Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Hivi hawa wakurugenzi wanateuliwa kwa vigezo gani?ingekuwa vizuri nafasi hizi ziwe za kuapply na halafu watu wanashinda kwa kuwa interviewed.Hii ya kuteuliwa sometimes mihemuko inatumika kuwapata.

Ila pia huyo mama majibu yake yalikuwa yanataka kumdharirisha Mheshimiwa Raisi kwamba amemuuliza swali ambalo agepaswa kumuuliza DT wake.kwa hiyo ni swali too operational ,yaani siyo strategic kwa ngazi ya DED.hapo ndipo alipochemka Kitu chochote anachoulizwa raisi ni kikubwa kinatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wa juu kabisa .maana yeye ndiyo mwenye maona ya juu kuliko yoyote nchini.

Kwa hiyo hilo ni somo kwa viongozi wote usije ukategemea Swali la bosi wako lijibiwe na mtu aliyeko chini yako(subordinate).hiyi ni insubordination

Ni sawa na Pale kamati ya Bunge walipomuita Mwenyekiti wa board ya UDSM Kwenda dodoma kuhojiwa halafu badala yake Mkandala VC akaenda,kamati ilifanya sahihi kumfukuza.
 
Bwana Pascali. Swali aliloulizwa yule mama mara tatu mfululizo tena kwa kuonywa juu yabmajibu yake kwa Rais si swali baya kwa MKURUGENZI.

Haiwezekani mkurugenzi asijue ameletewa pesa kiasi gani kwa ajili ya BARABARA na akiba iliyopo ni kiasi gani.

Mkurugenzi anatakiwa afahamu akiba ya pesa zote alizonazo kila siku. Anatakiwa afahamu mapato na matumizi on daily basis.

Tatizo ni kuteua wakurugenzi ambao hawajawahi fanya kazi serikalini hivyo kutijua nini cha kufanya ofisini. Badala yake anataka mhasibu ndiye amsemee kwa bosi wake kwamba kuna pesa kiasi gani.

Isitoshe. Pesa za halmashauri hazipo kwenye mkundi mengi. Sana sana ni pesa ya barabara. Maji. Afya. Makusanyo ya ndani na miradi mingineyo ya hapa na pale.
Majibu ya yule mama yanendana na CV yake tafute mtapata majibu
 
Huyu mama kazingua mwenyewe na ameonyesha uzembe wa hali ya juu sana...

Ukiwa kama mkurugenzi wa halmashauri huwezi kutokufahamu umepewa shilingi ngapi kwa ajili ya miradi mikubwa mikubwa....

Naweza nisikumbuke exactly figure mfano 2,855,000,000/=(bilion mbili na milion mia nane hamsini na tano)....lakini pia siwezi nikasahau totally kama nilipewa kiasi cha 2bilion na usheheee.....sasa alishindwa nini hata kutaja figure ya makadilio halafu akamwambia raisi kuwa iyo figure hana uhakika nayo kwa asilimia zote....eti sikumbuki nina majukumu mengi!!!

Hivi hata wewe tu ulieajiliwa kwenye kiofisi kinachokupa mkate wa kila siku ,hivi unaweza ukamwambia boss wako kuwa hii kazi sijafanya au hiki kitu sikijui kwa sababu nina majukumu mengi???!!!! Hivi ni heshima gani iyo unayomuonyeshea huyo mtu aliekupa hayo majukumu?? hawa wakurugenzi walistahili wakapimwe na mkojo kabisaaaa

Hata darasani kuna walimu wengine kama swali hulijui kabisa na ukajitahidi kujaza maelezo yako basi mwalimu atakupa asilimia 30 kati ya 100....sasa wewe swali hulijui halafu unaacha wazi kabisa hata hujisumbui kujaza chochote unategemea nini??...lazima nikupe Zero na masikio yake!!!!!
Jiandae kupewa cheo
 
Hivi hawa wakurugenzi wanateuliwa kwa vigezo gani?ingekuwa vizuri nafasi hizi ziwe za kuapply na halafu watu wanashinda kwa kuwa interviewed.Hii ya kuteuliwa sometimes mihemuko inatumika kuwapata.

Ila pia huyo mama majibu yake yalikuwa yanataka kumdharirisha Mheshimiwa Raisi kwamba amemuuliza swali ambalo agepaswa kumuuliza DT wake.kwa hiyo ni swali too operational ,yaani siyo strategic kwa ngazi ya DED.hapo ndipo alipochemka Kitu chochote anachoulizwa raisi ni kikubwa kinatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wa juu kabisa .maana yeye ndiyo mwenye maona ya juu kuliko yoyote nchini.

Kwa hiyo hilo ni somo kwa viongozi wote usije ukategemea Swali la bosi wako lijibiwe na mtu aliyeko chini yako(subordinate).hiyi ni insubordination

Ni sawa na Pale kamati ya Bunge walipomuita Mwenyekiti wa board ya UDSM Kwenda dodoma kuhojiwa halafu badala yake Mkandala VC akaenda,kamati ilifanya sahihi kumfukuza.
Kwahiyo ukiwa DED unatakiwa umeze data za idara zote!! Aisee nadhan watunge na mtihani kabisasa!!! Shame
 
Paskali,

Lets be serious. Mimi nadhani ifike sehemu tutofautishe majukumu yetu ya kila siku na sentiments/emotions. Hivi kweli itawezekanaje Mkurugenzi huna data za hela ya serikali kwa kitu sensitive kama barabara, maji, afya au elimu? Sasa itakuwaje kuhusu madai ya walimu na watumishi wa kada ya chini ambao wala hukutani nao na wala hawana access na wewe? Hawa ndo wanasababisha watumishi hewa, vyeti fake nk. Kwa sababu usimamizi ni zero.

Wote hata tusiokuwa wakurugenzi tunajua kabisa JPM anafanya detailed study kabla ya kwenda kwenye mkutano/kuhutubia. Hii tabia hajaianza leo wala jana. Lilikuwa swala la Mkurugenzi kuhakikisha anawaita watendaji walio chini yake (elimu, afya,barabara, maji nk) kila mmoja anampa summary ya page moja ya key things kwenye idara. Kwanza nilimshangaa kitendo cha kwenda pale mbele hana hata karatasi mkononi.

Halafu mama bila aibu anasema eti tumuite engineer ndo mwenye majibu! sasa yeye kazi yake ni nini pale???

Tufike sehemu tubadilike. tuache kutetea uozo. Hili swala lilikuwa halihitaji utaalamu zaidi ya ufuatiliaji tuu basi.

Mkuu, you also need to be serious.

Hata ukimfuata Rais kesho ukamwuliza hazina imekusanya kiasi gani mwezi huu, kama haja-consult na watu wa hazina hawezi kukupa jibu wakati ule. That is for fact. Hivyo hivyo na Mkurugenzi. Wewe unafikiri kazi ya Mkurugenzi ni kama kazi ya Headmaster?

Lakini Wilaya ina miradi, idara na vitengo vingi sana. Huwezi kukurupuka na kumwuliza Mkurugenzi bajeti fulani akakupa jibu hapo hapo (Hasa kama jibu linataka ataje figure). Mkurugenzi anafanya kazi through head of departments, na wakuu wa vitengo.

You people need to be reasonable in some of the things you say. Hata Rais anafanya kazi thru Ministers na RCs. Hujawahi kumwona akiulizwa na wananchi kisha anaomba Waziri au Mkuu wa Mkoa asimame na kutoa jibu?.

You need to be serious...
 
Kujua idadi ya fedha zako hiyo sio takwimu hiyo ni kujua ni sawa na kujua namba yako ya simu tu. Namba yako ya simu ni takwimu? Wale wakurugenzi ni wazembe.

Mwanangu wa miaka 14 amehifadhi namba za simu za familia nzima in case akipata matatizo itakuwa wao watu wazima na elimu zao. Wanachukulia mambo for granted let them go for granted.
Kwa hiyo wanaokwenda bank kuomba bank statement ya akaunti zao wanafanya makosa gani?
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, and the right time, but not doing it right.

Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, a human being, anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu, lakini pia yeye ni taasisi inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anategemewa kuwa perfect by doing the right thing, at the right time and do it right!. Makosa yoyote madogo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, but not our president.

Angalia kilichofanyika hapa:



Isn't This Bullying and Intimidation?.
Kwa maoni yangu, this is bullying na intimidation. Kwa rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi ya ng'ombe, mbuzi, tena nikasikia kuwa ana hadi idadi ya samaki wetu.

Alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za TANROADS na zimejengwa kwa kiasi gani. Then rais wetu asitegemee kila kiongozi wa umma, atakuwa mzuri kama yeye kwa kukurupushwa tuu na kuulizwa figures, alafu ajibu kutoka kichwani.

Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?.
This is not fair, hii sii haki, hii ni some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu. Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa.

Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu, hivyo mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye mambo madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakushuhudia makubwa zaidi, tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe tunamchoresha!.

Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali.
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya Tumbua tumbua, na kulalamikia double standards. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri

Marais Wengine Hufanya Vipi?.
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.

A Way Forward:
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two personalities, kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli, na Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Dr. Magufuli anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote, lakini Rais Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.

Namtakia ziara njema.

Paskali

Huyo DED hakutakiwa kukumbuka figure zote na kama alijijua ana mambo mengi na mengine hawezi kuyakumbuka angeyaandika mahali......pia yule mama hakupaswa kumjibu Rais vile.
 
Pascal Mayalla



6 most important features of Dictatorship

1. One Party, One Leader and One Programme:

In dictatorship only one party is allowed to exist and it is the dictator's own party. Other political parties, associations and organizations are not allowed to function. These are banned. All opposition to the dictator is ruthlessly suppressed. Hitler used to say, "Swastika or gallows".

One Leader:

Under dictatorship, leadership is given to a single man. Full faith is to be concentrated in the leader. The leader is supposed to represent national unity. He is considered to be a symbol of national prestige. He is the final authority in every matter and his word is supreme.

One Programme:

The whole country is supposed to have one political programme and it is the programme of dictator's own party.


2. Absence of Individual Liberty:

The individual does not enjoy any liberty or rights under dictatorship. Maximum obedience to the laws is equated to the maximum liberty. People are not allowed any liberty of speech, association and press. All agencies of education and propaganda such as schools, colleges, radio, papers and films are controlled by the state. In the words of Mussolini "people do not want liberty but they want law and order.

" No criticism against the dictator is tolerated. People are supposed to believe and obey. Democratic slogans of liberty, equality and fraternity are replaced by slogans like duty, discipline and sacrifice. Mussolini asserted, "Liberty is a dead carcass, I kick it."

3. National Glorification:

Dictators glorify their nations to an illogical extreme. A mad sense ol patriotism is inculcated in the minds of the people. They are made intensely nationalistic.

The state is regarded as the march of God on earth. The state is considered to be the end and the individual a means to that end. People are supposed to sacrifice their lives on the alter of state.

4. Glorification of War:

Dictators glorify war. War is considered to be essential for the normal health of body-politic. The state is all powerful and it must enhance its prestige. The dictators adopt a war-like policy and glorify brute force as the means for achieving national greatness. In the opinion of Hitler, "In eternal warfare, mankind has become great; in eternal peace it will be ruined."

To quote Mussolini, "War is to the man what maternity is to the woman."

5. Totalitarian State:

Dictatorship is a totalitarian state which controls each and every aspect of human personality, and takes into its fold all human activities in the social, economic, political, educational, religious and cultural spheres.

No margin for individual liberty is left behind. "Nothing against the state, everything for the state, nothing outside the state" is the basic principle of dictatorship.

6. Racialism:

Dictators preach racialism. The Germans under Hitler regarded themselves to be superior to the people living in the rest of the world. They claimed that they belonged to the ancient Aryan stock. As such they regarded themselves to be superior to others.

Similarly, the Italians claimed that they belonged to the race of the ancient Roman conqueror and that they had a divine mission to conquer the world.

Conclusion:

Dictatorship was a mad doctrine. World War II was the direct result of these dictatorships. Democratic camp led by U.S.S.R., England and America uprooted dictatorship from the world and gates for the growth of democracy were again opened.
 
Kwa hiyo wanaokwenda bank kuomba bank statement ya akaunti zao wanafanya makosa gani?
Mfano wangu haufanani na bank statement unafanana na bank balance kwa maana ya kwamba bank statement ni takwimu za akaunti husika lkn bank balance ni jumla ya fedha zilizopo kwenye bank account husika. Kujua bank balance ni rahisi kuliko bank statement. Mh Rais alitaka kujua idadi tu ya fedha za road fund sio takwimu zake kwa maana zitajenga nini wapi n.k hizo ndio takwimu.
 
Mkuu while I may agree with you, Lakini tukubali huyu mama ndo accounting officer! Hivi kweli hakuona yaliyomkuta mama Malecela RC wa Shinyanga?

Hii haikuwa ziara ya ghafla. Alijua Mkuu anakuja. Na kwenye mikutano kama ile..kinachoongoza ni kero za wananchi (barabara, umeme, maji, afya na elimu). JPM ni mwanasiasa. Alipigiwa kura. Waajiri wake ndo wale walikuwa wamekusanyika pale.

Mkurugenzi alishindwa kupewa summary ya page moja kila idara?? common bro! Lets be real.

Tujifunze. Mama hajaulizwa details za barabara na mitaro. Ameulizwa pesa na yeye ni mtaalam wa fedha! By the way pesa haiendi kwa engineer wa wilaya bila mkurugenzi kuiidhinisha! Then tunaambiwa hajui!

Hapana akapumzike tuu. Hakuna namna.
Swali la JPM ni la kiidara na ndio maana tuna wakuu wa idara!

Kwamba alishindwa nini kwenda na japo na summary page moja ya kila idara... hapo tena tujiulize, as a DED, kwanini aende na summary ya accounts balances na sio idadi ya shule za msingi, idadi ya shule za sekondari, idadi ya zahanati, idadi ya vituo vya afya, idadi ya walimu wa shule ya msingi, idadi ya walimu wa sekondari, idadi ya manesi, idadi ya visima, idadi ya watoto wa mitaani na kadhkalika na kadhalika... hayo yote yapo chini ya DED!

Sasa ataenda na summary ya vitu vingapi wakati hafahamu ataulizwa nini?!

Kwamba, DED ni mtaalamu wa masuala ya fedha, not necessarily tena kwa kipindi hiki cha JPM ndo kabisa manake usisahau JPM kamteua hadi Hudson Kamoga wa Clouds kuwa DED.

As far as I know, Kamoga ana Diploma ya Marketing na Bachelor ya Mass Communication... sasa hapo wapi na wapi kuwa mtalaamu wa masuala ya fedha!!

Historically, ma-DED wengi walikuwa wanatokana na Planning Officers ambao wengi wao background yao wala sio masuala ya fedha though kuna idadi ya kutosha ambao background yao ni economist!

Still, economist sio mtalaamu wa masuala ya fedha!

Halmashauri mtu ambae moja kwa moja anahusika na masuala ya fedha ni District Treasurer. Chini ya DT ndo kuna accountants.

Kwamba pesa haiendi kwa Engineer bila ya yeye kuidhinisha, jibu NDIYO kwa sababu DED na DT ndio Chief Signatories na signature nyingine ya Mkuu wa Idara plus at least one more signature. Sasa ikiwa akaunti zote lazima apige sahihi, do you really believe ndo anawajibika kufahamu balances zake just at a glance?! Unataka kuniambia yule Dr. Mpango leo hii ukimsimamisha atakutajia balances za akaunti za Hazina?! Anaweza kutaja kila wizara imepewa shilingi ngapi?!

But all in all, hivi hilo peke yake lilitosha kumfukuza kazi!!! Yaani unafukuza mtu kazi eti kisa haja-memorize amount ya Road Fund!!!
 
Accountant wa nini wakati yeye ndio accounting officer wa wilaya?si hata angetembea na ''tablet''basi zenye kukokotoa matumizi na mahesabu,wacha awanyoshe bana watu walizoea kufanya kazi kwa mazoea unajua mkubwa wako anakuja basi hata ''kujisomea ''kidogo ili uwe na la kujibu napo unashindwa

I agree she should have done her homework so does any other responsible person on his field... [emoji116] je kwa hili kwa maoni yako tusimteue Rais kwa kukosa kuelewa A. geography, B. a well documented facts C. Rais of the neighbouring country

The answer is No, that’s why he is our President, but what are you suggesting in this case is hypocrisy!




Stop being emotion, if we allow our emotion to get better of us, a lot will be said in reverse by his critics, probably you believe everything what comes from the pulpit?, then it is very much a lost cause for so many of us...
 
sasa subiria wengine watakapojibu maswali hata wasiyoulizwa ikifika zamu ya kuchinjwa kwao....
 
Mfano wangu haufanani na bank statement unafanana na bank balance kwa maana ya kwamba bank statement ni takwimu za akaunti husika lkn bank balance ni jumla ya fedha zilizopo kwenye bank account husika. Kujua bank balance ni rahisi kuliko bank statement. Mh Rais alitaka kujua idadi tu ya fedha za road fund sio takwimu zake kwa maana zitajenga nini wapi n.k hizo ndio takwimu.
Mkuu, usizungushe sana maneno bila sababu za msingi. Bank balance inapatikana kwenye bank statement. Kwa hiyo anayeomba bank statement anafanya kwa makusudi ya kuangalia transactions na ili hatimaye ajiridhishe kuhusu bank balance. Your point is so moot...
 
Mkuu, usizungushe sana maneno bila sababu za msingi. Bank balance inapatikana kwenye bank statement. Kwa hiyo anayeomba bank statement anafanya kwa makusudi ya kuangalia transactions na ili hatimaye ajiridhishe kuhusu bank balance. Your point is so moot...
Unaweza ukaomba bank balance pekee bila bank statement. Kitaalam bank statement maana yake ni takwimu za account na bank balance ni salio la account. Mh Rais alitaka Salio sio Takwimu.
 
Well thought out Pascal!

Mimi naona rais anatawaliwa sana na mihemko ya sifa za kushangiliwa jukwaani yeye akidai anawajali masikini na wanyonge.

Bahati mbaya wengi wanaomshangilia ni wale wenye uwezo mdogo sana wa uelewa na upambanuzi wa mambo. Hao ndio kazi yao kushangilia kila analolisema rais hata kama ni la kijinga.

Hata hizo takwimu anazotaja jukwaani za mabilioni na matrilioni ni watu wachache sana wanaozielewa vizuri. Naona kama anamatatizo ya managerial skills na ukosefu wa elimu ya mawasiliano kwa umma - mass comunication. Anaongea kila linalokuja kichwani mwake. Wakati mwingine anajipiga chenga mwenyewe.

Wakati akiteua huwa anadai kuwa amewachunguza na kujiridhisha vya kutosha. Wakati wa kutengua huanza kuwakandia kana kwamba hakuwateua yeye.

Rais pia anahitaji elimu zaidi kwaupande wa hotuba. Wataalamu wa hotuba na public speaking. Upande huuu wamsaidie yuko chini sana!
 
Katika hili namuunga mkono Mh. Rais kwa hatua aliyochukua, mkuu wa taasisi haujui umeletewa kiasi gani kwenye kipengele cha mapato yako! Hii ni uzembe wa hali juu kabisa, pesa ndio uti wa mgongo wa taasisi yeyote ukiona Accounting Officer hajui issue za pesa basi fahamu kuwa hakuna anachokijua kwenye taasisi yake.

In fact issue za pesa zinatakiwa zichukue 50% ya muda wa kazi zake ili aweze kupanga priority kwenye kutekeleza objective zake pamoja na kutafuta mapato zaidi. Hawa ndio wale hata idadi ya wafanyakazi alionao hajui, namna hii hawezi kukosa kulipa mishahara hewa aliyobambikiwa na maafisa utumishi
 
Hao DED'S ni wazembe tu, Paskali unalea uoza ambao ndio umekua kansa ya kuturudisha nyuma kama taifa;

Inakuwaje mhusika mkuu hufahamu lolote kuhusiana na kazi yako?? Sasa upo hapo kufanya nini?? Mfano sisi wanasheria tunajua kila jambo kuhusiana na files tunazohandle; hata ukimwamsha mtu toka usingizini ukimuuliza kuhusiana na file flani lazima uwe unalifahamu; sasa kama hufahamu facts kuhusiana na kesi zako utazisimamia vipi ipasavyo??

Huo ni uzembe na kiashiria cha uvivu uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom