Jelavic
Senior Member
- Dec 28, 2016
- 183
- 381
Kwa wale tuliofatilia hotuba ya Mh. Rais mpaka mwisho katika hotuba ya ufunguzi wa Bunge na kusikiliza wageni mbali mbali wa Jumuiya za Kimataifa wadau wa maendeleo pamoja na wawakilishi na mabalozi wa mataifa mbalimbali, hatujaona ushiriki wa balozi wa Marekani, Ufaransa na Ubelgiji.
Mabalozi hawa ambao kwa pamoja walimsaidia na kumsindikiza Tundu Lissu mpaka uwanja wa ndege kwa UPAMOJA WAO HUO HUO hawajahudhuria ufunguzi wa bunge leo huku mabalozi wa nchi nyingi za Afrika wakihudhuria.
Najua sio lazima wahudhurie lakini kutokuhudhiria katika hiki kipindi kwa haya mazingira kunafikirisha.
Unadhani Tanzania imeanguka machoni mwa hizi nchi au wameogopa kuonekana pande mbilimbili leo wanaunga mkono kesho wanakosoa hivyo wameamua wabaki katikati au katika kimya kinene kuna msindo mkubwa?