Wanabodi,
Naendelea na zile mada zangu za kusisitiza ukweli, ukiwa mkweli, ukweli utakuweka huru!. Hili ni swali, "Jee Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga?!. Jee, Kutasaidia?!.
Hiki nilichokishuhudia leo Eapoti jamani sio!. Tufike mahali watu wanaommudu, wamshauri, that is not the right way.
Leo nimemshuhudia ngosha pale eapoti anavyo waterorize wale maofisa pale!, tangu lini domestic arrival wanapita kwenye scanner?!, akashauri eti kwa nini nao wasizungukie pale kwenye scanner za depature ndipo waingie nchini!, kiukweli watu wenye akili zao, wanaanza kumuona huyu jamaa kama sio!, kiukweli ule ni terorising!, nitamshauri yule kaimu, vitu vingine viishie kwenye habari tuu na sio kuleta kipindi maalum wakidhani wanamjenga kumbe ndio wana mdhalilisha bure!, na jamaa anavyopenda masifa mbele ya kamera, kiukweli huu ushamba wa kabila langu sometimes unanchekesha!.
Nasisitiza naunga mkono kinachofanyika kuisafisha serikali yetu na madudu yaliyokithiri, the man is doing the right thing but in a wrong way!. Every human being needs dignity!. Pomoja na yote jamani, ka human dignity kawepo, na sio huu udhalilishaji mbele ya kamera halafu wanausha kipindi maalum!. Please wajemeni!.
Namshukuru sana Mzee wa kutumbua, leo kashtukiza lakini hakutumbua zile za papo kwa papo, labda sauti zetu zinaanza kusikika and to make sense, ila kufuatia nidhamu ya woga na kujikombakomba, mnaweza kushuhudia utumbuaji majipu ukifuatia ziaa hii pale Eapoti leo Jumamosi, au siku ya Jumatatu, kisa jamaa kapita pale kashuhudia na kadanyanywa!.
Tanzania inachohitaji sasa sio one man show, na movie za ze comedy!, tunahitaji kujenga mifumo, systems, kama hakuna scanner kwenye arrival zote duniani, bali kuna declaration forms, kila mzigo unaofikia arrival ulikuwa scanned kule ulikotoka na ukawa cleared ni majangili mataahira tuu ndio watauwa tembo wetu kisha wabebe pembe za ndovu kuingia nazo arrival! wakati mipaka yetu yote ni very porous!. Vitalu vyote vya uwindani vina private air strips midege inaingia na kutua na kujichukulia chochote na kuishia zao juu kwa juu, kwa kisingizio ni vitalu vya uwindaji!, ni kichaa tuu mwenye uwezo wa kutua porini kubeba nyara na kuja nazo arrival!.
Kila ndege kabla haijaingia Tanzania lazima ipate clearance toka TCAA, tuweke watu kwenye every private air stripe na kujenga mfumo toka TCAA kuwa hakuna ndege itakuwa cleared kutua kwenye shamba la bibi, bila bibi kutuma mjukuu ashuhudie hiyo ndege imeleta nini, na hakuna clearance kupaa hadi mjukuu athibitishe imebeba nini!.
Kiukweli hii ya leo kwangu ilikuwa Ze Comedy!, hatuwezi kwenda hivi jamani!.
Namalizia kwa lile swali la msingi, "Jee Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!".
Nawatakia Jumamosi Njema.
Pasco