Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Hata kama basi linaondoka saa 7 usiku siwezi chelewa, ni mipango tu, kuacha mda wa kutosha, na nusu saa ya zarura, ni discipline tu na kuwa in control.
Hii nidhamu sisi tulijengewa na mama yetu. Gari ya saa 12 asubuhi mama anakuamsha saa 10 kasoro. Unashangaa kituoni umefika saa 11:30

Na ukishafika hakuna kuzunguka ni ndani ya gari.
 
Bladi fakeni 2016, Nikiwazangu Karagwe chuma ya city boy iliniacha, nafika stendi naambiwa chuma imesepa siyo muda.... Boda akaniambia siyo kesi hebu tuanze ligi. Kwakua nilikua nawahahi seminar Dom nikakubali ushauri wa bwana bodaboda. Boda akawasha pila tukaanza kushuka kuitafuta kiyanga. Sasa kati ya kiyanga na Kayanga Kuna mteremko mkali na Kona kama upo Nepal au Jimbo la Kashmir. Bodo yupo speed anazifyeka zile Kona, Sasa sijui boda alibonyezq kitu gani nikashangaa tunaseleleka kuelekea kwenye mtaro. Tulitoka salama na boda wangu ila pikipiki ilikua haitamanuniki.
 
Kufukuzia gari kwa boda ukiachwa ni michezo ya hatari sana siwezi ijaribu Ajali ni nyingi sana
 
Usithubutu kuifuata na boda boda SAULI au Golden deer.. utagombana na dereva wa boda boda na hautasafiri maana hautazipata.
 
Enzi za kina Matema Beach, Safina, Tawakal ukiachwa dakika tano achana nayo. Basi zilikuwa zinsondoka Dar saa 12 asubuhi saa nane mchana ziko Mbeya na saa 10 jioni ziko Kyela.
 
Aiseee umeongelea kitu ambacho hata mimi ilikua bdo kdogo sana niachwe na bus hyo siku..,
Ilikua ni haohao jamaa wa HAPPY NATION bus nlilokata online Plate number yake ni tofauti na ambalo lilikua linasafiri kwny mda husika npo zangu Ofisini kwao pale me kazi yangu ilikua ni kucheza na plate number tu maana nlikua na mishemishe kdogo sasa nlipotoka nkarudi mda husika wa kuondoka bado basi husika siioni nkatulia zangu tu kule ofisini nkiwa najipa moyo bus halijafka kumbe waliokuepo pale walitangaziwa bus husika litalokua linasafiri na mimi sikuepo mda huo,,,
Ila anyway wacha niishie hapo ila nnachokumbuka ile siku niliwasha MOTO huo hawatoweza kunisahau..
 
Hii nidhamu sisi tulijengewa na mama yetu. Gari ya saa 12 asubuhi mama anakuamsha saa 10 kasoro. Unashangaa kituoni umefika saa 11:30

Na ukishafika hakuna kuzunguka ni ndani ya gari.
Mimi huwa ninawahi sana stand ila suala la kuzungukazunguka na kutotulia ndani ya basi limewahi kunifanya nikutane na misala mingi sana ya kutaka kuachwa na bus japo sijawahi achwa..
 
Vipi bus mliinyaka..?🤣
 
Uwa sielewi ni kwanini wanafanya hivyo kwa maana ya plate number inayowekwa mtandaoni kuwa tofauti na gari linaloondoka. Binafsi nilikwazika sana na nligharimika sana sema nkasema wacha nilichukulie kama funzo.
Hakuna siku ntapanda tena gari zao wapuuzi wale.
 
Hii nidhamu sisi tulijengewa na mama yetu. Gari ya saa 12 asubuhi mama anakuamsha saa 10 kasoro. Unashangaa kituoni umefika saa 11:30

Na ukishafika hakuna kuzunguka ni ndani ya gari.

Shukrani nyingi na pongezi kwa Mama.
 
Niliachwa na happnation Bukoba nikachukua boda Hadi Kimondo wapiiii!!!
Hawa maagent huwa wanauza abiria Mimi waliniambia ndo limetoka Sasa hivi basi chukua boda fast. Aisee boda alitembea speed zaidi ya 140 wapiiii?
Basi likishatoka stand dakika 5 ni nyingi kulikamata
 
pole sana
 
Pole sana kijana
 
Ukiambiwa ufike stand saa 11, ukagika saa 11 kasoro na basi halipo usihangaike kulifukuza waambie tu wameyatimba maana umewahi na wao wameleta usela. Kuna Mabasi wanakwambia fika stand saa 9, saa 9 na nusu tunaondoka. Ukifika saa 8 na dakika 50 unaambiwa washasepa wakimbize.
 
Vipi speed ya boda ilikuaje mkuu
 
Nimewahi achwa basi la Capricorn la Musoma Tarime, kutokea stand ya Magufuli pale aisee bodaboda alinipeleka hadi maili moja lakini wapi sikulikamata na alinitoza sh 20,000/=nikaenda siku inayofuata
Mimi ilinitokea mwaka juzi tunaenda msibani nmekata siti za kutosha 480000, fresta ikatuacha. Shida tulikuwa na watoro so kuifukuza na boda tusingeweza. Fresta nyingine ikatubeba tukaja ikuta moro, konda wa fresta iliyotuacha alimaindi nadhan alikuwa ashaona atauza siti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…