- Source #1
- View Source #1
Wakuu
Naona kuna watu wanasambaza picha inayodaiwa kuwa ndiyo ya mrithi wa El Mincho lakini mbona kama imetengenezwa na AI
Naona kuna watu wanasambaza picha inayodaiwa kuwa ndiyo ya mrithi wa El Mincho lakini mbona kama imetengenezwa na AI
- Tunachokijua
- Baada ya kifo cha cha kiongozi wa kundi la wuazaji wa dawa za kulevya nchini Mexico, El Mencho zimesambaa picha ikiambatana ujumbe kuwa huyo ndiye mrithi wa El Mencho.
Wadau wa JamiiCheck kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wameshiriki kuthibitisha uhalisia wa wa picha hiyo na kubainisha dosari walizoziona.
Wengi wamebainisha dosari tofauti tofauti ikiwemo viganja vya mikono kuwa na vidole pungufu huku vikiwa pia katika muonekano usio wa kawaida.
Uhalisia wa Picha hiyo ni upi?
Picha hiyo ina viasharia vya kuwa imehariria ama kutengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde.
Ufuatiliaji zaidi umebainisha kuwa picha hiyo imehaririwa kutoka katika picha ya Waziri wa mambo wa nje wa Marekani Marco Rubio akiwa kando ya Makamu wa Rais wa Marekane JD Vance iliyopigwa Februari 24, 2025.
Licha ya dosari zake lakini pia nyenzo za kidigitali za kubainisha maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde, matahalani Hive Moderation imebainisha kuwa 99% ya picha hiyo ina viashira vya AI.