Je, huwa unaignore baadhi ya status za watu whatsapp? Kwanini?

Je, huwa unaignore baadhi ya status za watu whatsapp? Kwanini?

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Natumai mko poa na mnaendelea vyema kuchapa kazi katika kipindi hiki kigumu kwa sasa duniani. Kila mtu kwa imani yake na aendelee kuomba Mungu atuvushe salama.

Iko hivi, leo katika kupitia pitia whatsapp kule status nimegundua kuna baadhi ya watu huwa nina kawaida ya kutohangaika kuview status zao kabisa. Yaani huwa napita tu naenda kuview kwa baadhi, nadhani huenda maudhui yao mara nyingi huwa hayanifurahishi. Kuna wengine kila mara ni watu wa kuweka vijembe. Wengine kuweka weka tu picha na video zao zisizo na mbele wala nyuma(mara anaimba imba). Sasa kwa kiasi flani kama nimewakalili status zao siku zote huwa za aina fulani. Inaweza isiwe mada muhimu sana lakini nilijiuliza tu maswali.

Vipi wewe huwa huangaiki na status kabisa? Kwanini? Au kipi hupelekea wewe kupuuza badhi ya status za watu fulani mara nyingi?


Fuata maelekezo ya wataalamu, jilinde na linda na wengine dhidi ya COVID-19.
 
Mi wasap mwaka wa 3 huu sina, wakati natumia wasap gb au fm nilikua naangalia za dada yangu na mama yangu tuuu, nyingn siangaliii.
Niliacha kuangalia za wengine baada ya kuona mwanaume anaweka picha status karibia 10 hiv na mdada anaweka karibu 15 hiv hlf mwanaume anakuuliza kama umeona status aliyoweka. Mdada naye anakutumia msg "mbn huangaliii status zangu na wasap unaingia kila mda?" Nikaona isiwe kesi, hakuna kuona za kwao jumla
 
Wapo wawili mmoja shabiki wa Liverpool na mwingine wa Chelsea
Wanajua kuumiza hawa maboya aseee!

Yaaaaani wao wakishinda badala ya kufurahia ushindi wao,wanachofanya ni kutuattack sisi....nimemute status zao muda sana
 
Kuna wale Ndugu zetu wa kuweka picha zaid ya 20 kwa siku, Wale huwa naskip bila hata kujiuliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa huwa napita tu kiukweli hata mimi.
Mkuu kama unauzoefu na WhatsApp gb nisaidie sababu ninayoitumia inataka update na nimeenda playstore hawana Google na wao hawana...msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulienda kuupdate playstore kwani mwanzo ulidownload playstore?
Shusha hapa latest version
GBWhatsapp APK Download (Updated) Anti-Ban V9.1 | OFFICIAL
 
Mkuu kama unauzoefu na WhatsApp gb nisaidie sababu ninayoitumia inataka update na nimeenda playstore hawana Google na wao hawana...msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasap gb haipo playstore ila washaifuta nahic, ipo ile y wasap, zile ni apk so unasachi kwenye gugo injini. Nachokumbuka ni kua, unaingia kwenye official site yao au kupitia link iliyoko kwenye hiyo app unapakua faili lingine then unainstol.
Ila ujue ili uweze dowload app nje ya google playstore, lazima uende kwenye setting uruhusu kule kweny security ndy itakubali
 
Tafuta Yowhatsup ni nzuri kuliko GB .
Mmiliki wa GB Yousuf al Baashar wenye whatsup official walimtait akaiondoa hewani.

Nilikuwa mtumiaji wa GB ila Yowhatsup ni zaidi
Mkuu kama unauzoefu na WhatsApp gb nisaidie sababu ninayoitumia inataka update na nimeenda playstore hawana Google na wao hawana...msaada

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, Kuna watu wanaweka vijembe hao,mtu anaweka status si chini ya picha 10 why?, ni mwendo wa kuskip na kumute tu.

Hivi inawezekana mtu akaview status yako afu asionekane kwenye viewers ?,I mean akaview kimya kimya bila wewe kujua??
Hasa wadada wa makazini.😃
 
Back
Top Bottom