Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kutudharau Walimu Shule za Msingi?

Je, huu ni mwendelezo wa Serikali kutudharau Walimu Shule za Msingi?

Nipo shuleni ofisini

Mbele yangu Kuna mzigo mkubwa wa daftari za stadi za kazi darasa la tano ninazopaswa kusahisha

Naangalia nje namuona mwalimu wa sekondari yuko bize kusimamia mtihani wa darasa la Saba

Najiuliza kwanini nisisimamie mwenyewe mwalimu wa shule ya msingi?

Je, Serikali imenichukia sana kiasi cha kuninyang'anya majukumu yangu?

Hili limenisikitisha sana nahisi nakosa furaha yangu ya kawaida hapa shuleni

Ni kawaida yangu asubuhi kuwatia moyo watahiniwa kuwa watulivu kisaikolojia ila ukweli leo nimejikuta nimeshindwa kufanya hivyo

Je, huu ni muendelezo wa serikali yetu kutudharau waalimu shule za msingi?
Ni Kwa sababu ya ujinga wenu
Wewe umefell kidato Cha nne alafu unataka heshima ya kazi gani
 
Akili ndogo ni akili ndogo tu

Kama nilikariri theory mbona wewe zilikushinda ukaishia kupata four failure?

Alafu unajua unabishana na mwalimu wako niliyekufundisha chuoni hadi ndo akapata hako ka cheti ka grade A?

Hahahhahhha
Wewe ungekuwa mwalimu usingesema four ni failure, wakati four ni pass
Bado unaniaminisha kuwa uwezo wako wa kutathmini Mambo ni mdogo
 
Akili ndogo ni akili ndogo tu

Kama nilikariri theory mbona wewe zilikushinda ukaishia kupata four failure?

Alafu unajua unabishana na mwalimu wako niliyekufundisha chuoni hadi ndo akapata hako ka cheti ka grade A?

Hahahhahhha
Mimi ni mtu mzima zaidi yako Msovero!
Bila Shaka nilikufundisha kkk
[emoji23][emoji23]
 
Mleta mada kama ni mwalimu serikali ilikuajiri kimakosa

Hiyo kitu inaitwa segregation of duties

Huwezi kufundisha wewe,utunge mtihani wewe, usimamie wewe na usahihishe wewe!

Walimu - TAMISEMI
NECTA - Wizara ya Elimu
 
Nipo shuleni ofisini

Mbele yangu Kuna mzigo mkubwa wa daftari za stadi za kazi darasa la tano ninazopaswa kusahisha

Naangalia nje namuona mwalimu wa sekondari yuko bize kusimamia mtihani wa darasa la Saba

Najiuliza kwanini nisisimamie mwenyewe mwalimu wa shule ya msingi?

Je, Serikali imenichukia sana kiasi cha kuninyang'anya majukumu yangu?

Hili limenisikitisha sana nahisi nakosa furaha yangu ya kawaida hapa shuleni

Ni kawaida yangu asubuhi kuwatia moyo watahiniwa kuwa watulivu kisaikolojia ila ukweli leo nimejikuta nimeshindwa kufanya hivyo

Je, huu ni muendelezo wa serikali yetu kutudharau waalimu shule za msingi?
Anayewafundisha na anayetunga mitihani huwa hatakiwi kuwasimamia wanafunzi. Suala la msingi ombeni mkasimamie mitihani ya form six husasani ni masomo ya arts
 
Haiwezekani mtambuliwe na na kuheshimiwa na wengine wakati ninyi wenyewe hamjitambui. Jipeni moyo yawezekana nanyi mtakwenda kusimamia mtihani wa kidato cha nne mwezi November.
Kama huu wa kwao NANGA zinapaa haya huo wa kidato Cha 4 si ndo MELI itapinduka kabisa mkuu
 
Mkuu mbona kama vile wewe sio mwalimu maana kipindi cha mitihani ya taifa ya darasa la 7 huwa hawaruhusu walimu wengine tifauti na headteacher kuwa maeneo ya shule
"A good liar must have a strong memory".
Kama namuona Charles Msonde akisoma maoni humu na kutabasamu, na akijisemea 'tumewanyoosha'.
 
Ni dharau tu. Mlifeli fom foo, nani awaheshimu?
Hakuna siku mwalimu wa msingi ataheshimika, ni aina ya watu wanaojituma sana ila output yao ndogo sana. Toka shule wale wanaojituma sana halafu wanafeli ndo huja kuwa walimu. Serikali imewadharau mnooooo. Na itaendelea kuwa hivyo. Sasa ili uepukane na hili, kajiendeleze kimasomo wakufanyie UGATUZI. Nje ya hapo wewe ni wa kudharaulika mpaka mwisho.
 
Na bado ile mbinu ya mwalimu anayesimamia ndani ya chumba kuwawezesha wanafunzi kwa kuwafafanulia maswali na kuashiria majibu inafanyiwa kazi.
Walimu wa Sec walikuwa wasimamizi wakuu tu, next time wataelekezwa vyumbani, na ikiwa kama hawatoshi, NECTA inaweza kuomba nguvu kutoka kada zingine, ikizingatiwa mtihani ni siku 2 tu.
 
Kwakua kusimamia Ni rahisi ila Kuna hitaji uaminifu mkubwa nashauri kipindi kingine waweke wasimamizi kutoka kada nyingine kabisaaa hata suma tu lakini wasivae sare
 
Tujikite kujadili chanzo ni nini kwa nini mitihani ivuje nadhani kuna vitu vikuu vitatu 3. Serilali, mwalimu na jamii au wazazi

Serekali haiko makini na Elimu yetu na taifa letu sera ya Elimu haiendani hata kidogo na maisha halisi ya watanzania haiwaandai watahiniwa kupamban na changamoto ya maisha tumekuwa tunawafundisha zaid wanafunzi Elimu ya kukariri na Elimu ya makaratasi wakati Elimu ya msingi inatakiwa iwe ya ujasiria mali kumwaandaa mtoto kimaisha kupambana na changamoto zote

Walimu ndio kiungo pekee maana mwalimu ndio mtu pekee anakaa mda mrefu na mwanafunzi kuliko mzazi pili mwalimu anatakiwa awe mwalimu kweli kama jina linavosadifu yani wapatikane wenye division 1 na 2 basi maana mwalimu ndio anazalisha kila sekta kuanzia afya mpaka raisi mwalimu ndio anastahili kuwa na maslahi makubwa kuliko mtumishi yoyote ili kazi ya walimu ipendwe lakin haipendwi na imekuwa na wengi waliofeli maisha ndio maana inadharaulika na haina maslahi

Jamii au wazazi isiishie kumpeleka shule tu mwanao nakudhani jukumlako limeisha iende sambamba na kufatilia mwanao anasoma nini na anauelewa gan au anapenda fani gani anza kuanda mazingira kwa anachopenda mwanao ili aje kuwa bora zaidi ya kile anachopenda jukumu la mzazi ni kubwa kuliko la mwalimu kwani wazazi au jamiii ndio watu wanaoweza kupaza sauti zaid kwa serikali

Hitimisho
Kuvuja kwa mitihani serikali ijitathimini mara mbili kuhusu sera ya Elimu imekuwa ya kukariri zaid ndio maana mwanafunzi anajibu a. b.c .... na maswali ya mwisho tu ndio anajibu tunze kumwandaa mtoto ajifunze kujieleza kwenye mtihani na sio kuchagua a. b. c na walimu pia tujikite zaid kuwaandaa wanafunzi kuelewa zaid na sio kufaulu au kukariri. Wazazi pia tufatilie maendeleo ya watoto wetu
 
Walimu wa msingi mlikuwa na kasumba ya kuiba mitihani na kuisovu kisha mnawapa wanafunzi vimemo vya majibu wanaingia navyo kwenye chumba cha mtihani.

Matokeo yake mkatuzalishia wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika kujiunga sekondari. Naona mwaka huu serikali imewabana sasa mmeanza kutoa milio ya kila aina. Hahahhahahah Tulieni dawa iwaingie
Tuliwasoma ,tukawajua tukaleta solusheni kumaliza huu ujinga wa kuzalisha vilazaa na mazazwa kwenye nchi hii😂😂yamebak yanalia😂
 
Kwakua kusimamia Ni rahisi ila Kuna hitaji uaminifu mkubwa nashauri kipindi kingine waweke wasimamizi kutoka kada nyingine kabisaaa hata suma tu lakini wasivae sare
Next time tunapeleka wataalamu wote nchi nzima,toka tra,nhc,nssf,bank tote,malekchara wa vyuo vyote nchi nzima,wanajeshhi,mama ntilie,walinzi wa kampuni zote nchi nzima,Hadi wa ubalozi zetu😂👆tutaelewana tu👆👊🏼🙏
 
Ni dharau tu. Mlifeli fom foo, nani awaheshimu?
Hakuna siku mwalimu wa msingi ataheshimika, ni aina ya watu wanaojituma sana ila output yao ndogo sana. Toka shule wale wanaojituma sana halafu wanafeli ndo huja kuwa walimu. Serikali imewadharau mnooooo. Na itaendelea kuwa hivyo. Sasa ili uepukane na hili, kajiendeleze kimasomo wakufanyie UGATUZI. Nje ya hapo wewe ni wa kudharaulika mpaka mwisho.
We mtu hata kuandika jina lake kamili hawezi,👆😂atakufundishia mtoto huyo?jiongeze😂hatuhitaji wajinga kwenda mfumo wetu wa elimu,👊🏼👆🙏
 
Back
Top Bottom