Je, huyu ni rafiki mwema kwangu?

Mimi nilikuwa naye wa aina hii. Nilijaribu sana kumvumilia. Akawa ananifanyia visa lkn naendelea kumsaidia. Nikawa namchangia michango mikubwa mikubwa ya harusi, misiba... Lakini upande wangu hatoi kitu! Mara ya mwisho nilimkopesha milioni 1. Akarudisha lakhi 6 ikabaki lakhi 4.

Mpaka leo hajairudisha iliyobaki. Nikamwacha. Wala simdai. Kila mtu akaendelea na maisha yake. Miaka zaidi ya 8 hajawahi kuomba mkopo tena. Siku hizi nasikia anakopa kwa watu wengine, ambao nawafahamu kwa sababu tulisoma pamoja. Jibu langu - binadamu wa aina hiyo wapo. Ukishawajua, wasikusumbue.
 
Huyo ni mwanaume mchane live wala huna haja ya kumblock wanawake ndo wako ivi ila mwanaume unamchana ukweli afu unatulia zako
 
Rafiki mkia wa fisi.......
 
Hao nilisha kutana nao , nlichouma ukiamua kumsaidia mtu fanya kama unatoa sadaka tu usitegemee chochote kutoka kwake
 
Hao nilisha kutana nao , nlichouma ukiamua kumsaidia mtu fanya kama unatoa sadaka tu usitegemee chochote kutoka kwake
Sio hivyo mkuu, huyo jamaa nilishawahi kumuomba msaada wa kumkopa tu na nilimuhaidi wiki ijayo namrudishia hela yake na hapo nipo msibani, kilicho niuma ni matatizo yaliyo nipata alafu jamaa asinikope na pesa alikuwa nayo, nisingepata matatizo wala nisingemsumbua. Nilifanya hvyo kwa kuamini ndio pekee mtu aliye karibu yangu
 
Dawa yake mkaushie atajileta tu na shida zake.
 
Roll model sanamu letu limetua bandarini, ulinzi tutaomba suma Jkt
 
Kwani lazima kua na no Zake .tumia vizuri storage ya simu yako bhna vitu kama ivyo nivya kuondoa haraka sana
 
Huyo anaroho ya kimasikini kama maisha yake yalivyo kua, maskini huzaliwa na roho mbaya ni wachache wakarimu...tenda wema uende zako usisubirie malipo
 
Kwani lazima kua na no Zake .tumia vizuri storage ya simu yako bhna vitu kama ivyo nivya kuondoa haraka sana
Kabisa mkuu watu wengine hawafai hata kuwa nao karibu.
 
Sasa maana ya kusaidiana ni nini!?

We ndo kiazi mviringo tena.
Ndo jamii yenu mnataka msaidiwe tu halafu nyie kusaidia mkono birika pumbufu kabisa.
una ID ngapi ?

kusaidia ni hiari sio lazima, ukisaidia ili utegemee usaidiwe na yule uliyemsaidia , inabidi upimwe mkojo na akili
 
Nahis rafiki yako wa damu kutembea na mpenz wako ndio inauma zaidi. Ila pole mzee baba
 
Yawezekana ulihisi ni rafiki yako kwakuwa mlikuwa karibu na alifaidika nawe, kumbe mwenzio kwake wewe sio rafiki. Lakini pia moyo wa kutoa sio kila mtu anao, wengine uchoyo uko damuni.
 
Huyo ni wa kutema. achana naye
 
Yawezekana ulihisi ni rafiki yako kwakuwa mlikuwa karibu na alifaidika nawe, kumbe mwenzio kwake wewe sio rafiki. Lakini pia moyo wa kutoa sio kila mtu anao, wengine uchoyo uko damuni.
huyo jamaa amezidi aisee
 
Watu wote tuko hivyo kama alivyo huyu unayemwita rafiki yako. Hata mimi hapa nilipo, ningeweza kufanya kama alivyofanya huyu mtu. Wapende watu bila kuwachukulai kuwa ni marafiki ama la, expect the least or nothing at all from everyone you regard as a friend or an acquaintance. That way you will live your life, a wonderful life.

Hayo uliyofanyiwa na huyo mtu hata mimi hapa nilipo sioni shida yoyote ya kukufanyia hivyo, ningeweza kukufanyia hata mimi.

Wapende watu but be very careful with the way you deal with them. Live your life hizi marginals zisizokuwa za msingi achana nazo kabisa
 
Mkuu kiingereza hicho [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
una ID ngapi ?

kusaidia ni hiari sio lazima, ukisaidia ili utegemee usaidiwe na yule uliyemsaidia , inabidi upimwe mkojo na akili
Kuna mfumo unaitwa mutualism na parasitism.
Mutualism maana yake wote mnafaidi Katika mahusiano au urafiki wenu.
Leo ukipata tatizo mm nikusaidie kkuinua na ikitokea na mm nimepata tatizo unisaidie maisha yaende.
Parasitism ni sawa na kupe kwenye ng'ombe, yeye awe anamnyonya mwenzake wakati yeye hapati chochote zaidi ya maumivu.
Jifunze vzr kitu kinaitwa association halafu tofautisha na kumsaidia mtu njiani at once huyo huwezi tegemea na yeye akusaidie tunazungumzia mtu mliyepo jiran au ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…