Natoka zangu Mbulu kwenda Babati, usafiri ni land cruiser, tumefika maeneo ya Magugu kuna abiria akawa anashuka, me nimekaa siti ya mbele pembeni ya dereva, kwa jinsi gari ilivyojaa na yule abiria anayeshuka kakaa nyuma kabisa, nikasema na mimi nishuke chap ninunue maji ya kunywa. Nikakikimbia duka la karibu chapchap nikapata Maji. Dah! Ile kurudi kwenye gari naiona cruiser ileee ishaishia. Kwenye gari nimeacha begi langu lina vitu vya muhimu Sana. Magugu na Babati sio mbali, zipo bajaji zinaenda. Nikachukua bajaji nikitegemea nitaikuta tu ile cruiser stand nichukue vitu vyangu. Hao, tukaanza safari na bajaji kufika maeneo ya daraja la Kiongozi, naiona ile cruiser kwa mbali imepaki kando ya barabara na abiria wameshuka. Nikaona baadhi yao wanaisimamisha ile bajaji ili kutaka kupanda.Nikashangaa!! Kumbe cruiser imezingua asee, naona boneti iko juu, gari imechemka haiwezi endelea. Haha! Nikasema dah! Kumbe ni Mungu kaniepusha na ile gari, nikamwomba dereva bajaji nichukue begi langu pale, kisha haooo mpaka Babati. Abiria wa ile cruiser walikosa nafasi sababu bajaji nyingi zinazopita hapo zinakua zimeshajaza kutokea Magugu.