
Nimekata tiketi saa 2 na walisema litaondoka saa 2 ½, kibaya naingia ndani nakuta abiria kama watano tu nikasema leo nimeyakanyaga
Nimejaribu kwenda Kwa konda akawa anakazia abiria wapo wengi tu wametoka nje na akanionyesha kitab Chao Cha tiketi kweli kilikuwa kinakaribia kujaa
Tukikaa kwenye gari kuanzia saa 2 hadi saa 5, kibaya zaidi gari lilikuwa lipo limewashwa likazimwa na wakalipaki pembeni kabisa kuonesha hakuna ratiba ya kuondoka
Kuna jamaa mmoja, akawafuata makonda akawaka sana na akawaambia wamrudishie nauli yake huku wengine tupo kimya tu tunasapoti kimoyomoyo
Jamaa wakataka kumrudishia Hela yake akagoma akasema yeye atakuwa wa mwisho kupewa, yaani Hela Kila mtu apewe nauli yake ili akapande gari lingine
Jamaa wakapagawa wakaamua kuanza safari.
NILICHOJIFUNZA
1. Hutakiwi kuwasikiliza maagent vishoka maana waliniongopea gari kama kimbinyiko, shabiby nk zimejaa kumbe uongo
2. Sikuwahi kukata tiketi mpaka niingie ndani ya gari nijirishishe kuwa lina abiria wa kutosha
3. Kusafiri na kampuni za uhakika sio magari mabovumabovu /ya zamani