Je, huwa unaota umepoteza kiatu/viatu?

Je, huwa unaota umepoteza kiatu/viatu?

Duh... na vp kuota unakimbizwa alafu unashindwa kukumbia ?

Ama ile undadondoka let's say kutoka hewani hadi chini ila hufiki unaelea tu hewani
 
Kuota umepoteza kiatu cha mguu wa kushoto hubeba ujumbe unaohusu hisia zako, upande wa kiroho, ubunifu, au mahusiano ya karibu.

Mguu wa kushoto unahusishwa na upande wa hisia, silika (intuition), na amani ya moyo.Kupoteza kiatu hiki kunaashiria unanyimwa amani ya nafsi au unapitia kipindi cha msukosuko wa kihisia.
 
Duh... na vp kuota unakimbizwa alafu unashindwa kukumbia ?

Ama ile undadondoka let's say kutoka hewani hadi chini ila hufiki unaelea tu hewani
Ndoto hii inaashiria kuwa kuna tatizo au jukumu zito kwenye maisha yako halisi ambalo unahisi huna uwezo wa kulitatua.
Unajihisi "umekwama" na huna nguvu ya kubadilisha mambo yanayoendelea.

Kumkimbia mtu au kitu kunaonyesha unajaribu kukimbia matatizo badala ya kuyakabili.Kushindwa kukimbia ni ishara kutoka kwa akili yako (subconscious mind) ikikukumbusha kuwa huwezi kuyakimbia matatizo hayo milele, lazima usimame na uyatatue.

Kuota unaanguka kutoka hewani halafu unashindwa kufika chini na kuishia kuelea tu, huakisi hali yako ya sasa ya maisha ambapo upo katikati ya mabadiliko makubwa lakini hujui hatma yako itakuwaje.
 
Nna kama mwezi hivi naota nnatoka na visichana vidogo yaani miaka 18 mpaka 20 sio zaidi ya hapo

Na ndoto inajirudia rudia baada ya siku 3 mpaka wiki inajirudia

Na nampango wa kuoa sasa sijui hii ndogo inanishtua nn? Maana mimi ni babu wa miaka 30.
 
Wasichana wa umri huu wanawakilisha mwanzo wa ujana, nguvu, na maisha yasiyokuwa na majukumu mazito.

Ndoto hii inaweza kuashiria kuwa unatamani kurejesha nishati, uhuru, au msisimko uliokuwa nao zamani, hasa kama kwa sasa maisha yako yamejaa majukumu mazito ya kikazi au kifamilia.
 
Umeanza ulozi tena
Ndoto ni unajimu sio ulozi😀
7858e003-ff7a-4c91-884e-d89f252a9f9e.jpeg
 
Kuwa wengine wanaota wako uchi, hawana nguo in a public place.
Tena mimi naotaga napuuu kabisa ndani ya ndoto nagundua hapa sio chooni 🤭

Nashutuka kabla ya usumbufu

Ila sema naota sana nikiwa uchi ile ile utasema me ni mwanga😒
 
Wasichana wa umri huu wanawakilisha mwanzo wa ujana, nguvu, na maisha yasiyokuwa na majukumu mazito.

Ndoto hii inaweza kuashiria kuwa unatamani kurejesha nishati, uhuru, au msisimko uliokuwa nao zamani, hasa kama kwa sasa maisha yako yamejaa majukumu mazito ya kikazi au kifamilia.
Mkuu nifafanulie tena kidogo

So nioe tu wa umri huo hamna shida.. nidadavulie kidogo MH… tafadhali kabla ya yote nakushukuru sana mkuu , asante sana
 
Kuota umepoteza kiatu kwa ujumla kunaashiria kupoteza mwelekeo, kukwama kwa safari ya mafanikio, au kupoteza utambulisho na ulinzi katika maisha yako ya kila siku.
View attachment 3589211

Kiatu katika ulimwengu wa ndoto huwakilisha maandalizi ya hatima yako, mamlaka, na jinsi unavyopiga hatua kuelekea malengo yako.
Watu hawaelewi katika ulimwengu wa ndoto na kwa kiaisi gani transaction za hatma hufanyika. Na hapa ndipo watu wanatakiwa waelewe concept ya kulala na usingizi, pasipo kuelewa kwa kina kwa habari ya usingizi na ndoto hatma nyingi za watu zimekuwa locked na kupewa na direction na viumbe wengine kupitia ulimwengu wa ndoa ( usingizi na kulala ni fumbo sana ) na ndio maana mtu ane tembea katika daraja flani ndani ya ulimwengu wa roho hukuti analala zaidi ya masaa mawili na haya masaa mawili analala kimkakati sio kama nyau 😁😁😁
 
Tena mimi naotaga napuuu kabisa ndani ya ndoto nagundua hapa sio chooni 🤭

Nashutuka kabla ya usumbufu

Ila sema naota sana nikiwa uchi ile ile utasema me ni mwanga😒
Inabidi Kuchukua maamuzi ya Kuchagua serikali gani uitumikia, ili ikupe Vazi. Kingdom of Light ot Kingdom of darkness,,,

Kunya kwenye ndoto ina maana nzuri kwamba unatoka taka mwili (matendo mabaya) lakini ukiona umeshindwa kupata huduma ya toilet hilo ni Tatizo.
 
Respect mkuu..... umeongea vitu really na sensitive kabisa khs hizo ndoto 2..
1... unakimbizwa unashindwa kukimbia
2... ile unadondoka hufiki chini unaelea hewani

Swali dogo, haya mambo unayajuaje mkuu ? Dah ama kipaji au mnafunuliwa
Mshana Jr
 
Back
Top Bottom