Majibu ya yule mama yanendana na CV yake tafute mtapata majibuBwana Pascali. Swali aliloulizwa yule mama mara tatu mfululizo tena kwa kuonywa juu yabmajibu yake kwa Rais si swali baya kwa MKURUGENZI.
Haiwezekani mkurugenzi asijue ameletewa pesa kiasi gani kwa ajili ya BARABARA na akiba iliyopo ni kiasi gani.
Mkurugenzi anatakiwa afahamu akiba ya pesa zote alizonazo kila siku. Anatakiwa afahamu mapato na matumizi on daily basis.
Tatizo ni kuteua wakurugenzi ambao hawajawahi fanya kazi serikalini hivyo kutijua nini cha kufanya ofisini. Badala yake anataka mhasibu ndiye amsemee kwa bosi wake kwamba kuna pesa kiasi gani.
Isitoshe. Pesa za halmashauri hazipo kwenye mkundi mengi. Sana sana ni pesa ya barabara. Maji. Afya. Makusanyo ya ndani na miradi mingineyo ya hapa na pale.
Jiandae kupewa cheoHuyu mama kazingua mwenyewe na ameonyesha uzembe wa hali ya juu sana...
Ukiwa kama mkurugenzi wa halmashauri huwezi kutokufahamu umepewa shilingi ngapi kwa ajili ya miradi mikubwa mikubwa....
Naweza nisikumbuke exactly figure mfano 2,855,000,000/=(bilion mbili na milion mia nane hamsini na tano)....lakini pia siwezi nikasahau totally kama nilipewa kiasi cha 2bilion na usheheee.....sasa alishindwa nini hata kutaja figure ya makadilio halafu akamwambia raisi kuwa iyo figure hana uhakika nayo kwa asilimia zote....eti sikumbuki nina majukumu mengi!!!
Hivi hata wewe tu ulieajiliwa kwenye kiofisi kinachokupa mkate wa kila siku ,hivi unaweza ukamwambia boss wako kuwa hii kazi sijafanya au hiki kitu sikijui kwa sababu nina majukumu mengi???!!!! Hivi ni heshima gani iyo unayomuonyeshea huyo mtu aliekupa hayo majukumu?? hawa wakurugenzi walistahili wakapimwe na mkojo kabisaaaa
Hata darasani kuna walimu wengine kama swali hulijui kabisa na ukajitahidi kujaza maelezo yako basi mwalimu atakupa asilimia 30 kati ya 100....sasa wewe swali hulijui halafu unaacha wazi kabisa hata hujisumbui kujaza chochote unategemea nini??...lazima nikupe Zero na masikio yake!!!!!
Kwahiyo ukiwa DED unatakiwa umeze data za idara zote!! Aisee nadhan watunge na mtihani kabisasa!!! ShameHivi hawa wakurugenzi wanateuliwa kwa vigezo gani?ingekuwa vizuri nafasi hizi ziwe za kuapply na halafu watu wanashinda kwa kuwa interviewed.Hii ya kuteuliwa sometimes mihemuko inatumika kuwapata.
Ila pia huyo mama majibu yake yalikuwa yanataka kumdharirisha Mheshimiwa Raisi kwamba amemuuliza swali ambalo agepaswa kumuuliza DT wake.kwa hiyo ni swali too operational ,yaani siyo strategic kwa ngazi ya DED.hapo ndipo alipochemka Kitu chochote anachoulizwa raisi ni kikubwa kinatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wa juu kabisa .maana yeye ndiyo mwenye maona ya juu kuliko yoyote nchini.
Kwa hiyo hilo ni somo kwa viongozi wote usije ukategemea Swali la bosi wako lijibiwe na mtu aliyeko chini yako(subordinate).hiyi ni insubordination
Ni sawa na Pale kamati ya Bunge walipomuita Mwenyekiti wa board ya UDSM Kwenda dodoma kuhojiwa halafu badala yake Mkandala VC akaenda,kamati ilifanya sahihi kumfukuza.
Paskali,
Lets be serious. Mimi nadhani ifike sehemu tutofautishe majukumu yetu ya kila siku na sentiments/emotions. Hivi kweli itawezekanaje Mkurugenzi huna data za hela ya serikali kwa kitu sensitive kama barabara, maji, afya au elimu? Sasa itakuwaje kuhusu madai ya walimu na watumishi wa kada ya chini ambao wala hukutani nao na wala hawana access na wewe? Hawa ndo wanasababisha watumishi hewa, vyeti fake nk. Kwa sababu usimamizi ni zero.
Wote hata tusiokuwa wakurugenzi tunajua kabisa JPM anafanya detailed study kabla ya kwenda kwenye mkutano/kuhutubia. Hii tabia hajaianza leo wala jana. Lilikuwa swala la Mkurugenzi kuhakikisha anawaita watendaji walio chini yake (elimu, afya,barabara, maji nk) kila mmoja anampa summary ya page moja ya key things kwenye idara. Kwanza nilimshangaa kitendo cha kwenda pale mbele hana hata karatasi mkononi.
Halafu mama bila aibu anasema eti tumuite engineer ndo mwenye majibu! sasa yeye kazi yake ni nini pale???
Tufike sehemu tubadilike. tuache kutetea uozo. Hili swala lilikuwa halihitaji utaalamu zaidi ya ufuatiliaji tuu basi.
Kwa hiyo wanaokwenda bank kuomba bank statement ya akaunti zao wanafanya makosa gani?Kujua idadi ya fedha zako hiyo sio takwimu hiyo ni kujua ni sawa na kujua namba yako ya simu tu. Namba yako ya simu ni takwimu? Wale wakurugenzi ni wazembe.
Mwanangu wa miaka 14 amehifadhi namba za simu za familia nzima in case akipata matatizo itakuwa wao watu wazima na elimu zao. Wanachukulia mambo for granted let them go for granted.
Huyo DED hakutakiwa kukumbuka figure zote na kama alijijua ana mambo mengi na mengine hawezi kuyakumbuka angeyaandika mahali......pia yule mama hakupaswa kumjibu Rais vile.Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, and the right time, but not doing it right.
Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, a human being, anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu, lakini pia yeye ni taasisi inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anategemewa kuwa perfect by doing the right thing, at the right time and do it right!. Makosa yoyote madogo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, but not our president.
Angalia kilichofanyika hapa:
Isn't This Bullying and Intimidation?.
Kwa maoni yangu, this is bullying na intimidation. Kwa rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi ya ng'ombe, mbuzi, tena nikasikia kuwa ana hadi idadi ya samaki wetu.
Alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za TANROADS na zimejengwa kwa kiasi gani. Then rais wetu asitegemee kila kiongozi wa umma, atakuwa mzuri kama yeye kwa kukurupushwa tuu na kuulizwa figures, alafu ajibu kutoka kichwani.
Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?.
This is not fair, hii sii haki, hii ni some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu. Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa.
Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu, hivyo mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye mambo madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakushuhudia makubwa zaidi, tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe tunamchoresha!.
Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali.
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya Tumbua tumbua, na kulalamikia double standards. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri
Marais Wengine Hufanya Vipi?.
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.
A Way Forward:
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two personalities, kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli, na Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
Dr. Magufuli anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote, lakini Rais Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.
Namtakia ziara njema.
Paskali
Mfano wangu haufanani na bank statement unafanana na bank balance kwa maana ya kwamba bank statement ni takwimu za akaunti husika lkn bank balance ni jumla ya fedha zilizopo kwenye bank account husika. Kujua bank balance ni rahisi kuliko bank statement. Mh Rais alitaka kujua idadi tu ya fedha za road fund sio takwimu zake kwa maana zitajenga nini wapi n.k hizo ndio takwimu.Kwa hiyo wanaokwenda bank kuomba bank statement ya akaunti zao wanafanya makosa gani?
Swali la JPM ni la kiidara na ndio maana tuna wakuu wa idara!Mkuu while I may agree with you, Lakini tukubali huyu mama ndo accounting officer! Hivi kweli hakuona yaliyomkuta mama Malecela RC wa Shinyanga?
Hii haikuwa ziara ya ghafla. Alijua Mkuu anakuja. Na kwenye mikutano kama ile..kinachoongoza ni kero za wananchi (barabara, umeme, maji, afya na elimu). JPM ni mwanasiasa. Alipigiwa kura. Waajiri wake ndo wale walikuwa wamekusanyika pale.
Mkurugenzi alishindwa kupewa summary ya page moja kila idara?? common bro! Lets be real.
Tujifunze. Mama hajaulizwa details za barabara na mitaro. Ameulizwa pesa na yeye ni mtaalam wa fedha! By the way pesa haiendi kwa engineer wa wilaya bila mkurugenzi kuiidhinisha! Then tunaambiwa hajui!
Hapana akapumzike tuu. Hakuna namna.
Accountant wa nini wakati yeye ndio accounting officer wa wilaya?si hata angetembea na ''tablet''basi zenye kukokotoa matumizi na mahesabu,wacha awanyoshe bana watu walizoea kufanya kazi kwa mazoea unajua mkubwa wako anakuja basi hata ''kujisomea ''kidogo ili uwe na la kujibu napo unashindwa
Mkuu, usizungushe sana maneno bila sababu za msingi. Bank balance inapatikana kwenye bank statement. Kwa hiyo anayeomba bank statement anafanya kwa makusudi ya kuangalia transactions na ili hatimaye ajiridhishe kuhusu bank balance. Your point is so moot...Mfano wangu haufanani na bank statement unafanana na bank balance kwa maana ya kwamba bank statement ni takwimu za akaunti husika lkn bank balance ni jumla ya fedha zilizopo kwenye bank account husika. Kujua bank balance ni rahisi kuliko bank statement. Mh Rais alitaka kujua idadi tu ya fedha za road fund sio takwimu zake kwa maana zitajenga nini wapi n.k hizo ndio takwimu.
Unaweza ukaomba bank balance pekee bila bank statement. Kitaalam bank statement maana yake ni takwimu za account na bank balance ni salio la account. Mh Rais alitaka Salio sio Takwimu.Mkuu, usizungushe sana maneno bila sababu za msingi. Bank balance inapatikana kwenye bank statement. Kwa hiyo anayeomba bank statement anafanya kwa makusudi ya kuangalia transactions na ili hatimaye ajiridhishe kuhusu bank balance. Your point is so moot...