Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!.

Ukiwa Rais wa Toyota huruhusiwi kutembelea idara yoyote na kutoa ushauri jins ya kuboresha utendaji wao wa kazi?

Mnaoshangaa hamuamin kuwa Rais anaweza kuwa na nawazo ya kuboresha
 

Ni gharama kuonyeaha Bunge lakini si Gharama.kuonyeaha utendaji wa kushtukiza na kurudia tena na tena.Hilo ulijue.Na pia siyo maruku kwa wabunge wa CCM kuonyeshwa live kwenye mikutano yabhadhara lakini ni marufuku kwa upinzani kufanya mikutano maana kuna hatari ya kuzuka vita.Ni Bongo tu
 
Huwezi kujenga mifumo, systems sijui wakati una watu MAZUZU, WEZI, WAONGO, WASIO NA MAADILI. Hata akisema ajenge mifumo he will prove failure coz wa Tanzania wengi tukiachwa tuongozwe na hiyo mifumo hatuwezi kujiongoza.

Nitatoa mfano, huko ulaya na nchi zilizoendelea, ukitumia metro (underground trains), kuna maeneo wala.watu hawajawekewa vizuizi wakati wa kuingia. Una scan kadi na kuingia, hakuna askari wala kizuizi. Na watu wanatii sheria, wanascan, wanapita na huwezi kuona mtu anapita bila kufuata utaratibu. Now, do it in Tanzania, utanipa matokeo yake. Hii nchi na watu wake wanebeba aina fulani ya laana. Tuombe Mungu JPM atengeneze mfumo, sisi ndio tutakua wa kwanza kulalamika. Huwezi kuweka mifumo kwa watu kama sisi, tumesoma lakini hatujaelimika hata kidogo, tunataka vitu vizuri lakini hatuwezi kuvitunza, hatuna uzalendo wala maadili. Let him do what he can do lakini nimeshaona shida ipo kwa wananchi.
 

Hoja kama hizi haziwezi kukosa. Tatizo ni nini kwa Rais kuhoji mtendaji hata yule wa chini kabisa? Wewe unataka bureaucratic system ambapo Rais analetewa taarifa za kupikwa na kuchakachua; mara ataambiwa mashine zote zinafanya kazi nk nk? Hapo ametoa mfano hataki kudanganywa siku nyingine wakileta taarifa zitakuwa taarifa za uhakika.

Katika uzembe ufisadi na rushwa iliyokuwa inaendelea nchini lazima kazi nzuri ya Mheshimiwa JPM ya kutumbua majipu ipate wakosoaji hasa wale wanaonyang'anywa donge mdomoni! Hata huyo Lissu na wapinzani kwa ujumla wanaanza kuwa kichekekesho kwa kuunga mkono "status quo".

Yaani sasa hivi wapinzani kwa sasa hoja zao utafikiri ni CCM ya 2015!! Kweli wapinzani hawaaminiki tena nimekubali.
 
Kwa hiyo ni afadhali ukose huduma hospitalini (mfano) kwa sababu kuna mkubwa mmoja ameamua kuuza dawa kwa kuwa haogopi?
Ndio!, nidhamu ya woga Ni kutimiza wajibu wako pale Tu mabosi wako wanapokuwa eneo lako la kazi, wakiondoka usanii unaendelea, sasa faida yake nin nini?, bora kutokuwa Na nidhamu kabisa ili tunapofanya maamuzi tujuwe upana wa wigo wetu kwa mfano ulioutoa Kuna faida gani kun'golewa jino Na ganzi viongozi wakubwa wakiwepo Na wasipokuwepo ganzi inatumika kwa maslahi ya akina fulani Tu,
 
Ukiwa mpinzani haimaanishi kuwa unakuwa mjinga au unakosa ufahamu. Au wapinzani mmelogwa na aliyewaloga alishakufa? Hivi itakapofika mwaka wa 3 wa utawala wa JPM baada ya kuimalisha hiyo mnayoita nidhamu ya woga akaanza kujenga mifumo dhabiti mnayoililia nyie mtabaki na ajenda ipi? Nina uhakika kuwa, uwezi kujenga kitu bila kuwa na pa kuaanzia. Miaka miwili ya kwanza au hata mitano kabisa ni miaka ya vita ya kufyeka, kuchoma nyasi/misitu, kulima n.k. miaka ya baada ya hapo, itakuwa ya kujenga hiyo mifumo. Hiyo ndiyo TZ tuitakayo....siyo TZ iliyojengwa bila msingi sahihi na imara.
 
Kama una hisi unaogopa acha kazi.

Hivi kama domestic arrivals hawapiti kwenye scanner ziliwekwa za nini in first place?
 
Kuna uwendawazimu wa baadhi ya watanzania kushawishi tumuamini mtu mmoja katikati ya uendelevu wa mfumo mbovu kwa sababu tu anasema:- "Nina nia ya dhati...., mniombee!".
 
We mpuuzi tulia dawa ikuingie .

Tunatambua unatetea majizi wenzako
 

Kwani kapoteza nini kufanya hiyo wondering management, hapo hoja ya Lissu haina nguvu tena basi yeye mwenyewe kama Rais kuongea na junior staff inampa uwanja mpana wa kujua matatizo from the grass root kuliko kuongea na watu wa juu wanaishia kukupa report za kupika za uongo ambazo hazija tusaidia kwa miaka hamsini sasa.
 
Pasco Ukibeza ni mtazamo wako nikuombe Uangalie ktk jicho la tatu.Ziara ya Mh.Raisi imefundisha mambo makuu mosi Tabia ya kusema Ukweli tuache tabia ya Uongo uongo hii imekuwa ni Hulka miongoni mwetu Sote Tujirekebishe.Kudaganya hakusaidii japo katika kuficha baadhi ya mambo ili Watu waendelee kufanya yao hapa naamanisha kupiga Dili.Umaskini wetu na Njaa zetu zinatufikisha hapo Na kuacha kabisa Nidhamu Kazini,Maadili,Uwajibikaji na Ufutiliaji ktk Sekta zote kuanzia Wakuu wa Idara,Wakurugenzi,Makamishna,Mameneja hadi Cheo cha chini kabisa.Tuache haya ya Kusema Uongo na siyo Pale tulivyoona hata kwenye Maofisi Ofisa anamwambia Njoo kesho ili hali anajua na hata hiyo kesho akija Hatapewa Majibu au kukuta kazi yake imeshughulikiwa hilo Mosi.
La pili Uwajibikaji katika Nyanja zote Idara na Vitengo.
Tatu Usalama na Tahadhari Tuondokane na BUSINESS AS USUAL.Kwa walio wengi Wataona ni KERO na WATASEMA SANA NA HUMU JF WATAANDIKA SANA .Niseme TUJIFUNZE KUTOKA KWA MH.RAISI. Nimalizie NJAA NI MSHAURI MBAYA
 
Bwana pasco naheshimu sana mada zako.Lakini kwa jana naona Mheshimiwa alikuwa sawa kabisa.kumbuka nyara kukamatiwa Uswiss toka JKNIA, Kwa hiyo kila kitu kinawekana ktk nchi hii.Nafikiri bila kujua sisi wananchi nchi ilibinafusishwa. Tena bila tenda.
 
hakuna nidhamu ya woga kwenye private sector.kuna nidhamu
Mkuu, ndiyo maana yangu. Huyo mdudu anaitwa nidhamu ya uoga sijapata maana yake halisi. Nidhamu ni nidhamu tu. Private Sector mtu anajua akiharibu anatimuliwa
 
Naona mkuu umekaa sana marekani Kiswahili shida. Nidhamu ya woga maana yake ni nidhamu muda mfupi kwa kumuogopa mtu au mfumo kwa wakati fulani. Mtu au mfumo ukiondoka muhusika anarudi kwenye utovu wa nidhamu ambao ni jadi yake. Sasa umechambua maneno in your favor kwa malengo tunayoyajua. Kukiwa na mfumo mzuri kila mtu anakuwa na nidhamu kwa vile asiye na nidhamu atafukuzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…