Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!.

Kuna matatizo ya nidhamu. Mtu hawezi kupelekwa Mahakamani mpaka afanye kosa kubwa. Lakini siyo hivyo jeshini. Jeshini mtuakifafanya kosa dogo anawekwa ndani;siyo miaka mitatu kwa kufanya kosa dogo,hapana,anawekwa ndani saa 24,saa 48. Mtu wa heshima,ukimfunga siku chache au wiki chache,anakuelewa,hafanyi kosa tena. Halafu,most important,ukimweka mtu mahabusu wiki moja au mbili,adhabu yake ni restrictition of movement for two weeks,nothing more. Yakitokea matatizo mengine huko mahabusu,incaceration inakuwa siyo halali. Wanajeshi wanajua hilo. Akiwekwa mahabusu,anajua maana yake ni kupumzika tu pale siku chache. Kwa sababuhawa watu wanatembea na silaha. Huwezi kumweka mahabusu siku mbili,halafu ukamletea uhuni au udhalimu. Lakini uraiani,its different. Kwenda mahabusu wiki moja tu inaweza kuwa hatari.Mambo kama hayo yakitokea,ukiukaji wa haki za binadamu,watu hawataiogopa serikali,no matter how fierce it is.
 
Hiyo kauli yako ya "Maisha bila sukari yanawezekana" kama ingekuwa ni ya kweli Serikali ingekaa kimya na kuacha Watanzania tuendelee kulanguliwa kwa bei ya shilingi 4,000 kwa kilo au hata zaidi, lakini hiyo kauli yako si kweli ndiyo sababu Serikali inahaha kumaliza hili tatizo lililosababishwa na Magufuli na sera zake za kukurupuka.

Angeweza kabisa kuwaita Wataalam toka Wizara ya Viwanda na biashara ili wampe takwimu za uzalishaji wa sukari nchini kwa siku, wiki na mwezi na sukari inayoingia nchini toka nchi za nje kwa wiki na mwezi. Kisha kukaa chini na management ya viwanda vya sukari ili kutathmini kama vinaweza kuongeza production capacity ili kufidia sukari toka nje. Si ajabu wangemwambia hawana uwezo huo kwa sababu mbali mbali au wangeweza kuongeza uzalishaji wao kwa kiasi fulani na kisha Serikali ingeweza kufanya maamuzi yake nini kifanyike bila kusababisha upungufu wa sukari nchini. Ila huyu Magufuli kwa kutaka sifa zisizohusu kitu na cheap popularity akakurupuka na sera zake za kukurupuka.

Acha ubishi wa kitoto, kama wewe unaweza kunywa chai/uji kwa kuweka chumvi basi Watanzania wengi hawawezi na pia sukari inatumika katika mahitaji mbali mbali ya kila siku na mabiashara na Watanzania mbali mbali nchini. Maisha bila sukari hayawezekani ndiyo sababu Serikali inahaha kwa kuogopa kupoteza credibility yake.

Sure thing. Hakuna haja ya bunge kujadili sukari. Ingekuwa vema km wabunge wangeshauri serikali iongeze fedha za research kuhusu ugonjwa wa kisukari. Tusitegemee tafiti za nje tu.

Maisha bila sukari yanawezekana.
 
Tatizo hana exposure lakin bado anataka kufundisha watu cha kufanya.Na hizo ziara hazina manufaa Zaidi ya kujitafutia umaarufu kwa watu,sasa sasahivi magazeti hayahangaiki nae tena kumsifia "anavyoshtukiza",wameamua kumfanyia bwana mkubwa kipindi maalumu ili aonekane "anavyoshtukiza!".I think this is lame...
 
Kwahiyo miaka mitano ataimaliza kwa "kushtukiza"?Maana watanzania ni vichwa maji,ukishapita wanajua hurudi tena soon wanaendelea na mambo yao...Na "atashtukiza" nchi nzima au ni Dar tu kwenye media?Tunachohitaji Tanzania ni strong institution zenye kujiendesha na kufuata sheria na taratibu zinazotakiwa,sio kushtukizana...akiondoka huyo mtu wa kushtukiza unajua watu watarudi kwa kasi namna gani katika mambo yao zamani na nini kitatokea?Total distruction ya kilichojengwa kwa kushtukiza kwa miaka kumi...
 
Taratibu mtanyooka tu...mkwere alikuwa anawaonea aibu aibu sana. Sasa hizi ni zama za ngosha.
 
Nidhamu ya woga inatakiwa sasa itajenga nidhamu kamili mbeleni. Tulijisahau sana! Zamani Mwalimu alikuwa na hizo kwa sana lakini matokeo yake nidhamu ilijengeka. Sikiliza wimbo wa ' Nidhamu kazini ni msingi wa mafanikio mema kazini viongozi na wafanyakazi lazima wote tuwe na nidhamu.....migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu" ona walivyojichanganya maelezo ??!! Hii style inatufaa sana
 
hao wafanyakazi walijua scanner ni mbovu walisema kwa nani kama ni mbovu…!?

Kwanini wasifanye kazi zao kama mikataba yao inavyosema.

Hakuna ushamba hapo hakuna tatizo la kabila wala la ushauri.
watanzania tunatakiwa tubadilishe aina yetu ya ufanyaji kazi, sio mpaka tupigiwe kelele au tulazimishwe.
ni watu wazima wabaofanya kazi lakini bado wapigiwe kelele.
hili linalofanyika liendelee mpaka tunyooke.
Wala haliitaji mwenye akili aseme magufuli anakosea ndio tuamini anakosea.
kila mtu ana akili na anajua mazuri na mabaya.. kwaio tuchague kufanya mazuri kwa maendeleo ya taifa.
 
Mimi niliona clip yote ya yaliyojiri JKN airport. Rais alikuwa anauliza maswali kwa upole kabisa. Wahusika walipoanza kuficha ukweli na kujichanganya hapo ndipo Rais alipoanza kuja juu na kueleza athari za kuwa na vitendea kazi muhimu visivyofanya kazi. Rais si mjinga wa kukurupuka bila kujua nini kinaendelea. In dhahiri kabisa alikuwa na data zote za ubovu wa mashine za kukagua mizigo pale airport. Alichokifanya sio kuagiza watu wafuatilie na kumpa taarifa akatumia style yake akaenda mwenyewe kutafuta ukweli. Ifike mahali watendaji serilkalini na wananchi kwa ujunma waielewe style ya utendaji ya Rais wa awamu ya tano na waikubali. Ni dhahiri anayoyafanya in mageni kwa baadhi ya wananchi ambao hawakushudia utendaji kazi wa Rais wa awamu ya kwanza Mwl. Nyerere na baadhi ya viongozi wa awamu ile hususan waziri mkuu Sokoine ambao walikuwa hawamwachii mtendaji yeyote had I ithibitike kile alichotakiwa afanye kimefanyika!

Asilimia kubwa ya mapungufu ya vitendeakazi serikalini na taasisi zake yanatokana na uzembe na hujuma. Mashine zisizo na viwango na hata zilizo mbovu hununuliwa na baada ya muda mfupi huharibika. Ni wazi ktk hali ya nchi yetu ilipofikia inahitaji Rais mwenye style ya Magufuli ili watu waogope kidogo na kujirekebisha.
 
The reign of terror imeingia CCM, wameisoma number.

Paskali
 
Hahahahahahaha mie sijui kuremba ukiandika upuuzi kwanini nifiche? Lini uliwahi kukemea matusi ya nguoni ya dikteta na kudhalilisha wake kwa waume? Mchumia tumbo ni lazima aanikwe hadharani hakuna KUREMBA. Au matusi ya dikteta hukuwahi kuyasikia?
Karibu pande hizi.
Vipi na hapa nasifu?.
P
 
“Heshima iliyokuzwa ni ya woga
heshima inayotakiwa iwe ya moyoni.
---
Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Mkuu Mmawia , asante kwa hoja hii ya nidhamu ya woga.

Kuna watu humu hili la nidhamu ya woga ndio wamelijua Leo baada ya kusemwa na Mama Samia.

If you have time, angalia tarehe ya bandiko hili na hoja yake muone sisi wengine tulilisema lini.


Kwa wavivu wa kufollow links, hapo niliuliza
Hatukuishia Kwa Number 1 tuu,
ila pia niliendesha somo humu namna ya kutofautisha kuongea Kwa ukali na kufoka foka

hata number 3, yule Kiranja Mkuu wa viranja pia tuliwahi kumshauri

Hata baadhi ya Mawaziri walipokosa utu, akina sisi tuliwasema...

Na hatukuishia viongozi wakuu na Mawaziri pekee, hata ma RC tuliwamulika

Huyu pia

Hivyo hili la nidhamu ya woga lilikuwepo sana kwa JPM, lakini twende nyuma na kurudi mbele,
Kwa hali hii, mfano Mama naye ni binadamu, anaweza kukosea, jee akikosea kibinaadamu, kuna kiongozi yoyote ndani ya serikali anaweza kum correct, au kuna any main stream media that would dare criticize or correct her, or the epitome of cowardice inaendelea?!.

Nasisitiza Mama naye she is a human being, anahitaji kusapotiwa, kusaidiwa, kushauriwa, na akikosea akosolewe kistaarabu kwa lugha ya heshima na staha huku akishauriwa the right thing to do, ushauri wangu wa kwanza, ni Tanzania tunaweza kabisa kusonga mbele na kufanya mazuri bila kunyoosheana vidole and calling names kama "Simba wa Yuda".
Nashauri tufanye tuu mambo tofauti bila kumtaja taja Kwa ubaya!
Aachwe Apumzike!.

Jumapili Njema

Paskali.
 
Prophetic!
 
Kwa mfumo uliopo hayupo mwenye ubavu na jeuri ya kumkosoa kiongozi mkuu, hata Bunge haliwezi. Hata kauli ya mzee Kinana kwamba Chama hakipokei maagizo kutoka serikalini sio kweli. Mamlaka ya Rais na Mwenyekiti wa Chama sio mchezo. Nani ataweza kumfunga paka kengele na kwa njia zipi. Hapo ndipo dhana ya Katiba inapoonekana. Lakini hilo ni kaa la moto. Kwa hali hiyo 'simba wa yuda' hataepukika, ataendelea 'kuwatesa' wabongo. Ni zimwi lililotoka tayari kwenye chupa. Nani atalishawishi kurejea ndani ya chupa. Muulizeni Rais Mustaafu Kikwete na Mzee Warioba na rasimu ya katiba.
 
Lile bandiko lako la 2014 ulionesha kukosa amani juu ya uteuzi wake hata hapo ulionesha kabisa wanaommudu ndio wamshauri wachache walijua huyu mtu ni tatizo muda mrefu na nchi ilipata ajali kubwa ya kisiasa itachukua hata miaka 10 kufuta ombwe lake.
 
Mimi nilikuwa nakosoa na kushauri Swali kwa Viongozi/Wanasiasa Wetu: Kama Waliuona Udhalimu wa Awamu Iliyopita, na Wakaunyamazia, Is it Right Kuusema Sasa au Waendelee Kunyamaza?.
Pascal tumia akili kama msomi. Ulitaka waseme wauawe, wapotezwe, wabambikiwe kesi za uongo? Tumia akili!

Nipe thread yako yoyote uliyomkosoa Magufuli Kwa ukali
Utamkosoaje bosi wako kwa ukali?.
na kumpa ukweli kama Ben saanane alivyofanya kuhusu PhD ya mchongo.
Kuna wengi humu wanadhani kupotea kwa Ben Saanane ni shauri ya issue ya Ph.D ya mchongo!. Not necessarily!.
Ben alikuwa na computer program ya kufanya election tallying verification.
Baada ya matokeo ya uchaguzi, akafanya verification kutumia matokeo ya kura za urais, akajumlisha kura zote valid, plus invalid akapata total votes counted, kisha akatoa idadi ya waliojitokeza, akapata idadi ya kura fake zililiongezwa!. Lile bandiko sijui kama bado lipo humu!.
Hii documentary evidence by computing ni very dangerous then PhD ya mchongo!.
Nawe ulikaa kimya na uliposema ulisifia kupata uteuzi
Kati ya watu ambao hatukuwahi kukaa kimya, mimi ni mmoja wao.
Japo ni kweli baadae Blaza wangu ali changes for the better na mimi nikawa namsifu genuinely
P
 
Kuna watu wana utu hawawezi kushabikia uovu regardless kitakachowapata, najua wewe siyo miongoni mwao ndiyo maana maandiko yako mengi yanaegemea utawala dharimu.
Karibu kwenye baadhi ya mabandiko yangu kutetea udhalimu
P
 
Link for evidence by computing documentary please🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…