itakuwa kweli maana kuna kasichana fulani miaka 2 iliyopita alikuja field ofisini kwetu kutoka chuo flani hivi, alikuwa ananiangalia sana kwa jicho la husda kila tulipokutana na alikuwa anapenda sana kuongea na mimi yaani kila ninachoongea alikuwa anafurahia sana
nikawa nachukulia poa tu kama ilivyo kwa college girls wengine wanaojiachia kwa kuvizia kupiga vibomu muda wa Lunch na lift, lakini huyu binti hakuwahi kunipiga kurungu chochote mpaka pale yeye mwenyewe aliponichana live kwamba ananipenda coz nimefanana na baba yake kuanzia sura,umbo mpaka kuongea....hahahahaah kilichoendelea hakina haja ya kuhadithia
TURUDI KWENYE MADA:
Hii dhana inaukweli flani hivi sababu kabla ya kuingia kwenye ndoa kuna stage za kupitia kama vile uboyfriend na ugirlfriend,uchumba na ndoa kwa ujumla sasa katika stage zote hizo kuna jambo au kitu ambacho kimekusukuma kufikia hatua zote hizo na kitu chenyewe kinaweza kuwa hicho unachosema kuhusu kufanana kwa mmoja wa wazazi ingawa inakuwa ni vigumu kuangalia tabia esp mnapofikia kwenye hatua flani maana mara nyingi hisia na mahaba ndio zinakuwa zimehusishwa zaidi kuliko kitu kingine (soma kitabu- The Case Against Divorce)
my take;kila mtu anapenda kile chenye faida na manufaa so hata mimi napenda kupata mke mvumilivu kama mama yangu...period