Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Mkuu Paschal hao wakurugenzi kuna taarifa kuwa walikuwa wanafanyakazi kwa kushirikiana wa madiwani wa Chadema bila kubaguana, tatizo mzee hataki kuona watu waccm wanaelewana na wapinzani, mkuu umewahi kuona maswali kama hayo ameulizwa Bashite, Ally Happy, Mnyeti, Gumbo? hawa walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu, Mkurugenzi anawakuu wa idara kuna Engineer wa barabara kwa nini asiulizwe yeye?
Wewe na huyo Paschal mnaleta ngonjera za kisiasa Mkurugenzi gani asiyejua hata hela za mradi zimeingia ngapi na ngapi zimetoka ,ngapi zimefanya hiki au kile,kazi yake nini?

Akiwa ndie accounting officer, tusilete siasa kwenye mambo ya msingi wewe na huyo mwandishi wako Mayala,huu ni uzembe walijua kabisa mkubwa wao anakuja hata kujiandaa walishindwa.

Kila siku utasikia oh mkurugenzi ana kikao oh mkurugenzi yupo saiti,tuache kufanya kazi kwa mazoea.hata paschal mwenyewe anajua kama mtu aliyemwajiri kwa kazi fulani basi hata akimuuliza ,''habari kuu'' ya mwaka jana basi huyo mhariri wke lazima ajue ndio kazi yake sasa sijui kama Mheshimiwa akimuuliza huyo kijana wake kuhusu habari fulani na huyo kijana akashindwa kujibu wakati ni kazi yake sijui atampandisha cheo au atamwambia ondoka kazi imekushinda sababu umeshindwa kuonyesha wapi lile faili la barua ya khaki lipo wapi
 
You already said you are an accountant! She is not!

She directly mentions, I need to get with the accountant to get him Mh Rais the correct figures,

Do you have specifics of what Mkurugenzi entails?
Accountant wa nini wakati yeye ndio accounting officer wa wilaya?si hata angetembea na ''tablet''basi zenye kukokotoa matumizi na mahesabu,wacha awanyoshe bana watu walizoea kufanya kazi kwa mazoea unajua mkubwa wako anakuja basi hata ''kujisomea ''kidogo ili uwe na la kujibu napo unashindwa
 
Pascal,

Usitumie nguvu nyingi kuhalalisha vitu vidogo vidogo na visivyo vya msingi. Kama Rais tunamtegemea kiongozi wetu awe perfect katika kila mambo analolifanya na ikiwezekana kwa ubora kuliko aliyetangulia but kamwe haijawahi wala haitatokea kwenye nchi yoyote kupata mtu perfect kwa kila jambo analofanya. Cha ajabu umekalia kuangalia udhaifu wa JPM as a person na kuhusisha na Ofisi ya Urais Lin sijawahi kukuona ukitake trouble kuonyesha strength zake as a person na kuzihusisha na Ofisi yake pia.

Udhaifu na ubora wa mtu ndio unamfanya kuwa personality he/she is. La muhimu kama Rais, je ana madhaifu mengi yanayomdisqualify ama ana ubora mwingi unaomfanya ku-qualify kama mojawapo ya viongozi bora kuwa hi kutokea barani Afrika na duniani?

As an analyst usilinganisha Magufuli asa a Person na Magufuli as a President, linganidha Magufuli dhidi ya Rais yeyote, hapo ndo utamchambua ili kumtendea haki, japo napo unaweza ukaambulia utumbo kama haujui kile jamii inayoyataka kutokana kwa Rais.
 
Mkuu Paschal hao wakurugenzi kuna taarifa kuwa walikuwa wanafanyakazi kwa kushirikiana wa madiwani wa Chadema bila kubaguana, tatizo mzee hataki kuona watu waccm wanaelewana na wapinzani, mkuu umewahi kuona maswali kama hayo ameulizwa Bashite, Ally Happy, Mnyeti, Gumbo? hawa walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu, Mkurugenzi anawakuu wa idara kuna Engineer wa barabara kwa nini asiulizwe yeye?
Kushirikiana na madiwani wa Chadema ndio kumewafanya wasifahamu au kusahau total figure ya road funds ktk halmashauri wanazoziongoza?
 
Daaah ningekua mimi na kazi naacha... Mama wa watu anajikanyaga ka mtoto asee!!

Kuna kitu hujui, kuna LEADER na MANAGER!! Magufuli is not a leader, he is a manager!! Na angefaa sana angekua waziri mkuu!! Rais huwezi fanya upuuzi kama ule!! Inadhihirisha ni kiasi gan magu alivyo na stress na hapo ndio kapata pa kuzitolea!!

Sasa embu jiulize yule mama ataweza kufanya kazi kwa ufanisi tena kweli?? Psychologically atakua okey tena??
Anaweza endapo atapangiwa majukumu yasiyohotaji kumbukumbu sensitive.
 
Tunashukuru kwa tafakari yako lakini Paskali nakuomba unapowasilisha jambo lako chonde tumiia lugha moja, usichanganye lugha. Kuna mahali unaenda vizuri lakini unapochanganya unaharibu. Tunajua umesoma na unajua Kingereza lakini hata wataalam wa lugha hii wanaona waziwazi unapojikanyaga mara unapoanza kuchanganya lugha.

Wachangiaji wengi wa JF ni wale wakujionyesha kwamba wanajua jambo fulani na wana uwezo wa kuchambua lakini nadhani wewe siyo wa aina yao.

Kiswahili bado ni lugha inayojitosheleza na hakihitaji mbwembwe za kupambwa na lugha nyingine.
 
Back then, nimefanya sana kazi na halmashauri! Labda kwa sasa, lakini kwa miaka ya nyuma Halmashauri walikuwa na rundo la accounts ambazo si rahisi mtu ukariri! Bora basi kama alivyojibu huyo mama kwamba anagalau angeulizwa DT badala ya DED ingawaje, hata DT nae ingekuwa ni kumuonea na mtu wa kuulizwa direct question namna hiyo alipaswa kuwa Mkuu wa Idara.

Yaani alichofanya JPM ni sawa sawa na kumsimamisha Kassimu Majaaliwa na kumuuliza Bajeti ya Wizara ya Kilimo ni kiasi gani na akishindwa kujibu, anatumbuliwa!!
 
Paskali,

Lets be serious. Mimi nadhani ifike sehemu tutofautishe majukumu yetu ya kila siku na sentiments/emotions. Hivi kweli itawezekanaje Mkurugenzi huna data za hela ya serikali kwa kitu sensitive kama barabara, maji, afya au elimu? Sasa itakuwaje kuhusu madai ya walimu na watumishi wa kada ya chini ambao wala hukutani nao na wala hawana access na wewe? Hawa ndo wanasababisha watumishi hewa, vyeti fake nk. Kwa sababu usimamizi ni zero.

Wote hata tusiokuwa wakurugenzi tunajua kabisa JPM anafanya detailed study kabla ya kwenda kwenye mkutano/kuhutubia. Hii tabia hajaianza leo wala jana. Lilikuwa swala la Mkurugenzi kuhakikisha anawaita watendaji walio chini yake (elimu, afya,barabara, maji nk) kila mmoja anampa summary ya page moja ya key things kwenye idara. Kwanza nilimshangaa kitendo cha kwenda pale mbele hana hata karatasi mkononi.

Halafu mama bila aibu anasema eti tumuite engineer ndo mwenye majibu! sasa yeye kazi yake ni nini pale???

Tufike sehemu tubadilike. tuache kutetea uozo. Hili swala lilikuwa halihitaji utaalamu zaidi ya ufuatiliaji tuu basi.
 
Amezoea kupika data, sasa alitaka na wenzake pale wapike data, huyo mama kajitahidi sana.

Sema ndio walikuwa wanatafutwa na hasa ukizingatia ni dada yake Dr. Dau, pia kama wanaelewana na Upinzani ndio balaa.
 
Mkuu Pascal Mayalla,

Ingawaje binafsi mara kwa mara huwa naipinga serikali ya JPM na JPM mwenyewe lakini hili la huyu mama ningepinga hata kama lingefanywa na nani!!!

Back then, as a Banker, nilifanya sana kazi na halmashauri! Labda kwa sasa, lakini kwa miaka ya nyuma Halmashauri walikuwa na rundo la accounts ambazo si rahisi mtu ukariri! Bora basi kama alivyojibu huyo mama kwamba anagalau angeulizwa DT badala ya DED ingawaje, hata DT nae ingekuwa ni kumuonea na mtu wa kuulizwa direct question namna hiyo alipaswa kuwa Mkuu wa Idara.

Yaani alichofanya JPM ni sawa sawa na kumsimamisha Kassimu Majaaliwa na kumuuliza Bajeti ya Wizara ya Kilimo ni kiasi gani na akishindwa kujibu, anatumbuliwa!!

Mkuu while I may agree with you, Lakini tukubali huyu mama ndo accounting officer! Hivi kweli hakuona yaliyomkuta mama Malecela RC wa Shinyanga?

Hii haikuwa ziara ya ghafla. Alijua Mkuu anakuja. Na kwenye mikutano kama ile..kinachoongoza ni kero za wananchi (barabara, umeme, maji, afya na elimu). JPM ni mwanasiasa. Alipigiwa kura. Waajiri wake ndo wale walikuwa wamekusanyika pale.

Mkurugenzi alishindwa kupewa summary ya page moja kila idara?? common bro! Lets be real.

Tujifunze. Mama hajaulizwa details za barabara na mitaro. Ameulizwa pesa na yeye ni mtaalam wa fedha! By the way pesa haiendi kwa engineer wa wilaya bila mkurugenzi kuiidhinisha! Then tunaambiwa hajui!

Hapana akapumzike tuu. Hakuna namna.
 
Ndio shida ya wanawake ukimuuliza kuhusu gharama za gauni, nywele, mekapu, lotion nk atakupa data zote ila mambo ya serikalibhana kumbukumbu yoyote huo ni ujinga sana

Mimi ninaumia kwa huu utawala lakini kaa hili acha tu atolewe hafai kabisa anaweza hata asikumbuke siku zake za kuble..

Timulia mbali kuna watu wanajua hizo kazi wapo wengi tu

Aaaaaah pumbafu amenikera sana yule mama ndio maana nikipewa nafasi wanawake ni wa kupunguza kwenye utendaji, utamkuta anajiangalia kwenye kiyoo wakati yuko ofisini aaah pumbafu kabisa

Nenda zako bwaaanaaaa kalime viazi
 
Nilimwonea huruma sana huyo mama aisee alikuwa anatamani ardhi ipasuke aingie , huyu mzee noma sana hakuwa fair at all

Ni udhalilishaji Rais alitakiwa kumuuliza lakini si kama alivyofanya kama anaongea na mtoto vile

Mtamkumbuka sana mkwere zama hizi za tingatinga
 
Huyu mama kazingua mwenyewe na ameonyesha uzembe wa hali ya juu sana...

Ukiwa kama mkurugenzi wa halmashauri huwezi kutokufahamu umepewa shilingi ngapi kwa ajili ya miradi mikubwa mikubwa....

Naweza nisikumbuke exactly figure mfano 2,855,000,000/=(bilion mbili na milion mia nane hamsini na tano)....lakini pia siwezi nikasahau totally kama nilipewa kiasi cha 2bilion na usheheee.....sasa alishindwa nini hata kutaja figure ya makadilio halafu akamwambia raisi kuwa iyo figure hana uhakika nayo kwa asilimia zote....eti sikumbuki nina majukumu mengi!!!

Hivi hata wewe tu ulieajiliwa kwenye kiofisi kinachokupa mkate wa kila siku ,hivi unaweza ukamwambia boss wako kuwa hii kazi sijafanya au hiki kitu sikijui kwa sababu nina majukumu mengi???!!!! Hivi ni heshima gani iyo unayomuonyeshea huyo mtu aliekupa hayo majukumu?? hawa wakurugenzi walistahili wakapimwe na mkojo kabisaaaa

Hata darasani kuna walimu wengine kama swali hulijui kabisa na ukajitahidi kujaza maelezo yako basi mwalimu atakupa asilimia 30 kati ya 100....sasa wewe swali hulijui halafu unaacha wazi kabisa hata hujisumbui kujaza chochote unategemea nini??...lazima nikupe Zero na masikio yake!!!!!
 
Hapa kazi tu.

Wakurugenzi hao wamejidhalilisha wenyewe,Halmashauri na mamlaka ya uteuzi.

Katika muktadha wa ziara ya kiongozi mkuu katika eneo lako haitarajiwi ukakosa data zote muhimu au maeneo mahsusi ya miradi iliyoletewa fedha na Serikali kuu.

DED kama accounting officer ana wajibu wa kujua kila senti iingiayo na kutoka halmashauri kwa kichwa kwani ni kazi yake ya kila siku na ni maswali anayoyajibu kwa wawakilishi wa wananchi au wananchi moja kwa moja.

Isitoshe mkurugenzi ana vikao vya kila juma au kila siku au kila mwezi vinavyombrief kuhusu maswala ya miradi ya maendeleo na fedha zinazotarajiwa kupatikana au zilizopatikana kutoka vyanzo vyote.yaani kuhusu fedha ya miradi kwa mkurugenzi ni sawa na sala ya baba yetu na muumini wa kikiristu.

Unapokuwa na mkurugenzi asitefahamu ni kiasi gani cha fedha za road fund zimefika kwenye halmashauri yake hutegemei kama ataweza kusimamia mradi wa barabara husika na mambo ndipo yanapokwamia na lawama au matusi yatarudi kwa mh Rais.

DED kama accounting officer aka afisa masuhuri wa halmashauri huandikiwa kwa barua kiasi cha fedha za mradi zinazoingia halmashauri sometimes days or weeks before disbursement ya hizo funds.

DED hupelekewa na mweka hazina statement au taarifa ya fedha yoyote inayoingia halmashauri.
Pia fedha yoyote inayoingia halmashauri hujadilowa kwenye vikao vya kamati za mipango na fedha na hatimaye baraz zima la madiwani ambalo katibu wake ni DED.

Kwa maoni yangu hakuna excuse ya DED kushindwa kujua figure ya fedha nyingi za mradi wa barabara zaidi ya kiwango kikuu cha uzembe.

Kama DED hajui ni kiasi gani cha fedha za mradi wa road fund ambayo ni nyingi how come anaweza kujua deni au fedha ya mtumishi(say nauli ya likizo) kama mdogo mfano mwalimu wa shule ya msingi aliyeko kwenye halmashauri yake???

Wakurugenzi hawa waneonesha kiwango kikubwa cha irresponsibility na wamestahili adhabu waliyopata.

Hilo ni funzo kwetu sote especially watumishi wa umma.

JPM ni no nonesense President, every subordinate must have known him better and therefore he/she should be super prepared .

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Ivi unajua umbali Wa jua to ardhini,,nikisema alidanganya nitakosea?tuache kukurupuka kukubali kila kitu,,kubali kila kitu kama huna access ya kujua kutafiti
 
Back
Top Bottom