The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,550
Kiongozi ni yule Anaeonyesha njia.Na anayogafanya Mh.Raisi si ziara za kushtukiza.Nionavyo ni ziara anayoifanya tayari taarifa anazo mezani Hivyo basi anapojitokeza huwa anatoa Funzo kwa wale wote wenye Tabia na Mienendo ya Kuhujumu Nchi.Na kama Raisi aliyechaguliwa na Wananchi wake ni lazima afanye hivyo hiyo ni sehemu ya utendaji wake.Mnaoandika ya kuwa hii sasa ni ONE MAN SHOW IMA COMEDY Bakieni vivyo hivyo.Mwisho wa siku Tutarudi kwenye Mstari na siyo Bussiness as Usual,whether u like it or not.Wewe umeajiriwa eti ofisi yako siyo sitting room yako Nyumbani ufanye unapojisikia ima kupiga Dili NJAA NI MSHAURI MBAYA
Mantonga;
Nimekuelewa na ni vyema sana kwamba, Rais anapofanya ziara hizi tayari anakuwa na taarifa mezani kwake......kwa hiyo anakuwa anajua anachokwenda kukiona na kukifanya.
However, maswali yangu kwako na wengine wenye mtazamo na kuamini kama wewe ni haya;
Hivi hizi "taarifa za kiintelejinsia", zinakuwa zinamfikia yeye tu Rais na kuwapiga chenga wasaidizi wake mfano ktk ishu ya JNIA ni waziri wa sekta ya ujenzi, mwasiliano na uchukuzi, katibu mkuu wa wizara na kisha shuka chini huku hadi kwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege, mkuu wa mkoa nk??
Je, ni kwamba hawaamini hawa wasaidizi wake kwamba labda na wenyewe ni walewale tu, au ni kwa nini hasa?
Je, kuna umuhimu wa kuweka wasaidizi hawa kweli iwapo kazi zote za serikali zaweza kufanywa na mtu mmoja tu?? Je, si ingekuwa bora sana kupunguza gharama kwa kulifanya hili liwe rasmi kikatiba - kwa maana tusiwe na mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa nk?
I thought, kama Rais ana mainfoma wake na wanamletea taarifa yeye moja kwa moja, naye pia aweza kuzishusha taarifa hizi moja kwa moja kwa wasaidizi wake....kwamba mahali flani kuna moja mbili tatu, waziri au katibu mkuu au RC au yeyote nenda immeaditely shughulikia na niletee taarifa by this time.....
Hiki ndicho ambacho kina Ben Saanane wanakisema kuwa ktk serikali hii hakuna "chain of accountability" kiasi ambacho utendaji wa serikali ni ule wa ONE MAN SHOW....na ikitokea huyu mtu akatoweka leo aidha kwa kifo (Mungu apishilie mbali) au vyovyote vile, maana yake mchezo unakuwa umeishia hapo, tunaanza upya tena kumtafuta magufuli mwingine!!