Hiki kitu nlikitambua baada ya kuwa nimefanya makosa ila nilijifunza. Mwaka jana mwishoni nilikata tiketi mtandaoni ya kwenda Mwanza kwa bus la kampuni ya Happy Nation, tiketi ilionesha bus linatoka pale Shekilango saa tisa kamili.
Nimefika Shekilango saa tisa kasoro nikiwa na bodaboda naambiwa bus limetoka hapa sasa hivi, nikaanza kulikimbiza lakini silipati, nikaenda mpaka Mbezi silioni maana nilikuwa natizama plate number za mabus ya kampuni hiyo ninayopishana nayo.
Kufika Mbezi naambiwa limeondoka nikaanza kulifukuza tena ila nikawa nashangaa mbona magari ninayoyapita hayana hii plate number?
Nikaja kugundua baadae kuwa plate number ya kwenye tiketi haikuwa plate number ya basi liliondoka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],nikapanda bus lingine la kampuni hiyo mpaka Moro ndio nikakutana na bus la Mwanza, ila mpaka napata hilo bus lao jingine lililonifikisha Moro nilikuwa nimeshatoboka kinoma.
Na tangu hiyo siku nimeagana na safari kwa kutumia kampuni ya HAPPY NATION hata bure.